Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

Halafu ukiangalia tuhuma mojawapo ya kuwa kuna mwanafunzi mwenye number 01197/173 kuwa alifanya arts ila ameongezewa bookeeping na commerce sio kweli jaribu kuangalia utaona, swala la mwanafunzi kupewa marks wakati hakufanya ni ngumu kujua hasa kwa sisi wa nje mpka mwanafunzi mwenyewe athibitishe

Baadhi ya shule zimekuwa zikifanya biashara ya kuvutia wanafunzi wengi kwa kuiba mitihani. Waliokuwa wanafanya hivyo tayari wameshaumbuka kutoka mwaka jana. Tunaomba serikali ijizatiti kuhakikisha huo uzi wanaukaza zaidi. Ni kwa miaka miwili mfululizo tumebaini hicho kitu. Sitataja shule hata moja ila tutafakari!!
 
sijui tunaelekea wap>>>>? always tutabaki baki watu wa chini kwa kila kitu hii ni kashfa na ni aibu kwa Wizara husika, Waziri na Taifa kwa ujumla.
 
Hii habari na uongo ata mimi nimepitia matokeo yao hajaongezewa somo ata moja..Afu hiyo ya kujaziwa grades bila kupiga pepa pia ni uongo. Namba ya shule iliyoandikwa na mtoa mada haipo S01197. Namba ya G/acres ni S1197.

Benito hizo leading zero zisikusumbue. S01197 na S1197 ni shule/kituo kile kile.

----

Inayotia mashaka ni hii hapa ya kuhusu mwanafunzi namba S1197/0148 ambaye hakufanya mtihani.

Msemaji wa NECTA anasema "Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,".

Kwa hiyo amekubali kuwa kuna mtu kapewa alama ambazo si zake. Je ni wangapi wamekumbwa na hali hiyo ya kupewa marks ambazo si zao?
 
Benito hizo leading zero zisikusumbue. S01197 na S1197 ni shule/kituo kile kile.

----

Inayotia mashaka ni hii hapa ya kuhusu mwanafunzi namba S1197/0148 ambaye hakufanya mtihani.

Msemaji wa NECTA anasema "Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,".

Kwa hiyo amekubali kuwa kuna mtu kapewa alama ambazo si zake. Je ni wangapi wamekumbwa na hali hiyo ya kupewa marks ambazo si zao?

Na huyu mbona hakuna somo lililoongezwa apa
S1197/0173 M 34 FLD CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F
LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F
 

[TD="width: 6%"]
S1197/0173​
[/TD]
[TD="width: 4%"]
M​
[/TD]
[TD="width: 6%"]
34​
[/TD]
[TD="width: 4%"]
FLD​
[/TD]
[TD="width: 58%"]
CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F​
[/TD]

Huyu anasema ameongezewa Book Keeping na Commerce hebu jamani nisaidieni mbona mie sioni hayo masomo hapo juu?

Wala hajaongezewa na amepata 0

Regards,
Jonathan.
 
Alishayataja ile asubuhi na pia akitaja adi no zao za mtihani.
Akasema mwanafunzi wa kwanza kapewa dv iii Uku akiwa hajafanya mtihani na mwengine ni mwanafunzi wa arts lakini kaongezewa masomo ya book keeping na commerce akapa dv ii.
Na wengine 3 pia wamefauru kwa dv iii uki wakiwa hawajafanya mtihani kabisa.Na mmoja kafanya ila kawekewa absent.
Kuna kitu kinaendelea kwenye aya matokeo.
wenye akili ya kufikiri na kudadisi tunalijua hili lilianza tangu 2010.
Baraza linatekeleza sera ya usawa wa kuferi kati ya wakristo na waislam.Na hili mwaka jana lilifanyika bila kificho mwaka hui ndo balaa.yani kama watu dini A walikuwa wanafeli sana baraza lilaambiwa akikisheni iyo ratio inakaribiana na kwa hao wengine.
Ila kiukweli watoto.walisoma na hawakuferi kiivyo.kama aya hauamini basi tusubiri uchunguzi ufanywe alafu uje.
 
Ama kweli Tanzania kila jambo linawezekana, hii inanikumbusha mzee mmoja alimpeleka mwanae kwa DC kulalamika kuwa huyo mwanae alikuwa kati ya waliofaulu darasa la saba wakati alikuwa hajui hata kuandika jina lake. Pengine hata hao waliojinyonga kwa kufeli hayo hayakuwa matokeo yao sahihi, na hii inawezekana kwani mgomo baridi uliokuwa unaendeshwa na walimu mpaka sasa haujaisha na hii inaweza kuwa moja kati ya athari za mgomo huo.
 
S1197/0173 M 34 FLD CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F LIT ENG-F BIO-F B/MATH-F Huyu anasema ameongezewa Book Keeping na Commerce hebu jamani nisaidieni mbona mie sioni hayo masomo hapo juu? uongo tupu
 
Benito hizo leading zero zisikusumbue. S01197 na S1197 ni shule/kituo kile kile.

----

Inayotia mashaka ni hii hapa ya kuhusu mwanafunzi namba S1197/0148 ambaye hakufanya mtihani.

Msemaji wa NECTA anasema "Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,".

Kwa hiyo amekubali kuwa kuna mtu kapewa alama ambazo si zake. Je ni wangapi wamekumbwa na hali hiyo ya kupewa marks ambazo si zao?


Hapana, hukumuelewa vema. Imefafanuliwa kuwa mwanafunzi namba S1197/0148 ambaye amedaiwa na mkurugenzi wa G.A kuwa hakufanya mtihani, alifanya mtihani-lakini jina siyo lililoelezwa. Yaani mwenye namba hiyo siyo aliyeelezwa na mkurugenzi kwa kuwa muhusika wa namba hiyo alifanya mtihani. Hata hivyo, jina alilolitaja mkurugenzi wa G.A halikuwa na namba hiyo ya mtihani, hivyo mkurugenzi inaonesha hajua namba za watahiniwa wake.
 
huyu mtoto ni jirani yangu kule bunju, ni kweli hakufanya mtihani, na yuko shule moja mbeya, nimemuulizia mama yake mzazi kasema naye anasikia kwenye redio anashangaa.
Sawa unachosema je unahakika huyo mwnafunzi ndio mwenye hiyo number maana hapo kuna vitu viwili kuna jina na number. kuhusu jina hilo hata msemaji wa NECTA amekiri kuwa halikufanya mtihani.Ila bado nina wasiwasi na huyo mkurugenzi maana huyo mwingine wa S01197/0173 ambaye amesema ameongozewa masomo sio kweli ingia kwenye hayo matokeo utaona tujitahidi kuwa wafuatiliaji wa mambo na sio kuamini kila kitu.
 
Bila mabishano hata Mtanzania wa kawaida kabisa anaona kinachotakiwa hapo ni kuboreshwa kwa maslahi ya mwalimu na si vile ambavyo CWT na Serikali wanavyodai kila siku walimu wadai malimbikizo,nauli za likizo n.k.Kikubwa hapo ni Maslahi ya mwalimu kuboreshwa awe na hali nzuri kiuchumi.Siyo mtu wa kilimo analipwa vizuri,watu wa sekta ya afya malipo mazuri,mbunge posho safi,lakini mwalimu bora liende.Nani atakubali hayo?Fikirieni ugumu wa maisha ulivyo sasa,je mwl ana moyo gani wa kuvumilia hali hiyo?Mi nafikiri tusiwe wanafiki hapa,yaboreshwe maslahi ya mwalimu tuone.Hata hawa CWT TAIFA wanafiki tu mbona hawapiganii maslahi halisi ya mwalimu?Kazi yao kula michango inayokatwa kwenye kila asilimia 2 ya mshahara wa kila mwalimu kila mwezi.Hebu itumike busara ya kawaida kuwainua walimu ili waifanye kazi yao vizuri.Hakuna binadamu anayeweza kufanya kazi vizuri kama hahudumiwi na mwajiri wake vizuri.Hata wazir kama hana mshahara mzuri hawezi kufanya kazi vizuri.Tuliokoe taifa lisizame kwenye TOPE LA UJINGA.
 
lakini jamani wandishi fanyeni kazi kuliokoa Taifa lisiwe la mazezeta, sasa ni halali kabisa kumualika kijana aliefail kuja kwa kipindi cha redio? Ni kipi anawausia wenzake? Kweli crouds mnaboa sna,
 
Matokeo kidato cha nne ‘feki’

• Mkurugenzi Green Acres afichua siri nzito


WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.

Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.

Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.

Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.

Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alama za juu.

Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.

Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika
 
Kawambwa ni aibu kwa jinsia ya wanaume, na hatumtaki katika jinsia ya wanawake pia, kama kungekuwa na uwezekano wa kumuita mama kawambwa!

Ni aibu , mwanaume wa kweli, anakuwa na msimamo, na kufanya kile anachotegemewa kufanya.

Mwanaume suruali, kama umeshindwa kuongoza watu wako. Nin wasiwasi hata na nyumbani kwako matatizo matupu!! Ovyooooo
 
Na mwanaume wa ukweli, anamsimama na haoni aibu.

Ni aibu kwa serikali kuwa na kiongozi mheshimiwa feki mwenye tabia za kike.

Mama kawambwa na binti zake wizarani!
 
WAKATI mjadala wa kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne ukiendelea nchini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume kuchunguza na kutoa mapendekezo ya mfumo bora wa elimu nchini.

Alisema kwa hali ilivyo sasa mtu mmoja hawezi kujifungia ofisini peke yake na kuja na mfumo wa kuboresha sekta ya elimu utakaokidhi matakwa ya jamii.

Lowassa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

Ingawa hakutaka kuzungumzia hoja ya mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia (NCCR- Mageuzi), aliyetaka Bunge liunde kamati kuchunguza udhaifu katika sekta ya elimu na hoja hiyo kutupwa, Lowassa alisema hakuna sababu ya kubishana kama tuna mitaala au la, lakini jambo la msingi ni kuhakikisha tunapata sababu za matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne.

"Sitaki kuzungumzia mjadala wa bungeni huyo anasema hatuna mitaala, serikali inasema tunayo, hoja ya msingi zaidi ni kuangalia hii mitaala ni sahihi, inatufaa? Mfumo wetu wa elimu ni mzuri?" alisema Lowassa na kuongeza kuwa tume itakuja na majibu kama mitaala yetu ni sahihi na kama inatufaa au la.

Akitolea mfano, Lowassa wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, Waziri wa Elimu wakati huo, marehemu Jakson Makweta, aliunda tume kuchunguza mfumo wa elimu na ilikuja na majibu mazuri yaliyofaa kwa wakati ule na sasa tunahitaji tume nyingine kuja na majibu ya wakati uliopo.

"Miaka ya nyuma, Rais Reagan wa Marekani wakati huo, aliunda tume kuchunguza ubora wa elimu inayotolewa nchini mwake na tume hiyo ilikuja na majibu yaliyofanyiwa kazi na leo hii Marekani ina mfumo mzuri na bora wa elimu," alisema Lowassa.

Alisema matokeo ya kidato cha nne mwaka huu, yanasikitisha na kama taifa lazima tupate sababu za hali hiyo na kutafuta ufumbuzi.

Alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kuwa ni pamoja na kuangalia namna gani serikali inawaangalia walimu kwa maana ya mishahara na mazingira yao ya kuishi wawapo kazini.

