Matokeo Tata ya Kidato Cha IV: Mkurugenzi wa NECTA, Bi. Ndalichako Ajitokeza TBC, Ajikanyagakanyaga!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa, NECTA, kutangaza Matokeo Tata ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu badala ya Mkurugenzi wa NECTA, Mkurugenzi huyo, Bi. Joyce Ndalichako, ameibukia TBC-1 na yuko live kwenye kipindi cha Jambo.

Wenye access hebu shuhudieni jinsi anavyojikanyaga kanyaga kwa kupeleka karatasi halisi za kilichoandika na baadhi ya wanafunzi, kwa kupeleka zile zilizoandikwa matusi, ili kupata public sympathy kwa kilichotokea!.

Endeleeni kumfuatilia.

Pasco.
 
Bi Ndalichako, anahojiwa na Marine Hassan Marine, natamani swali la kwanza lilipaswa liwe, Nani mwenye Mamlaka ya Kuyatangaza Matokeo?. Nijuavyo mimi mwenye mamlaka ni Katibu Mtendaji, na ndivyo imekuwa ikifanyika miaka yote, kwa nini matokeo ya mwaka huu, yatangazwe na waziri?. Au ndio juhudi za Waziri Kawambwa, kujaribu kufurukuta, baada ya kupwaya kila alikopelekwa?, yaani Kawambwa ni "misfit!".
Pasco.
 
Kwa sasa, TBC-1 ni habari, ila Bi Ndalichako, anaendela live kupitia TBC-Taifa!.

Pasco.
 
Bi. Ndalichako, amepeleka nakala halisi za mitihani ili kuthibitisha baadhi ya wanafunzi, waliandika madudu, matusi na wengine wameandika "versi!". Kitendo cha kupeleka nakala halisi, badala ya kupeleka copy, ni kinyume cha kanuni, taratibu na sheria, kwa sababu mitihani halisi, ni miongoni mwa documents ziitwazo, "classified documents" ambazo zinakinga ya "confidentiality", linapotokea suala lolote linahusu kuonyeshwa kwa mitihani hiyo, Mkurugenzi wa NECTA, hana mamlaka ya kujibebea nakali halisi za mitihani hiyo, simply because mitahani hiyo iko in possession ya documents hizo!, alipaswa kutoa nakala, yaani copy na kupeleka TBC-1 na sio kupeleka nakala halisi!. Huku ni kujikanyaga kanyaga just to seek public sympathy ya justification ya matokeo ya mwaka huu kwa ku potray kuwa NECTA has no hand!, ni watahiniwa wa mwaka huu tuu ndio Vibonde!, na kuthibitisho hilo, ameleta mitihani halisi kuonyesha hivyi ndivyo walivyo!.
Pasco.
 
Uliambiwa utapewa msaada wa mabati kuezeka nyumba yako inayovuja. Mvua zimeanza na ndani hakulaliki. Utaendelea kulalamika au utachukuwa hatua. Kwa muda mrefu elimu ya nchi hii imekwenda alijojo na wawakilishi wetu wanakutana na kila aina ya vikwazo katika harakati za kurekebisha hali hiyo. Ni wakati wa wananchi kulitangaza janga hili na kuionesha mamlaka kwamba sasa basi. Vinginevyo tuvumilie tu mvua itunyeshee.
 
