Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

kama hayo matokeo ya Invisible yana ukweli sasa tuelezwe hayo CHADEMA wanayosema yalikuwa yamebadilishwa ni ya vituo gani? na je waliosaini hayo yasiotambuliwa na CHADEMA ni nani? ni hao hao walio saini yanayotambuliwa au nao CHADEMA wanarushiana changa za macho wenyewe kwa wenyewe?

Tunahitaji maelezo ya kina kwa hao wakuu wa CHADEMA. Kimsingi ninahisi humo ndani ya CHADEMA kuna watu mamluki wanaosaidia kufanikisha hujuma hizi za kisiasa. Kwakweli Upinzani usipolipatia ufumbuzi tatizo hili ama kwa hakika hawata kaa washinde changuzi zenye changamoto kama hizi na bahati mbaya sana hakuna jimbo lililo rahisi kushinda zaidi ya hayo mawili ya karatu, tarime na kigoma kaskazini ambayo nayo tushaanza kusikia vitisho kuwa hata hayo 2010 yanaweza kuchukuliwa vile vile.

Kwa kweli kazi ya ziada inahitajika.

Kibaya kingine watanzania wakishapiga kura huwa hawana mpango na matokeo. hilo wanawaachia wanasiasa waumane wenyewe kwa hiyo hata tukidhulumiwa we dont care na ndo maana turnover ya wapiga kura inazidi kushuka siku hadi siku.

Kwa kweli mabadiliko yahitaji uvumilimu na bidii ikiambatana na umakini kwa kila kinachotokea kwenye zoezi la upigaji kura.
 
Mkuu Invisible,

.....

Binafsi ningependa kweli kujifunza CCM wanatumia mbimu zipi kuiba? Hivi hakuna wana CCM hapa wanaotaka ku spill the beans? Yaani vyama vya upinzani mmeshindwa kabisa kuiba siri za CCM?

Kwa kuanzia tu,

Wanatangaza yule wanayetaka ashinde ...... huku wakiwa wamezungukwa na FFU.
 
Kwa kuanzia tu,

Wanatangaza yule wanayetaka ashinde ...... huku wakiwa wamezungukwa na FFU.
Wewe upo wapi?? unshindi gani kwani hujui kuwa mshindi amepatikana na CCM ndiye tume imemtangaza mshindi??
 
Bona hapo hapo Kabuye alichukuwa kutoka TLP,hata hivyo bado hujajibu swali.
Ni kitu gani unaamini kwamba kuna wizi umetokea.?Wanaoleta habari za wizi kumbuka nawo wako biased na chama chao.Sasa ni kigezo gani kinatumika kuutambuwa wizi ?

Waliko B'mulo kuna vurumai yoyote kati ya wananchi na ffu?? ama vurumai iko kwa viongozi wa chama kutoka dar?

Kwani CCM walimpa nafasi Kabuye siwalilishika jimbo kwa kuweka pingamizi mbona unataka kutufanya hatujui mpaka mzee wa watu anafariki bado walikuwa wameona wamemkomesha kipenzi cha wanachi ,watahadhalishe ni vizuri wasome nyakati mwisho wa siku watakuja kujikuta wakiondoka na wasigeuke nyuma nchi hii watakuja kuwa inavyofanana wanadhani yanayo watokea watu wengine hapa yatawashinda wakati wanashindwa kusimamia utashi wa wananchi
 
Wewe upo wapi?? unshindi gani kwani hujui kuwa mshindi amepatikana na CCM ndiye tume imemtangaza mshindi??

Samahani sana mkuu kama nimeji(ku)changanya. Nilikuwa ninajibu swali la Mtanzania (member wa JF) aliyetaka kujua kuwa ccm wanatumia mbinu gani kuiba kura.

Mie nikamjibu kuwa:

CCM wanashindwa uchaguzi, kisha wao wanamtangaza mgombea wao kuwa ndiye mshindi (kitu ambacho unaweza kuwa unakiongelea wewe hapo juu).
 
Invisible,

..jamaa aliyekupa matokeo mwanzo ana maelezo gani kutokana na haya yaliyojiri?

..sasa Chadema wana maelezo gani kwa matokeo haya?
 
Ukitaka kumshinda CCM mpigilie 60% kwenda mbele, mpaka aone aibu hata kuiba.

Huu ushindi wa 55% anageuza kibao tu. Muulize Seif.
 
Muda mchache uliopita nimesikiliza taarifa ya habari toka TCB-TV ambapo CCM imetangazwa kushinda kiti cha Ubinge-B’mulo. La kusikitisha na kushangaza matokeo rasmi hayajatangazwa hapa B’mulo. Hakuna kauli yoyote Zaidi ya mahojiano yaliyofanywa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Radio Kwizila ya Ngara ambapo Mkurugenzi alikiri CHADEMA kuelekea kushinda.
Sasa TBC inapomtangaza mgombea wa CCM kushinda ni kwa kura zipi? Zilizopigwa kupitia TV au mabox ya uchaguzi? Yawezekana kulikuwa na uchaguzi mwingine unaendeshwa kupitia TV!
Mkulu Invisible nawe uthibitisho wa matokeo rasmi umeutoa wapi?
Kwa sasa kinachofanyika ni propaganda. Invisible kuwa makini usijekuwa sehemu ya “Propaganda Pima Upepo Tutekeleze Letu”
Invisible anatakiwa awajibike kwa hili,maana taarifa ya awali ilionekana kama taarifa Rasmi kuwa CHADEMA imeshinda B'muro Magharibi na watu kibao wakajitokeza kuipongeza CHADEMA..Invisible tuombe radhi wana JF mkuu..Pia napendekeza heading ya hii thread iwe ni: CCM yashinda Biharamuro Magharibi....
 
Jamaa walikuwa wanashangilia.....ushindi....ila limebuma duu haya ila kama ccm hawakutilia nguvu kwenye hii ngoma
 
Mbowe, Slaa na Zitto washapanda ndege na kujirudia Dar, wale akina mwenzangu mie Mnyika, Lema, Tumbo wanachezea vumbi hivi ndani lori la Chadema ado ado Dar mpaka baada ya wiki moja!
 
Mbowe, Slaa na Zitto washapanda ndege na kujirudia Dar, wale akina mwenzangu mie Mnyika, Lema, Tumbo wanachezea vumbi hivi ndani lori la Chadema ado ado Dar mpaka baada ya wiki moja!

Mwenzako?
 
Du! Wandugu mbona mwanichanganya... nani mshindi?

Kile chombo cha habari za propaganda za kifisadi za serikali ya ccm - TBC1 kimeshamtangaza mshindi. Ukiwa unakiamini hicho, basi mshindi utakuwa umemjua tayari.
 
Swala linalozungumzwa hapa sio CCM kushinda, Swala ni wizi wa kura.
Mkuu maneno yako haya ni mazito sana,hope ulikuwepo B'muro,haya fanya utujuze basi huo wizi wa kura ulikuwaje?,tufumbue macho kidogo ili tujue hawa CCM wanavoiba hizo kura
 
Mkuu maneno yako haya ni mazito sana,hope ulikuwepo B'muro,haya fanya utujuze basi huo wizi wa kura ulikuwaje?,tufumbue macho kidogo ili tujue hawa CCM wanavoiba hizo kura

Mkuu soma matokeo hapo juu mwanzo wa thread, kilicho fuatia ni kushikilia matokeo yaani kuto yatangaza huku wakiendelea kubadilisha kura, then ni kuita FFU kuzunguka, then ni Kivuiti wa Tanzania kutangaza aliye shindwa kuwa mshindi, case closed

But for sure these thick skinned people , they will one day pay for what they are doing!
 
Kwa kuongezea hapo, wakimaliza kuita FFU, vyombo vya habari za kifisadi na propaganda za kifisadi za ccm (kama TBC1) vinaambiwa kutangaza hayo matokeo yao ya kifisadi.

Miafrika kuanzia Kenya hadi Zimbabwe yote ndivyo ilivyo tu. Usanii hadi visogoni. Na kisha wanakuja hapa kupretend kuwa hawajui kilichotokea.
 
Mkuu soma matokeo hapo juu mwanzo wa thread, kilicho fuatia ni kushikilia matokeo yaani kuto yatangaza huku wakiendelea kubadilisha kura, then ni kuita FFU kuzunguka, then ni Kivuiti wa Tanzania kutangaza aliye shindwa kuwa mshindi, case closed

But for sure these thick skinned people , they will one day pay for what they are doing!

Wapi Pasco? Hali ikoje huko? Lakini Rwabungiri alichotaka mwenzetu ni ushahidi. Kwa kweli kwa hili ushahidi ni wa mazingira mpaka sasa na kwa waliokuwa huko, wanashangaa kabisa kusikia CCM imeshinda. Wanashangaa matokeo yaliyosainiwa na mawakala wa CCM yamekataliwa na kuwekwa mengine katika vituo zaidi ya vitatu ambayo yamebadilika na kubadili sura ya matokeo ya awali. Huu si mchezo mzuri na haujengi.
 
Back
Top Bottom