Matokeo Kidato cha 4 ni batili

Matokeo Kidato cha 4 ni batili

PCGAMES

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
782
Reaction score
1,157
Tusiwe tunalaumu bila kufahamu jambo lenyewe kiundani.Kweli alieshiba amjui mwenye njaa. Matokeo ya mwaka jana ni batili kwa sababu hauwezi ukapandisha alama za wahusika bila kumjulisha au kumtaalifu muhusika mwenyewe, kuanzia wanafunzi, walimu, wazazi na wananchi wote kiujumla. Hizo alama za juu za 4m 4 kiukweli zimewaumiza wanafunzi wengi kiasi kwamba hadi wengine wamepoteza maisha yao kwa uchungu, hadi mwanafunzi kuamua kupoteza maisha yake inamaana hizo hazikuwa alama alizostaili kupata na ikumbukwe kuwa kabla ya mitihani ya kitaifa huwa na maandalizi kama vile mitihani ya moko na mingineyo sasa huko kote matoke yalikuwa ya kawaida then uje kupata matokeo mabaya ghafla kisa mijitu michache imekaa wao wenyewe na kujipangia kwa manufaa yao wenyewe sasa hii ni haki kweli? Hakukuwa na maandalizi yoyote kwa watahiniwa wala taarifa yoyote kuhusu kupandishwa kwa alama za mitihani sasa huoni kuwa haki haijafanywa hapo kwa wahusika? Mtahiniwa anafanya mtihani darasani huku kichwani kwake akiwa na mbinu ya kuvuka alama za ufaulu zilizo zoeleka alafu yanatoka majibu yake mabovu, wewe unafikiri atachukua uamuzi gani na ukizingatia anauwakika wa kufaulu coz kwake yeye kufaulu sio kitu kigeni. Alafu baadae unakuja kuambiwa alama zimepandishwa. Jamani kwa upeo wangu hii haijakaa sawa na Necta hawawezi kukubali kirahisi kushusha hizo alama coz lazima baadae itajitokeza hoja ya kuwataka wao wajieleze kwa nini walipandisha alama bila taarifa kwa wahusika? Na ukizingatia kuna wanafunzi wamepoteza maisha kwa ujinga au upuuzi wa watu wachache. Fikiria unafikiri nini kitaendelea hapo? Na hilo ni suala moja tu, kuna mambo mengi nayo yaliyochangia matokeo kuwa mabaya mojawapo ni usahihishaji mbovu wa hiyo mitihani so yote hayo Necta watatakiwa kujieleza. Necta pale kuna mapungufu makubwa miaka kibao ila hawezi kujishtaki wenyewe badala yake watajisafisha kwa njia yoyote ile, moja wapo ni hilo la upangwaji upya wa matokeo.
 
punguza jazba nili upate kuelewa zaidi. skuzote kutafakari jambo na kulifanyia uchunguzi wa kina ni muhimu kabla uja weka suluhu ya unacho kitarajia

watanzania wengi tunapenda kupata matokeo mazuri kwakilajambo huku tukiwekeza nguvu kidogo kwajambo husika.
umetoa mfano mzuri sana hivi matokeo yamoko ya mwaka jana katika wilaya, mikoa na kanda tofauti tofauti ulipatakuyaona, kuya chunguza na kujua undani wake? ntakupa mfano wilaya ya sengerema nzima hakukua na A ya somo lakingereza wala B ya somo hilo. marks zao zilianzia c tena ile ya mwisho, wengi walikua na f zakutosha tu.
ukienda kwenye hesabu, kiswahili, masomo yote ya science kwa ujumla tatizo lili kuwa kubwa sana. tulijaribu kulinganisha ufaulu huo na wilaya zingine kama vile ilemela, magu, nyamagana ingawa kila wilaya ilifanya mtihani wake, bado tatizo lilikua ni lilelile. ndio maana ukiwauliza bàdhi ya wàlimu wakuu washule nyingi za kata hasa wa mkoa wa mwanza hawashangai matokeo haya.

hali halisi ya ufaulu wa mwanafunzi anayeifahamu kwanza ni mwanafunzi mwenyewe na pili mwalimu lakini tatu ni mzazi mwenyewe ambae ndio anaishi na mtoto wake nyumbani.

uwezi sema matokeo ni batili kwakuwa wewe hukusahihisha hiyo mitihani. na kama unge sahihisha belive me usingeweza kutoa hicho ulicho kisema hivi sasa.
kama kweli unaamini unacho kisema hebu neda shule hizo za kata omba matokeo yao ya mock then linganisha na haya ya necta, utagundua tofauti ni kidogo sana. utakuta tu devision three ni nyingi kidogo ila huko kwenye ziro ni vile vile.

tatizo tupo kama timu yetu ya mpira, maandalizi hafifu alafu tunataka wrld cup. that is noncence. kama kweli umefanya uchunguzi hawa unao wlalamiki matkeon batili je unajua ufaulu wao wakuingia form three? unajua walipitaje hilo dara?

tazama tabia zao na mienendo yao we unawaona walikua nasifa zakuitwa wanafunzi? huku kuna shule inaitwa miama, igogo, kirumba secondari na nyingine nyingi tu utakuta wanashinda mitaani toka hasubuhi mpaka jioni. daftari hawana wapo wapo tu na jamii ina waona haisemi kitu mwisho wasiku mnataka wafaulu?

nakupa siri moja hebu anza kuulizia hawa watakao fanya mtihani ujue wakoje kitaaluma, kwa sisi tuliopo kwenye hii tasnia tumesha jua kuwa afadhali ya wamwakajana wanawża fanyiwa hata standardazation ila hawa sasa kazi ipo!

badala ya kutafuta cheap answers hebu tuji tathimini je ni kweli wanapaswakufaulu kwa kiwang otulicho dhania kwa kiwango hiki cha usereous ness tulicho wekez kwenye elimu yetu?

rudi tena huko chini chunguza utapata majibu tu. wazazi hatuoni umuhimu wa kuwafuatilia watoto wetu shule kujua maendeleo yao, wanafunzi ndo hawa wasikuhizi utoro, milegezo disco kwa sana, wàlimu wamegoma, serikali hayawausu fanyautafiti hizo ni hisia tu kaka
 
Back
Top Bottom