Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena ukichukulia kuwa hao wazee wa vijijini bado wana mpango wa kutuma vijana zaidi shuleni?!
Ndiyo wazee wenye hekima wanatuma vijana wao wakapate elimu na kuelimika ili waje wawakomboe na umasikini kwa njia sahihi ,najivunia kutumwa na wazee maana fikra za umwagaji damu ni mwiko kutokana na elimu bora.
Fikra ya umwagaji damu yatoka ka mwovu na mawazo ya manyanga'au .
Mkuu wewe una akili sana na inaonekana umeelimika sana. Wazee wa kijiji chako wana bahati sana kupata kijana mwenye akili kama wewe. Yaani una akili kuliko team nzima ya CHADEMA (wazee Mtei na Makani inabidi wakutafute ili uwape shule).
Hongera sana kwa elimu nzito unayotoa hapa.
Kama CUF ndio nyinyi- nasema wapumbavu- Lile lilikuwa ni kosa kubwa sana mlilolifanya CUF - Unaandaaje wafuasi wachezee Dola na wapigwe risasi- Jee unawafanya muhanga - Muhanga ni wa nini Tanzania hii? Umeshindwa uchaguzi. Taratibu si zipo?- dai haki ya-sawa. sasa wewe unawataka wa Chadema wa Biharamulo wakamchezee OCD. Ole wao!!!Zanzibar CUF imefanikiwa kuwaandaa wanachama wake ,zoezi la kuwakusanyanya wananchama wake kudai haki yao kwa mass people(Power of the people) pale Mjini Unguja lilifanikiwa ?
Kama ni kosa basi wao watakuwa sio wa mwanzo ni waendelezaji tu na ujuaji wako na huyo DC ikiwa uma utasimama kidete basi hakuna cha OCD wala cha RPG(C) wote watatafuta pa kukimbilia na wenyewe wanalielewa hilo ukizingatia polisi mmoja anasimamai watu 5000 au zaidi hapa Tz, ushahidi upo ,wacha vitisho wakati wa kuogopana umepitwa na wakati.Kama CUF ndio nyinyi- nasema wapumbavu- Lile lilikuwa ni kosa kubwa sana mlilolifanya CUF - Unaandaaje wafuasi wachezee Dola na wapigwe risasi- Jee unawafanya muhanga - Muhanga ni wa nini Tanzania hii? Umeshindwa uchaguzi. Taratibu si zipo?- dai haki ya-sawa. sasa wewe unawataka wa Chadema wa Biharamulo wakamchezee OCD. Ole wao!!!
Binadamu kamili hawezi ongea umwagaji damu ktk state iliyopo TZ
Tatizo lako wewe -Hebu fafanua nini huo Umma. na hiyo nguvu ya Umma. Unafikiri kule Biharamulo hakuna Umma wa CCM. sasa kama waingie uwanjani na kumtisha OCD nani ni wengi. Wa Chadema au wa CCM (kwa kule Zenj huwa tunauliza ni wa CUF au wa CCM) . Acha fikra mgando ndugu yangu. Tanzania ni nchi ya amani . Wazee wetu wametuachia hiyo na itabakia hivyo milele. Chadema kashindwa si ende Korti yakhe!!!Kama ni kosa basi wao watakuwa sio wa mwanzo ni waendelezaji tu na ujuaji wako na huyo DC ikiwa uma utasimama kidete basi hakuna cha OCD wala cha RPG(C) wote watatafuta pa kukimbilia na wenyewe wanalielewa hilo ukizingatia polisi mmoja anasimamai watu 5000 au zaidi hapa Tz, ushahidi upo ,wacha vitisho wakati wa kuogopana umepitwa na wakati.
Matokeo si sahihi si nenda kayapinge. Fuata taratibu za Kiungwana zilizowekwa. Unataka kuleta fujo umchezee OCD. Wewe Bwana -hata huko Marekani Dola haichezewi. Watu wakishindwa uchaguzi huenda katika vyombo vilivyowekwa kudai haki yao, na wako wanaofanikiwa. Lile la Zanzibar usilitolee mfano. Lakini Dola yoyote ile isingekubali upumbavu kama ule -ingemwaga risasi tu. sasa matokeo yake tunasikitika sote - Mungu tuepushe na uwandawazimu kama ule.Inaonekana mchezo anaocheza CCM mnaushangilia na kuuona ni mchezo .
