matokeo form 4: meya bukoba afanya utapeli

Joined
Mar 5, 2009
Posts
95
Reaction score
32
Matokeo ya kidato cha nne yalitoka hivi majuzi 2013 shule ya sekondari PEACE inayomilikiwa na meya wa bukoba bw. Anatori amani ilishika nafasi ya pili kimkoa ambapo watahiniwa 213 walifaulu na mmoja akkifeli. Lakini wanafunzi 72 aliofikiri kwamba wangepata alama za chini aliwatoroshea huko karagwe wakafanya mtihani shule ya sekondari iitwayo Adolec. Sasa ona matokeo ya adolec,kati ya watahiniwa 95 div. 4 wapo 54. walobaki yaani 41 wamepata 0.sasa katika 95 ina maana wanafunzi halisi wa adolec walikuwa 95-72=23 . Hata kama hawa wote wamepata 0 ina maana waliobaki yaani 17 wametokea peace sec. Hii ni baada ya mwaka juzi kufanya huu uhuni mpaka wanafunzi 84 wakafutiwa matokeo na necta. Ajabu hawa vijana wana leaving certificates za peace sec na wengine wamesoma amani tokea std 3 hadi form4.
Viongozi na wahusika wanajua na wako kimya na inaonekana hagusiki.
Sasa ebu amani atueleze hizi mbinu chafu za kuwadanganya wazazi kwamba shule yake inafaulisha ili aendelee kupata wateja na kuua elimu ya hawa watoto ataiacha lini?
Na je hata kwa hili wanamwonea eti kwa sababu ya ukristo wake?
Je hayo ndiyo maendeleo anayotaka kuwaletea wananchi huku akiua elimu ya watoto wao?
Je wazazi kwa nini msimchukulie hatua za kisheria huyu bwana hamuwezi kusimama mkasema inaotosha?
?..............ama kweli elimu yetu inauawa na viongozi wetu pia! )
 
Ngoja nipite haya ya Bukoba yana mambo mengi.
 
upuuzi uloufanya ww ni kuuingiza ukristo,sasa hapo ukristo unaingiaje?we ni mzima kweli wewe
 
Vita vya ukabila na siasa .za Mali taka .za kagera usizilete hapa
 
Hapa swali langu lillikuwa na bado lipo kwa bwana amani maana kila anapoulizwa badala ya kutoa majibu sahihi yeye anaeneza propaganda kwamba anashambuliwa kwa sababu ya ukristo wake.
 
Vita vya ukabila na siasa .za Mali taka .za kagera usizilete hapa
Mkuu ww ni mtu wa ajabu. Mimi siongelei siasa naongelea utapeli wa viongozi wanaowafanyia wananchi huku upande mwingine wakijifanya manabii wa maenddleo yao. Nakushauri ukifanyie utafiti hicho nilichoandika hasa kuhusu kuficha wanafunzi kisha ulete yako hapa, vinginevyo na ww utakuwa walewale badala ya kujibu hoja mnakimbilia majibu mepesi mara oh ni siasa chafu , oh ni udini. Mkuu hili ni jukwaa la elimu na tunajadili elimu si huo upuuzi.
 
Kiukweli huyu baba si mara ya kwanza wala ya pili huwa ndo utaratibu wa hiyo shule cha ajabu wazazi wako kimyaaa
 
Mbona unafiki wa wahaya unazidi?
Matokeo ya kidato cha nne yalitoka hivi majuzi 2013 shule ya sekondari PEACE inayomilikiwa na meya wa bukoba bw. Anatori amani ilishika nafasi ya pili kimkoa ambapo watahiniwa 213 walifaulu na mmoja akkifeli. Lakini wanafunzi 72 aliofikiri kwamba wangepata alama za chini aliwatoroshea huko karagwe wakafanya mtihani shule ya sekondari iitwayo Adolec. Sasa ona matokeo ya adolec,kati ya watahiniwa 95 div. 4 wapo 54. walobaki yaani 41 wamepata 0.sasa katika 95 ina maana wanafunzi halisi wa adolec walikuwa 95-72=23 . Hata kama hawa wote wamepata 0 ina maana waliobaki yaani 17 wametokea peace sec. Hii ni baada ya mwaka juzi kufanya huu uhuni mpaka wanafunzi 84 wakafutiwa matokeo na necta. Ajabu hawa vijana wana leaving certificates za peace sec na wengine wamesoma amani tokea std 3 hadi form4.
Viongozi na wahusika wanajua na wako kimya na inaonekana hagusiki.
Sasa ebu amani atueleze hizi mbinu chafu za kuwadanganya wazazi kwamba shule yake inafaulisha ili aendelee kupata wateja na kuua elimu ya hawa watoto ataiacha lini?
Na je hata kwa hili wanamwonea eti kwa sababu ya ukristo wake?
Je hayo ndiyo maendeleo anayotaka kuwaletea wananchi huku akiua elimu ya watoto wao?
Je wazazi kwa nini msimchukulie hatua za kisheria huyu bwana hamuwezi kusimama mkasema inaotosha?
?..............ama kweli elimu yetu inauawa na viongozi wetu pia! )
 
Kiukweli huyu baba si mara ya kwanza wala ya pili huwa ndo utaratibu wa hiyo shule cha ajabu wazazi wako kimyaaa

mi sioni tatizo hapo,hiyo ni tekiniki ya mchezo tu,ni biashara tu,kama wanafunzi wamesomea kwenye shule yake,kilichobadilika ni kituo cha mtihani tu,hakuleti tofauti katika ufaulu wa mwanafunzi
 
Binafsi nimesomea pale tokea chekechea (kabla ya kuihamishia kiteyagwa) hadi form 4.. 2009.
Nikweli nimeshuhudia hki kitu kikiwatokea vilaza tuliokuwa tnasoma nao.. Na walipelekwa kwenye shule hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom