Matokeo std 7 yatoka rasmi leo hii.

Kayabwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2012
Posts
385
Reaction score
86
Wana jf leo saa 7 mchana waziri ametangaza matokeo ya drs la 7.Kwa mujibu wa TBC-dira ya mchana kiwango cha ufaulu kimeongezeka!!Ilisemekana hali ni mbaya!Lakini hii ndio serikali ya ccm huwa hawasemi ukweli,wao ni kuchakachua kila kitu sasa hadi Elimu.
 
wamo wasiojua kusoma na kuandika,hivyo wao huwa hawaangalii uwezo,wanataka tu idadi.
 
maswali hamsini,yote kuchagua,passmark 60 out of 250..ccm mnatuharibia watoto na wadogo zetu
 

Kiwango kimeongezeka, wa kwake wapo uingereza. Wakulima mtajiju na watoto wenu, eti kimeongezeka!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwanini wasingetoa na form four watu tukajipanga kwa kupunguza matumizi xmas.
 
Yap, ufauru umeongezeka na wasojua kusoma na kuandika nao wamefauru!
 
Watanzania ukweli tuinuke kukemea udhalimu huu juzi tu waliotoka kusahihisha mitihani walikuwa wanasema hali ni mbaya sana lakini tumeambiwa ngoja tuangalie tena hivi kilichokuwa kinaangaliwa ni nini tena mtomto kaandika 2+2=5 sasa wameendafuta wakaandika na 4 au wamekubali kuwa na tano halafu wamefauru,watoto wa shukuru kawambwa hawapo huko jamani,wtanzania jamani tuamkeni jamani namtafuta waziri kivuli wa Elimu sijui nae yupo wapi atuambie ukweli ni upi na yeye kazi yake ni ipi,Ee Mungu sisi hatujui alietuloga ila wewe kwa kua unaona sirini tuokoe na huyo mchawi alituloga watz.
 
wakuu nikitaka niangalie matokeo ntayapata kwenye website gani ? msaada tafadhali
 
wakuu nikitaka niangalie matokeo ntayapata kwenye website gani ? msaada tafadhali
Yatabandikwa shuleni kwa mtoto wako au bomani. Hakunaga website inayoonyesha MATOKEO ya std vii.
 
kama kweli kuamka ni kutinga jf basi karibu sana, na nimekugongea 'like' ya kwanza.
Join Date : 20th December 2012
Posts : 5
Rep Power : 302
Likes Received 0
Likes Given 0
 
Uwezo mdogo wa kufikiri kwa watanzania ndio mtaji mkubwa wa ccm katika mafanikio yao.


Na wao ndio wasababishi! Na hii ndio sera yao kubwa,ili umtawale mtu kiurahisi mnyime elimu! Nenda vijijini uone wazee wanavyoikumbatia CCM wakati wao ndio wahanga wa elimu duni! Aargh &*¿!!
 
Tunatengeneza vilaza nchini...maswali ya kuchagua? Passmark 60 chini ya 250 si pumba hiz
 
Na wao ndio wasababishi! Na hii ndio sera yao kubwa,ili umtawale mtu kiurahisi mnyime elimu! Nenda vijijini uone wazee wanavyoikumbatia CCM wakati wao ndio wahanga wa elimu duni! Aargh &*¿!!

Punguza hasira mkuu, tunawasubiri kidato cha kwanza. Maticha tumegundua mtindo mpya wa kufundisha sasa hivi. Unaingia darasani una wasomea watoto Course contents kutoka kwenye syllabus kama University, then unawaachia wasurf from the sources they know. Tunakutana kwenye mdterm test, na Terminal, muhura unaisha. Tukifungua July, tunawasomea Course Contents za kumaliza muhula wa pili. Kisha tunakutana kwenye Midterm ya September na Annual za November, mwaka unaisha, unakuja mwingine tena. Form two anarudia mara ya kwanza, anarudia ya pili anaingia kitaaa!!!! Tufanye nini sana? Hata kama ni wewe ungelifanya nini? No need to serve the stupid Government like that being led by JK wa pili, Itafahamika tu.
 
Tuongeze kwenye maajabu ya dunia "Kilmanjaro,Ngorongoro,Serengeti,Tanzanite,WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA" Maana vinapatikana Tanzania pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…