Matokeo darasa la saba 2011 kutangazwa leo

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Taarifa ya habari toka TBC Taifa ya saa tano usiku wa jana imemnukuu naibu waziri wa elimu kuwa matokeo rasmi ya darasa la saba ya mwaka huu (2011) huenda yakatangazwa leo muda wowote. Taarifa hiyo imemnukuu waziri huyo akiwataka watu waliopata taarifa kuwa matokeo yalisha tangazwa kuzipuuza taarifa hizo kwani mpaka sasa matokeo bado hayajatangazwa. Jamani tukae tayari kusikia mavuno ya watoto wetu.
 
Mie wakwangu nishamchukulia fomu St. Francis, hizo za kata mhm?
 

hakuna mavuno hapo ni kata kwa kata kwenda mbele
 
haya sasa..... watu wale xmass na mwaka mpya huku wakijua kuna kupeleka watoto wao, na wadodo zao shule mapema januari.
 
Hivi kumbe kuna mtihani wa darasa la saba. Mi nilijua ni kama mtihani wa fomu tu. Mtoto anafanya mtihani wa gelesha tu, afaulu ama asifaulu anasonga mbele.
 
Mwanangu alivyo kilaza duh nnawasiwasi hata ya kata haitapatikana!
 
Hivi kumbe kuna mtihani wa darasa la saba. Mi nilijua ni kama mtihani wa fomu tu. Mtoto anafanya mtihani wa gelesha tu, afaulu ama asifaulu anasonga mbele.

anasonga mbele kwenye shule za kata.
kama unapenda maendeleo ya mwanao kielimu, unampeleka shule nzuri za binafsi au za mission.
 
darasa la saba la kujua kusoma na kuandika tu , akuna cha ziada, uwezi ajiriwa wala kudhaminiwa katika jamii, ndio maana ukiongea kitu wanakuambia hamna shule pale, darasa la saba, basi kuna haja ya kuwasongesha watz wote elimu ya mwisho iwe Form 6 kama kule zanzibar
 
Hivi hamsomi magazeti wala kusikiliza taarifa za habairi kuwa shule za kata zilitoa wanafunzi bora!
 
Unaandaa kilaza wa baadae??

nishauri nifanyaje.
Kama hajafaulu nisimpeleke St. Francis, akafundishwe na pesa za MoU ili angalau waache kulalama, maana angalau mwislam mwenzao(ingawa nakula Noah) nimefaidika na Mfumu Kilisito.
 
Mambo tayari toka saa 10:00jioni hii. Ufaulu wapanda kwa 4.7%. Endelea kufuatilia zaidi ndani ya mtandao huu wa Jf. Source LittleX
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…