MATOKEO MAKUBWA SASA YANAVYOLIUMIZA TAIFA
Siku za hivi karibuni tumekuwa na msamiati unaitwa “Matokeo makubwa sasa” Pamekuwapo na juhudi za makusudi kuhakikisha kwamba kila jambo linapata matokeo makubwa. Jambo hili likanikumbusha wakati fulani nilipokuwa shule ya bweni pale Ifunda, siku za kula wali tulikuwa tunaulizwa mnataka “Quantity” au “Quality” wakiwa na maana kwamba kama tunataka Quantity tupikiwe aina fulani hivi ya mchele unaitwa Kitumbo ukipikwa kidogo tu unavimba na kujaa sufuria kama tunataka Quality tupikiwe mchele aina ya supa unaonukia lakini tutapewa kidogo maana hauvimbi.
Sasa kwasababu tulitaka kushiba tu siyo kula kitu bora, tukawa tunaitikia tunataka Quantity, tukisha sema hivyo mchele aina ya kitumbo unachukuliwa na kupikwa. Sifa ya mchele huo kubwa haukolei mafuta, mbaya zaidi hauna ladha yoyote wakati unakula nikama unatafuna mahindi makavu yaliyochemshwa hapa Arusha yanaitwa “makukulu” kwahiyo tukawa tunafurahia kwasababu tuliwekewa mwingi kwenye sahani japo hatukuwa tunaufurahia kwa ladha yake.
Tumekuwa na tabia ya kupenda wingi katika maeneo mbalimbali bila kujali ubora.Tukaanza kwenye elimu, mtazamo wetu ukawa ni kupeleka vijana wengi sana sekondari, lakini msisitizo mkubwa ukawa ni matokeo makubwa sasa bila kutazama zaidi ubora wa matokeo hayo si kwa maana ya ufaulu wake, lakini kwa maana ya maarifa na ujuzi utakaowafanya watu wajiajiri tukafanikiwa na sasa leo shule zote nchini zinashindana juu ya matokeo ya mitihani siyo juu ya ujuzi wanaoupata.
Tukawa na vyuo vikuu vingi nchini si jambo baya hata kidogo na kuhakikisha kwamba vijana wengi katika dhana ya matokeo makubwa sasa wanapata nafasi ya kusoma elimu ya juu, tukafanikiwa na sasa tuna vijana lukuki waliohitimu na wengine wanaendelea kuhitimu vyuo vikuu lakini je tuna mipango gani juu ya ajira zao?
Tumejiuliza siku za mbeleni hali itakuwaje? Je hatutafanana na nchi kama Nigeria ambapo karibu kila mwananchi ana shahada ya chuo kikuu na sasa yameibuka makundi mbalimbali ya kihalifu yanayosemekana ni ya wahitimu wasiokuwa na uhakika wa kupata hata mlo mmoja? Kama taifa tumejiandaaje kukabiliana na changamoto hiyo huko tuendako au hatujaona hatari bado?
Baadaye katika dhana ya matokeo makubwa sasa, tukahamia kwenye eneo la kilimo, hapa hali ni mbaya zaidi, sina hakika kama wote tumeona kama ninavyotazama mimi. Kabla ya matokeo makubwa sasa tulikuwa na mbegu zetu za asili za mazao, matunda, mbogamboga nakadhalika mara tukaambiwa tunatakiwa kuzalisha kwa wingi na kwamba hizi za asili zinafanya tupate mavuno kidogo, tukaletewa mbegu tunazo ambiwa ni za kisasa na kwamba hizi zinazaa maradufu, lakini tukaambiwa hizi mbegu hazipandwi hivihivi lazima ziambatane na mambo mengine kama vile mbolea za kupandia, kukuzia lakini pia eti huwezi kuvuna kama hutapiga dawa za wadudu.

picha na magabilo masambu
Hili la dawa likanikumbusha nyakati zile nilipokuwa kijijini pale Bulenda Bufwe, kwamba zao pekee lililokuwa likipigwa dawa ilikuwa ni pamba na ile dawa ilikuwa ikitokea pengine ng’ombe au mbuzi akala majani ya pamba muda mfupi baada ya kupuliza alikuwa akifa, sasa nikajiuliza hivi huu utamaduni wa kupuliza dawa katika mazao tunayotumia kama chakula ni kweli kwamba umefanyika utafiti wa kutosha na kuleta majibu kwamba dawa hizo hazina athari zozote kwa afya zetu?
Ikanikumbusha zaidi kwamba mbona zamani tulikuwa tukivuna mahindi yetu haya ya kienyeji tulikuwa tunachagua mahindi ya mbegu, kisha tunayatundika kwenye mti au jikoni mpaka yanafika msimu wa pili bila kuoza? Leo ukishamaliza kuvuna mahindi bado unaambiwa weka dawa ili yasiliwe na wadudu yaani mahindi ambayo wadudu hawali ni salama kwa binadamu!
Lakini nikakumbuka jambo lingine, mwaka 1995 babu yangu alikuwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji, wakati ule kanda ya ziwa palikuwa na uhalifu wa kutumia sumu kuvua samaki na hivyo wale waliokuwa wakikamatwa pamoja na mitubwi yao walikuwa wakiadhibiwa kwetu, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mitubwi na boti zao, haya yalifanyika kwaajili ya kulinda afya za walaji, sisi walewale tuliopinga walaji wasile sumu kwenye samaki tumeona ni halali tule sumu kwenye mahindi, kabichi, mbogamboga, matunda na kadhalika tutakuwa salama kweli?
Mimi siyo Daktari na siwezi kuthibitisha hili, lakini tafiti ziendelee kufanyika kubaini chanzo cha ongezeko kubwa la wagonjwa wa salatani nakadhalika kwasababu mwaka 2006 nilipata nafasi ya kutembelea hospitali ya Ocean Road kama sikosei palikuwa na kitengo cha wagonjwa wa salatani, wakati ule wagonjwa walikuwa wachache sana sijapata nafasi ya kurudi pale siku za hivi karibuni, lakini kwa vyovyote vile idadi yao itakuwa imeongezeka maradufu, ni kweli kwamba inawezekana salatani hizo zinatokana na sababu mbalimbali, lakini mojawapo yaweza kuwa ni matumizi ya sumu katika vyakula tunavyotumia kuanzia kwenye wale samaki wenye sumu waliokuwa wakikamatwa wakati ule.
Jambo baya zaidi ni kwamba, huku kuhitaji matokeo makubwa sasa yameharibu kabisa ardhi yetu kiasi kwamba, ardhi imekuwa kama mwanaume asiye na nguvu za kiume ambaye anahitaji viagra ili kukamilisha utaratibu wake. Leo huwezi kulima bila kutumia mbolea wala dawa ukavuna ni sehemu chache tu huko vijijini zimebaki lakini kwakweli hali ni mbaya najaribu kuwaza miaka 20 mbele uzalishaji wetu katika eneo la kilimo utakuwaje? Je ni mpango mkakati uliyojificha kwenye matokeo makubwa sasa ili baadaye tusizalishe chochote na tutegemee misaada kutoka mahala fulani? Tusipokuwa makini tutakuwa tegemezi tangu kwenye elimu mpaka kwenye uzalishaji wa chakula chetu wenyewe.
Kweli waungwana tunasomesha wataalamu wetu wa kilimo wanaokwenda kuuwa mbegu zetu za asili kwa kisingizio cha mavuno mengi, je tunatofauti gani na wale waliokuwa wanatumia sumu kuuwa samaki wengi kwa wakati mmoja lakini madhara yake yakiwa makubwa, leo samaki wameisha lakini magonjwa kwa watu yanaongezeka.
Serikali inapowekeza nguvu kubwa sana katika kujenga hospitali na vituo vya afya kila kata, juhui hizo hazitakuwa na maana yoyote kama hatutawekeza zaidi katika kukinga watu asiuguwe kwa maana nyingine kujenga huduma za afya bila kuzuia visababishi vya magonjwa ni sawa na kukata matawi ya mti huku tukitegemea mti utakauka kumbe mvua ikinyesha matawi yanachipuwa upya.
Mwisho kwasababu afya bora ni kichocheo cha maendeleo, niombe iundwe tume maalumu ili kuchunguza madhara yatokanayo na matumizi ya vyakula vinavyopulizwa sumu. Kwasababu kuna siku nikiwa sokoni nilisikia mama mmoja anasema anatafuta mboga iliyoliwa na wadudu akiamini haina sumu maana yake tunakula sumu za kutosha na mwisho wa siku Tanzania tutakwisha.

0689157789
Upvote
1