Bi. Ndalichako, amepeleka nakala halisi za mitihani ili kuthibitisha baadhi ya wanafunzi, waliandika madudu, matusi na wengine wameandika "versi!". Kitendo cha kupeleka nakala halisi, badala ya kupeleka copy, ni kinyume cha kanuni, taratibu na sheria, kwa sababu mitihani halisi, ni miongoni mwa documents ziitwazo, "classified documents" ambazo zinakinga ya "confidentiality", linapotokea suala lolote linahusu kuonyeshwa kwa mitihani hiyo, Mkurugenzi wa NECTA, hana mamlaka ya kujibebea nakali halisi za mitihani hiyo, simply because mitahani hiyo iko in possession ya documents hizo!, alipaswa kutoa nakala, yaani copy na kupeleka TBC-1 na sio kupeleka nakala halisi!. Huku ni kujikanyaga kanyaga just to seek public sympathy ya justification ya matokeo ya mwaka huu kwa ku potray kuwa NECTA has no hand!, ni watahiniwa wa mwaka huu tuu ndio Vibonde!, na kuthibitisho hilo, ameleta mitihani halisi kuonyesha hivyi ndivyo walivyo!.
Pasco.
kwani shida ni mitihani? shule nyingi hazina walimu vijijini huko.watoto hawakuandaliwa walimu walikuwa kwenye migomo hayo matokeo mazuri yangetoka wapi? asituchoshe hapa!
 
Kwangu mimi maamini kabisa serikali haijaamua kushughulikia tatizo la elimu hapa nchini kwani inajua tatizo la kushuka elimu limeanzia wapi na nini soln yake!!

Madai ya walimu yanatupwa chini na watu wanaona uwezo wa kusolve upo, kifupi walimu wamekuwa too much discouraged na uababaishaji huu.
 
Wanabodi,

Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa, NECTA, kutangaza Matokeo Tata ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu badala ya Mkurugenzi wa NECTA, Mkurugenzi huyo, Bi. Joyce Ndalichako, ameibukia TBC-1 na yuko live kwenye kipindi cha Jambo.

Wenye access hebu shuhudieni jinsi anavyojikanyaga kanyaga kwa kupeleka karatasi halisi za kilichoandika na baadhi ya wanafunzi, kwa kupeleka zile zilizoandikwa matusi, ili kupata public sympathy kwa kilichotokea!.

Endeleeni kumfuatilia.

Pasco.
Public sympathy kwa kitu gani ambacho kakifanya against public interest? Kwani hatua walizochukuliwa public inaona hazikustahili? Ni kama umemuattack huyu mama bure. Kwa logic sioni kama kuna lolote kakosea. Watoto wamechemka, tatizo linajulikana limeanzia serikalini na walimu wake thats all.
 
Inawezekana nikawa nime-miss kitu, lakini sijaona wapi anapostahili lawama huyu mama. Kama maandalizi toka mwanzo hayakuwa mazuri, sasa tunaanzaje kumlaumu huyu bi mkubwa? Kwani maandalizi ya kufanya mtihani yanaanzia kwenye chumba cha mtihani? Mwanafunzi kashuka na the so called verses za bongo flavor, Ndalichako afanye nini?

Tukubali kuwa wote tumeshiriki kwenye matokeo mabaya ya watoto wetu. Mzazi, umefanya nini kuhakikisha mwanao anajiandaa vema na mitihani let alone kujijengea mazoea ya kujisomea? serikali, imehakikishaje kuwa mwanafunzi anapata mazingira swadakta ya kumwezesha kufanya vizuri kwenye mitihani? Hii ni kuangalia mifumo yake yote na miundo mbinu ya elimu pia. Mwalimu naye nafasi yake ikawaje kwenye kumsaidia mwanafunzi wake anafanya maandalizi since day one na sio kwa dhana ya 'ng'ombe kunenepeshwa siku ya mnada'?
 
Wanabodi,

Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa, NECTA, kutangaza Matokeo Tata ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu badala ya Mkurugenzi wa NECTA, Mkurugenzi huyo, Bi. Joyce Ndalichako, ameibukia TBC-1 na yuko live kwenye kipindi cha Jambo.

Wenye access hebu shuhudieni jinsi anavyojikanyaga kanyaga kwa kupeleka karatasi halisi za kilichoandika na baadhi ya wanafunzi, kwa kupeleka zile zilizoandikwa matusi, ili kupata public sympathy kwa kilichotokea!.

Endeleeni kumfuatilia.

