Brightman Jr
JF-Expert Member
- Mar 22, 2009
- 1,224
- 234
Taarifa ya habari toka TBC Taifa ya saa tano usiku wa jana imemnukuu naibu waziri wa elimu kuwa matokeo rasmi ya darasa la saba ya mwaka huu (2011) huenda yakatangazwa leo muda wowote. Taarifa hiyo imemnukuu waziri huyo akiwataka watu waliopata taarifa kuwa matokeo yalisha tangazwa kuzipuuza taarifa hizo kwani mpaka sasa matokeo bado hayajatangazwa. Jamani tukae tayari kusikia mavuno ya watoto wetu.