"Matokeo ya kidato cha nne yamenisikitisha sana maana asilimia 60 ya wanafunzi kupata ziro ni jambo la hatari. Na napenda kumsihii Rais Kikwete kwamba amefanikiwa sana katika sekta nyingine kama barabara, aunde tume kuchunguza sababu za wanafunzi kufeli, lakini kubwa kuliko zote tume hiyo ije na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mfumo wetu wa elimu," alisema Lowassa.

Alisisitiza kuwa hoja ya kutaka serikali iunde tume kuboresha mfumo wa elimu, alipata kuitoa mara kadhaa kwani anaamini Elimu Kabla, Kilimo Kwanza.

"Kila Mtanzania anasema lake, wengine wanasema ni hujuma, wengine wanadai kuna mgomo baridi wa elimu, malalamiko na sababu ni nyingi na njia pekee ya kujua ukweli ni kupitia tume," alisema Lowassa.

Akizungumzia shule za kata alizoziasisi nchini nzima, alisema anajivunia uwepo wa shule hizo hasa kutokana na mwitikio ambao wananchi waliuonyesha wakati anazianzisha.

Alisema matatizo na changamoto zinazozikabili shule hizo ni bora zikatafutiwa ufumbuzi kupitia tume anayopendekeza ianzishwe.
Alisema shule hizo ni mkombozi kwa wananchi wanyonge na zimeleta usawa na ni jambo la kujivunia kwamba ziko kwenye kila kata nchini.
"Hata hivyo kasi ya kuzihudumia shule hizo hatua kwa hatua imepungua na sitaki kumlalamikia mtu, lakini ni bora zikaendelezwa kwa kukabiliana na changamoto zake.
Mbali ya kuzungumzia anguko la elimu, Lowassa pia alizungumzia vurugu za kidini zinazoendelea nchini, hususan kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini visiwani Zanzibar.
Aliwasihi Watanzania kutambua kuwa amani iliyopo ina maana kubwa kwani zikianzishwa vurugu za kidini hakuna atakayebaki salama na hakutakuwa na mshindi.
Wakati huohuo, Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), limeitaka serikali kutangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyotoka hivi karibuni kuwa janga la kitaifa kwa lengo la kuliepusha taifa na fedheha ya kuzalisha kizazi cha watu wasiosoma.
Mbali na kutaka matokeo hayo kutangazwa kuwa janga la kitaifa, pia baraza hilo limesema limeshaanza kuwasiliana na vijana waliofeli kutoka maeneo mbali mbali ya nchi kwa ajili ya kuandaa maandamano ya kumtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA), Dk Joyce Ndalichako, na Mkaguzi wa Elimu ya Sekondari nchini, waachie nafasi zao kwa madai kuwa wameshindwa kusimamia majukumu yao.
Kauli hiyo iltolewa jana jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu BAVICHA, Deogratius Mushi, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea kusikitishwa kwao na matokeo ya mitihani hiyo yanayoonyesha asilimia 60 ya wanafunzi, wamepata ziro.

Mushi alisema sababu kuu ya matokeo mabaya ni udhaifu wa serikali kushindwa kusimamia majukumu yake na kuchukulia kila jambo kwa wepesi.

"Hii serikali dhaifu ya CCM, mwaka 2006 ilisema lengo ni kufikia ufaulu wa asilimia 70 wakati huo tukiwa katika asilima 34 leo hata hiyo haipo sasa tunakwenda wapi na jeshi hili kubwa ambalo litakuwa haliajiriki tena kwa kukosa hata sifa ya kuwa na vyeti vya sekondari!?" alisema Mushi.

Katika hatua nyingine kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi waliofeli kutasababisha shule na vyuo vingi kukosa wanafunzi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa kuzungumza na wataalamu wa elimu unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi watashindwa kujiunga na masomo ya juu pamoja na vyuo.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Lowassa amtaka JK kuunda tume
• Waliofeli wapanga kuandamana kumng'oa Kawambwa

na Waandishi wetu
Tanzania Daima



[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
 
Back
Top Bottom