Matokeo std 7 yatoka rasmi leo hii.

Matokeo std 7 yatoka rasmi leo hii.

Punguza hasira mkuu, tunawasubiri kidato cha kwanza. Maticha tumegundua mtindo mpya wa kufundisha sasa hivi. Unaingia darasani una wasomea watoto Course contents kutoka kwenye syllabus kama University, then unawaachia wasurf from the sources they know. Tunakutana kwenye mdterm test, na Terminal, muhura unaisha. Tukifungua July, tunawasomea Course Contents za kumaliza muhula wa pili. Kisha tunakutana kwenye Midterm ya September na Annual za November, mwaka unaisha, unakuja mwingine tena. Form two anarudia mara ya kwanza, anarudia ya pili anaingia kitaaa!!!! Tufanye nini sana? Hata kama ni wewe ungelifanya nini? No need to serve the stupid Government like that being led by JK wa pili, Itafahamika tu.

Nadhani haufahamu unapigana na nani wewe. Unaowafanyia hivyo ni watanzania wenzako wasio na hatia, ambao wamekandamizwa na system iliyopo. wakidanganywa na kutojua watokee wapi. Kuna haja ya kuwasaidia ili tujenge base ya watu wenye ufahamu na kujenga hoja thabiti za kuwaondoa wazalimu madarakani. Ukitaka kupambana nao sio walioko shuleni, and nobody care, kiwango cha ufaulu kitaendelea kutangazwa kimepanda na vigezo vya kupanda hutakaa uvijue.
Pigana vita vilivyo uweze kupambana. Bado nafasi na uwezo tunao tukipigana vita kwa usahihi tutashinda.
 
Hakika matokeo yamechakachuliwa kwasababu kuna ndugu yangu(DEO) alikwenda kwenye selection na aliporudi alitueleza kuwa matokeo ni mabaya kuliko kawaida. Kwa kauli yake alidai kuwa ufaulu kitaifa ulikuwa chini ya 50% na kuwa kuna mikoa ambayo imefaulisha kwa 20% na mingine chini ya 20%. Hii sera ya "UCHAKACHUAJI" ya hawa jamaa italimaliza hili taifa tusipokuwa waangalifu.
 
Back
Top Bottom