Pasco.
Pasco hivi NECTA kazi yao ni kufundisha au kutaini wanafunzi? Ukiangalia vyombo vyote vya habari vinaiangalia NECTA kama wao ndio wenye sababu ya wanafunzi kufeli bila kuangalia nani mwenye wajibu wa kuwaandaa wanafunzi hao yaani Commissioner wa elimu. NECTA walaumiwe kama walitunga mtihani ambao hautokani na "syllabus" inayotumika.
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana nikawa nime-miss kitu, lakini sijaona wapi anapostahili lawama huyu mama. Kama maandalizi toka mwanzo hayakuwa mazuri, sasa tunaanzaje kumlaumu huyu bi mkubwa? Kwani maandalizi ya kufanya mtihani yanaanzia kwenye chumba cha mtihani? Mwanafunzi kashuka na the so called verses za bongo flavor, Ndalichako afanye nini?

Tukubali kuwa wote tumeshiriki kwenye matokeo mabaya ya watoto wetu. Mzazi, umefanya nini kuhakikisha mwanao anajiandaa vema na mitihani let alone kujijengea mazoea ya kujisomea? serikali, imehakikishaje kuwa mwanafunzi anapata mazingira swadakta ya kumwezesha kufanya vizuri kwenye mitihani? Hii ni kuangalia mifumo yake yote na miundo mbinu ya elimu pia. Mwalimu naye nafasi yake ikawaje kwenye kumsaidia mwanafunzi wake anafanya maandalizi since day one na sio kwa dhana ya 'ng'ombe kunenepeshwa siku ya mnada'?

Upo sahihi kabisa mimi siku naamini kabla ya kutupia lawama Serikali na Walimu lazima tuangalie Wazazi na Wanafunzi wamefanya nini? sio siri utandawazi umetumaliza sana tena sana, Wazazi wamewaacha tu watoto wafanye wanavyotaka, kila siku watoto wanashinda kwenye mitandao, mwalimu anafundisha dent anasikiliza mziki kwenye simu.

Nachokiamini mimi hata serikali iwalipe walimu mshahara wa milioni, na hata walimu wafundishe namna gani kama Wanafunzi na wazazi wataendelea na life style ya kujiachia tusitegemee kabisa elimu ya nchi hii kupanda.

Miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000 hakukuwa na walimu wengi kama ilivyo sasa lakini ufaulu ulikuwa mzuri tu, mimi nimesoma advance shule ambayo haikuwa na mwalimu hata mmoja lakini katika darasa letu hakuna aliyefeli kwa kuwa tulikuwa tunajituma wenyewe bila kutegemea mwalimu wala serikali
 
kuna factors nyingi zimechangia hawa watoto kufeli mkuu,hata watoto wenyewe wanahusika maana wenyewe ni wadau wa starehe fiesta,dar live facebook ,bbm .whatsupp nk
lakini kuna sababu za wengi kama hivo walimu hakuna ,watoto wamechaguliwa sec hawajui kusoma wala kuandika.walimu wanagoma ,watoto watafaulu vipi hapa.hawa watoto utawalaumu vipi? ni kweli wapo watoto wanakuwa na access zote za elimu bora ila wanafeli hilo lipo toka enzi za mwalimu,hao tunasema ni natural failure.kama mwanaasha yule mnamsemaga humu,ila kuna wengi walofeli asilimia kubwa serikali ndo ya kulaumiwa 100%
 
Ndachuwa
Pasco hivi NECTA kazi yao ni kufundisha au kutaini wanafunzi? Ukiangalia vyombo vyote vya habari vinaiangalia NECTA kama wao ndio wenye sababu ya wanafunzi kufeli bila kuangalia nani mwenye wajibu wa kuwaandaa wanafunzi hao yaani Commissioner wa elimu. NECTA walaumiwe kama walitunga mtihani ambao hautokani na "syllabus" inayotumika.
Mkuu Ndachuwa, kiukweli huyu kipanga wangu wa hesabu kupata C hata mimi nimesikitishwa sana!. Nawaombeni tuamini there was something wrong with NECTA!.
Pasco
 
Barza la mitihani kuna tatizo hasa kwenye usahihishaji, yaani marking. mfano mwanafunzi asipofanya swali la compulsory section C yenye marks 60% kwenye mitihani ya lugha (kiswahili na Englis) section yote atapata zero. Huoni kama kuna haja ya kuangalia tatizo?
 