Kwa sababu zipi hizo ambazo zitamfanya mtu asiongelee umwagaji damu ,kwani sababu za umwagaji damu ni zipi hata mtu asiziongelee ?
Kwa kukusaidia tu ,ni yepi yaliopelekea umwagaji damu Kenya na ZImbabwe na hata Zanzibar ?
Inaonekana mchezo anaocheza CCM mnaushangilia na kuuona ni mchezo mwema ,watu hawawezi kukubali kuwa matokeo ni sahihi na hayabadilishwi kwa kuwa tume iliyokuwepo inapigiwa makelele ni na inatokana na Chama kimoja cha CCM.
Hata kama matokeo yakijumuishwa na kuonesha Chadema au TLP ni mshindi ,Tume inabaki na veto ya kumtangaza mshindi na sheria zinasema wakishatangaza ndio hivyo hivyo ,mwenye malalamiko aende mahakamani na huko nako unakutana na CCM wengine ,hivi utategemea haki kutendeka ?
Ukienda kwenye tume ni MaCCM watupu,ukienda mahakamni wamijaa ,polisi ndio usiseme ,sasa kama watu hawakuipigania hali hii unafikiri itaondoka kwa miujiza ?
Hivyo kuingiana mwilini inaonyeshea ni jambu lisilo epukika na halina mbadala ,bado saa na wakati muwafaka tu na haupo mbali.
Habari ndo hiyo..Mtaji wa CCM siku zote uko vijijini.Swali la msingi ujiulize je CHADEMA wana mtandao wa kuanzia kwenye Mashina,Matawi,kata,Wilaya,Mkoa na Taifa kama ilivyo kwa CCM?,vipi kamaw angejiimarisha kuanzia shinani si wangekuwa tishio kwa CCM kuliko sasa??,bado hawajachelewa,muda wanao wa kutosha
Wakulu kila nikisoma hii thread kutoka mwanzoni, presha inapanda sana...yaani kama ni filamu, sterling ameuwawa kabla hata picha haijaisha....ngoja niangalie thread nyingine😕
Kumbe Luteni Kanali Mstaafu Y. R. Makamba alishayajuwa matokea hata uchaguzi bado, na ndo maana wakafanya mikutano yao kivulini, ata hawakujisumbua,wamewaachia chadema wahangaike na mji.Pole mkuu, si we peke yako, kila mpenda haki kaguswa! na kwa hakika idadi ya maadui wa chama cha mafisadi imeongezeka!
Chadema Poleni sana na hongereni, hata kama wamewakivuiti wadau tumeona, na ujumbe wameupata! Keep it up!
Ziara imesaidia sana asante Mkuu.Stand up fight for your rights na ndivyo CUF inavyowashawishi wananchi wake ,sasa ikiwa CHADEMA ni chama cha kubweteka hakina maana kabisa .Haki inalindwa na haki inapiganiwa ,CUF katika kuilinda haki yake imeyakataa matokeo ya Uchaguzi kule Zanzibar na hadi hii leo hawamtambui Raisi wa Zanzibar kama Raisi halali,katika kuilinda haki yao wananchi wamepambana na polisi kule Pemba kupinga vyombo hivyo kutumika na kwa uchaguzi ujao wamekusudia kuwavaa wanaosimamia tume roho kwa roho.
Matokeo ya Uchaguzi mdogo: Rafu Biharamulo
• Mawakala wa vituo tisa vyenye utata watoweka
na Mwandishi Wetu
DALILI zinaonyesha kuwa, matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Biharamulo Magharibi, yaliyompa ushindi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Oscar Mukassa, yana kasoro, Tanzania Daima imebaini.
Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka Biharamulo zinaonyesha kuwa, matokeo hayo yamepokewa kwa hali ya mshangao na kutoamini na wananchi wa jimbo hilo, ambao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa kampeni, upigaji kura na uhesabuji wake.
Kwa mujibu wa habari hizo, kikubwa kilichosababisha mshangao huo ni kuibuka kwa mzozo wa wazi wa matokeo kati ya vyama vikuu viwili, CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambavyo kila kimoja kimejitokeza na kudai kuwa kimeshinda uchaguzi huo.
