VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Katika kile kinachoonekana kama jitihada za Serikali kuhakikisha ufaulu wa kidato cha nne unapanda, wasahihishaji wa mitihani hiyo mwaka huu wamepewa maagizo maalum. Maagizo hayo ni kusahihisha hoja na si lugha wala mpangilio wa jibu. Maagizo hayo yalisambazwa katika vituo vyote vya kusahihishia mitihani hiyo kikiwemo kile cha Mbezi Beach,jijini Dar es Salaam.
Wasahihishaji mara nyingi walijikuta katika wakati mgumu katika kutekelezamaagizo hayo kwakuwa 'walilazimishwa' kutafsiri kile ambacho wanafunzi walilenga kukisema. Ilikuwa kazi pevu kuingia kwenye vchwa vya wanafunzi. Lakini,wasahihishaji hawakuwa na jinsi. Ni mbeleko kuta juu.
Nyaraka za awali zinaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka huku wavulana wakifaulu zaidi katika wastani. Hatahivyo, wasichana wameng'ara katika wanafunzi bora wa kitaifa. Matokeo husika yatatolewa rasmi kabla ya kusha mwez wa Februari.
More to come...