joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Wakenya wengi wanazidi kuchanganyikiwa baada ya kuona hali zao za maisha zikiendelea kuwa mbaya, Huduma za kijamii kuendelea kuzorota kutokana na ahadi hewa walizopewa na viongozi wao wakati wa uchaguzi.
Walipoona viongozi wao hawawasikilizi, wakaamua kutumia haki yao ya kikatiba kama ilivyoainishwa katika " Katiba nzuri " ya Kenya ya kufanya maandamano ya amani, kama kawaida ya POLISI wa Kenya, kuthibitisha kwamba demokrasia Kenya ni jambo linalotajwa ktk makaratasi pekee, wamewamiminia risasi waandamani na kukatisha maisha ya KIJANA mmoja na kujeruhi kadhaa.
R.I.P.
Sent using Jamii Forums mobile app