Taarifa ambazo wakazi wa Biharamulo walikuwa nazo hadi kufikia jana asubuhi, ambazo zilitiwa nguvu na habari zilizoandikwa na baadhi ya magazeti, zilikuwa zikionyesha kuwa, mgombea wa CHADEMA, Dk. Anthony Gervas Mbassa, alikuwa akielekea kushinda katika kinyang'anyiro hicho.
Hata hivyo, matumaini hayo ya CHADEMA ambayo yalichagizwa na taarifa za ushindi zilizosambazwa na viongozi wa chama hicho walioko Biharamulo, zilianza kuzimwa taratibu kuanzia asubuhi hiyo hiyo ya jana.
'‘Wakati tukisubiri mgombea mbunge wetu atangazwe kuwa ameshinda baada ya kuwa tumekusanya matokeo kutoka katika vituo vyote vya uchaguzi kutoka katika kata zote nane, tulianza kusikia taarifa za wanachama wa CCM, nao wakishangilia kuwa wameshinda kwa tofauti ya kura 2,000 kabla ya idadi kupungua hadi 1,500 na mwishoni kuambiwa kwa kura 800.
'‘Taarifa hizi zilianza kututia wasiwasi sana, na tulipokuwa tukipitia matokeo hayo, bado tuliendelea kupata hesabu zilezile kuwa sisi ndio washindi," alisema Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA wakati alipozungumza na Tanzania Daima, jana asubuhi.
Wakati taarifa za kukinzana zikiendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) walionekana kuanza kukusanyika kuzunguka jengo la Halmashauri ya Wilaya ambako ndiko ziliko ofisi za msimamizi wa uchaguzi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mzozo wa kupingana kuhusu nani hasa alikuwa mshindi kati ya vyama hivyo viwili, zilisababisha msimamizi wa uchaguzi huo, kuitisha kikao na viongozi wa pande zote mbili na kujadili kile kilichokuwa kimetokea.
Habari ambazo zilipatikana ndani ya mkutano huo zinaeleza kwamba, wakiwa ndani ndipo ilipobainishwa kuwa CCM walikuwa wameshinda, uamuzi ambao ulipingwa na CHADEMA iliyokuwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu kutoka Biharamulo, Zitto alisema mara baada ya kukutana na mahasimu wao hao, walibaini kuwapo kwa kasoro za uhesabuji kura katika vituo tisa vilivyo katika kata tatu tofauti.
'‘Msimamizi wa uchaguzi amemtangaza mgombea wa CCM kuwa ameshinda. Tumeyakataa matokeo, kwani tumebaini tumeibiwa kura waziwazi katika vituo tisa vya kata tatu ambako kura za CHADEMA zimepelekwa CCM na zile za CCM wamepewa CHADEMA," alisema Zitto kwa masikitiko.
Zitto, mmoja wa wanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa mwepesi kukubali kushindwa kwa chama chake katika chaguzi ndogo ndogo kama zile za Busanda, Kiteto na kabla ya hapo Tunduru, alieleza kusikitishwa na hatua ya msimamizi wa uchaguzi kukataa ombi la CHADEMA la kutaka kura katika vituo tisa vyenye utata kuhakikiwa na kuhesabiwa upya.
Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kutoka Biharamulo kinaeleza kuwa, CHADEMA walianza kupata taarifa za matokeo ya uchaguzi ‘kuchezewa' kutoka kwa baadhi ya maofisa wa serikali waliokuwa katika vituo kadhaa vya uchaguzi.
Zitto alipoulizwa kuhusu ukweli wa taarifa hizo, hakuwa tayari kukubali au kukataa zaidi ya kusema kwamba, walianza kupata taarifa mapema za kuwapo kwa mkakati wa kura zao kuhamishwa na kupewa mgombea wa CCM.
Katika hali ya kustaajabisha, Zitto alisema, mawakala wa chama chao wa vituo vyote tisa vyenye utata, ambavyo hakuvitaja, walikuwa hawajulikani walipo, tukio ambalo linawatia wasiwasi wa kuwapo kwa vitendo haramu katika zoezi hilo.
Wakati CHADEMA wakilalamika, matokeo ambayo yalitangazwa majira ya saa 7:05, mchana jana yanaonyesha kuwa, mgombea wa CCM, ameshinda kwa kura 17,561 (51%) dhidi ya yule wa CHADEMA aliyepata kura 16,700 (48.4%), huku mgombea wa TLP akiambulia kura 198.
