mabutu1835
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 909
- 1,425
Hivi karibuni Baraza la mitihani Tanzania limetoa matokeo ya darasa la Saba na katika taarifa yao ni kwamba, ufaulu umeongezeka. Hilo halikunipa shida isipokuwa waliofutiwa matokeo kwa sababu kuu mbili:
1: Kuibia katika mtihani, hili halikunipa shida sana katika masuala ya mitihani ni kawaida kwa wanafunzi wa ngazi zote.
2: Kuandika matusi katika karatasi za majibu; HILI linaleta ukakasi na maswali mengi nayo ni:
i. Je mtahiniwa ana afya ya akili sawa sawa au Kuna shida pahala?
ii. Je ni kweli kwa HIYARI yake ameandika hayo matusi au kuna msukumo kutoka kwa wazazi au walezi?
Serikali isichukulie poa walioandika matusi wafanye jitihada kuwahoji vinginevyo naona tatizo linaweza kuongezeka siku za usoni.
Wewe una mtazamo gani katika hili na mengine yahusuyo matokeo ya darasa la Saba?