Black Jesus
JF-Expert Member
- Mar 7, 2008
- 256
- 10
Hicho kituo kimoja ndicho kitaipatia CCM ushindi wacha tusubiri filimbi ya mwisho.
Nini nilikiandika jana kisome hapo juu na matokeo yake nini kimetokea,Black jesus never be wrong
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hicho kituo kimoja ndicho kitaipatia CCM ushindi wacha tusubiri filimbi ya mwisho.
Hao wakala wa CHADEMA wamepotelea wapi? Je wamefichwa na CCM baada ya kununuliwa? Au CHADEMA wamewaficha ili wapate sababu za kulalamika?
Inamaana CHADEMA imeshindwa ,kule mwanzo nilisoma na kuona watu wengi wanaisakama CUF, sijui kwa nini ,ila hisia zinaonyesha kuwa CUF ni tishio hata katika vyama vilivyo upande wake wa upinzani.
Baada ya kukaa na kuratibu kinachoendelea wameivamia CUF matokeo yake CCM anaondoka na kapu la kura taratibu na kulikarabati.
Hivi tunaposema matokeo ya Uraisi ,Wabunge na Wawakilishi kule Zanzibar huwaga yanabadilishwa na tume ya uchaguzi mlizani tunatania ?
Mnapoambiwa CUF mara zote inashinda uchaguzi wa Zanzibar kuanzia wa Uraisi mpaka wa Udiwani ,mnaonana mnadanganywa ,CUF ni wagonvi ,walafi wa madaraka au sio ?
Basi kwa taarifa yenu CCM imepima wizi wa kubadilisha matokeo kwa upande wa Tanganyika (Hakuna Tanzania Bara kwenye makubaliano ya Muungano,mnielewe) hivyo kipimo hicho ndicho kitakachotumika ,na kwa wale waliozoea kutokuwa tayari kwa lolote kwa kuogopa kuwa damu itamwagika basi msahau ushindi .
Kuiong'oa CCM kunahitajika nguvu za ziada kushinda zilizotumika Kenya au Zimbabwe maana hao akina Zimbabwe na Kenya ,Tz ni baba yao ,sasa ikiwa watoto wamekurupushwa kwa mbinde ,je CCM Baba ,si mnawasikia wakiimba CCM baba ,baba uyoo ! Akili kichwani mwenu ,ila kwa kuongezea akiba ya maneno ,vyama vya upinzani upande wa Tanganyika zi lazima viwaandae wanachama wake kwa lolote lile na sio lelemama kutegemea ushindi wa kugaiwa.
Zanzibar CUF imefanikiwa kuwaandaa wanachama wake ,zoezi la kuwakusanyanya wananchama wake kudai haki yao kwa mass people(Power of the people) pale Mjini Unguja lilifanikiwa (Ule ulikuwa mwito tu wa kujaribisha kama watu wanaweza kuitikia na nyote mmeona na CCM wameona) ,sasa pale palikuwa hapana mipango yoyote ile zaidi ya CUF kuipima nguvu yao kwa siku zijazo ,sasa kama kukiwa na mipango watu hawatakusanyika tena makao makuu bali itakuwa kujigawa kila kona na pembe ya Zanzibar Pemba na Unguja ,ikiwa Pemba peke yake ,serikali ilibidi iagizie polisi kutoka DSM ,je ikichafuka Zanzibar nzima ?
Ni lazima wananchi waandaliwe kupambana kikweli na sio ya anao anao ! Siku zote atakuwa nao CCM kama upinzani nao haukujiandaa kucheza rafu ,tena rafu za kweli ili kumng'oa Baba 😀
Mukasa keshatangazwa mshindi. Hakuna sababu ya watu kuumia sana au kuwa na anza na hisia ya kuona kuonewa. Japo kuwa hisia hizo zina msingi uhalisia unatulazimisha kukubali kuwa njia ya kuelekea demokrasia haiwezi kuwa mteremko hivyo.
Sio lazima kuwe na tume huru wala nini wafanykazi wote wakiacha kazi na mtanzania yoyote akakataa kazi mpaka ccm itakapong'oka mbona ni tiba tena ya week tu
Ndugu yangu hadi hapo, kwakweli umechangia very low.
Kama unadai kwamba wazee wako vijijini walikutuma ukasome upate elimu kisha uje kuwasaidia kuondokana na hali duni, na hapo juu umeonyesha kuwa umesoma kama ulivyotumwa na wazee wako.
Lakini ghafla unapogeuka na kutoa hoja dhaifu kama hii, nabaki kuwaonea huruma hao wazee wako huko kijijini. Watakuwa wamekula hasara kama hali yenyewe ndio hii.Tangu mwanzo nilikuwa nasoma post zako naona kama una kitu cha maana unataka tukifahamu toka kwako, pamoja na mapenzi yako ya dhati kwa ccm, lakini kwa ushauri huu, umejishusha mno. Pole sana yego mwamba.
Mkuu
mimi nafikiri njia nzuri ya kumkoti mtu ni ukoti yote harafu upigilie mstari sehemu panapo kupa duku duku ,hii tabia nafikri sio nzuri sana ya kunukuu nusunusu.
Mimi nimesema kama kweli mnawafuasi wengi watoweza kumwaga damu yetu Basi hiyo nawashauri si njia sahihi nakama mnaweza hilo basi wito kwangu kwenu ni bora mhamasishe wafanyakazi na watanzania wagomee kufanya kazi si mnaungwa mkono na watanzania wanyonge nadhani mtafanikiwa zaidi kuliko kumwaga damu mkuu wangu.
Angalia UKRAINE walifanya nini kama kweli mnaungwa mkono kisawa sawa TUME HURU si hoja kabisa itakuja yenyewe tu ,hebu waambieni wafuasi wenu wote wagome kwenda kazini si wafuasi wenu ni watanzania wanyonge ama vipi? serikali itatulia yenyewe.
Kinyume chake hamna wafuasi mnaotaka watu wawaamini mnao na wala huko kuonewa mnakoku amplify hakuko ktk magnitude mnayotaka tuamini.
Fafanua hii sijaelewaCHADEMA mnapofanya tafakuri ya kushindwa huko B'mulo pia tafakarini sana mwenendo wa mpiganaji wetu mmoja mashuhuri ndani ya chama chenu- nadhani anatumikia mabwana wawili- ushahidi unaendelea kukusanywa ikiwa tayari tutaumwaga hapa na pia wengine wenye kulijua hilo karibuni
Sema ni nani hapa ni ni ukweli na uwaza na sisi kama ni tuhuma ni za kweli tutajua kama ni kweliCHADEMA mnapofanya tafakuri ya kushindwa huko B'mulo pia tafakarini sana mwenendo wa mpiganaji wetu mmoja mashuhuri ndani ya chama chenu- nadhani anatumikia mabwana wawili- ushahidi unaendelea kukusanywa ikiwa tayari tutaumwaga hapa na pia wengine wenye kulijua hilo karibuni