Akitoa sababu za kukataa matokeo hayo, ikiwa ni pamoja na kugoma kusaini fomu ya kukubali matokeo, mgombea wa CHADEMA, Mbassa alisema kuwa, matokeo ya kata tatu yalikuwa yamebadilishwa tofauti na walivyosaini wasimamizi wa matokeo na yalivyohesabika vituoni.
Alisema matokeo ya jumla yaliyokuwa yamebandikwa awali katika vituo vya kupigia kura baada ya kura kuhesabaiwa, yalionyesha kuwa CHADEMA ilikuwa imeshinda.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, hali ya mji wa Biharamulo ilikuwa kimya huku askari wa kutuliza ghasia wakiwa wamezunguka mitaani. Licha ya wafuasi wachache wa CCM kushangilia, watu wengine walionekana kuwa kimya katika vikundi wakijadiliana.
Kwa mujibu wa CHADEMA, matokeo yao yalikuwa yakionyesha kuwa mgombea wao alikuwa amepata kura 17,313 wakati yule wa CCM akipata kura 16,682.
Akizungumzia hali hiyo, Zitto alisema kuwa wamekataa kusaini fomu ya kukubali matokeo kwa sababu wanajua kuwa wamechezewa rafu, na kwamba wananchi wa Biharamulo wamenyimwa haki yao ya kumchagua kiongozi.
"Sisi tulijua kuwa tumeshinda tangu jana usiku (juzi) baada ya kuhesabu kura na kuhakikisha hilo, ndiyo maana wafuasi wa CHADEMA walianza kushangilia," alisema Zitto.
Aliongeza kuwa, wamewatuliza wafuasi wao wasionyeshe hali yoyote ya hasira au kufanya vurugu, wala hawataenda mahakamani, kwani wanaamini chama hicho kitafanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
"Tumewatuliza wananchi wasifanye fujo yoyote, kwani walikuwa na jazba. Sisi hatuamini kilichotokea, ndiyo maana ukimya umetawala Biharamulo. Ni vigumu kuamini mchezo uliofanyika," aliongeza Zitto.
Habari nyingine kutoka huko zinaeleza kuwa, wakati matokeo yanatangazwa, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakihofiwa kuwa wangeweza kufanya vurugu, walikuwa wakishuhudia ulinzi mkali wa polisi katika maeneo mbalimbali.
Akizungumzia hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Kapteni mstaafu, George Mkuchika, alisema kuwa, wao walihesabu kura tangu juzi usiku, wakajua mapema kuwa wameshinda.
Alisema walipolibaini hilo, walianza kuwawatuliza wafuasi wao wasishangalie mpaka hapo Tume ya Uchaguzi itakapotoa matangazo rasmi.
Aliitaka CHADEMA kuyatambua matokeo hayo kwani ushindi wao ulionekana wazi tangu awali. "Tunaitaka CHADEMA itambue matokeo hayo, kwani hata sisi tulihesabu kura tangu jana usiku (juzi), tukajua kuwa tumeshinda," alisema Mkuchika ambaye alikuwa akizungumza akiwa jijini Dar es Salaam. Katika taarifa za awali, mpaka zinapatikana hesabu za mwisho kutoka katika vituo vya kupigia kura kukiwa bado kituo kimoja cha Nyabugombe B chenye wapiga kura 394, CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa asilimia 50.6, huku CCM ikiifuatia kwa karibu ikiwa na asilimia 48.8 ya kura zote na TLP ikiwa imejinyakulia asilimia 0.55.
Chadema wamefanya kazi nzuri sana huwezi walaumu, wameibiwa kura matokeo yamebadilishwa tume ya uchaguzi ya jaji Lewis na Fisadi chama wanauwa demokrasia. Bila kufumua tume ya uchaguzi kazi ngumu mbele ipo.Habari ndo hiyo..Mtaji wa CCM siku zote uko vijijini.Swali la msingi ujiulize je CHADEMA wana mtandao wa kuanzia kwenye Mashina,Matawi,kata,Wilaya,Mkoa na Taifa kama ilivyo kwa CCM?,vipi kamaw angejiimarisha kuanzia shinani si wangekuwa tishio kwa CCM kuliko sasa??,bado hawajachelewa,muda wanao wa kutosha