Bi. Ndalichako, amepeleka nakala halisi za mitihani ili kuthibitisha baadhi ya wanafunzi, waliandika madudu, matusi na wengine wameandika "versi!". Kitendo cha kupeleka nakala halisi, badala ya kupeleka copy, ni kinyume cha kanuni, taratibu na sheria, kwa sababu mitihani halisi, ni miongoni mwa documents ziitwazo, "classified documents" ambazo zinakinga ya "confidentiality", linapotokea suala lolote linahusu kuonyeshwa kwa mitihani hiyo, Mkurugenzi wa NECTA, hana mamlaka ya kujibebea nakali halisi za mitihani hiyo, simply because mitahani hiyo iko in possession ya documents hizo!, alipaswa kutoa nakala, yaani copy na kupeleka TBC-1 na sio kupeleka nakala halisi!. Huku ni kujikanyaga kanyaga just to seek public sympathy ya justification ya matokeo ya mwaka huu kwa ku potray kuwa NECTA has no hand!, ni watahiniwa wa mwaka huu tuu ndio Vibonde!, na kuthibitisho hilo, ameleta mitihani halisi kuonyesha hivyi ndivyo walivyo!.
Pasco.

Bahati mbaya sikuona hicho kipindi ila kama kweli amepeleka nakala halisi ya walichokiandika wanafunzi mimi nampongeza sana huyo mama kwa sababu kama akiendelea kufanya haya mambo siri kwa kivuli cha classified document watoto wetu wataendelea kuangamia. Nadhani wazazi walioona kwao ni darasa tosha wakikaa na watoto wao watakuwa wanawaasa ili wasiandike mambo ya kipuuzi kwenye mtihani. Lazima wachukulie mitihani seriously kwa sababu hiyo ni hatua muhimu sana katika maisha yao. Kwa maoni yangu wazazi wa watoto wote walioandika madudu wangeoneshwa madudu ya watoto wao.
 
Barza la mitihani kuna tatizo hasa kwenye usahihishaji, yaani marking. mfano mwanafunzi asipofanya swali la compulsory section C yenye marks 60% kwenye mitihani ya lugha (kiswahili na Englis) section yote atapata zero. Huoni kama kuna haja ya kuangalia tatizo?

Mkuu umeshasema kuwa swali ni Compulsory, sasa kama mwanafunzi hajalijibu, msahihishaji afanyeje?
 
Ndachuwa
Mkuu Ndachuwa, kiukweli huyu kipanga wangu wa hesabu kupata C hata mimi nimesikitishwa sana!. Nawaombeni tuamini there was something wrong with NECTA!.
Pasco
Pasco Kifungilo wao wamepata Division I mpaka III; IV na Zero hakuna wao mtihani wao haukutungwa na kusahihishwa na NECTA? Kama wewe ni mtafiti wakaguzi wa elimu huwa wakali zaidi kwa shule za binafsi kulizo zile za umma matokeo yake shule za binafsi zinatimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na kuwa na walimu, matundu ya kutosha ya choo; walinzi nk. mazingira ambayo humjengea mwanafunzi utulivu wa masomo na hivyo kufauli zaidi ya wale wa shule za serikali.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umeshasema kuwa swali ni Compulsory, sasa kama mwanafunzi hajalijibu, msahihishaji afanyeje?

Nafikiri hujanielewa, ni kwamba section C inaweza kuwa na mwaswali 5, mtahiniwa akambiwa ajibu 4 lakini moja ya mwaswali kati ya hayo moja ni compulsory, sasa katika marking iwapo mtahiniwa hajalifanya hili swali la compulsory akafanya mengine basi hata hayo mengine hawafanyi marking. umenipata?
 
Back
Top Bottom