Matokeo ya katiba nzuri na GDP kubwa, POLISI wawapiga risasi raia waliokuwa wakiandamana kwa amani

Matokeo ya katiba nzuri na GDP kubwa, POLISI wawapiga risasi raia waliokuwa wakiandamana kwa amani

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Wakenya wengi wanazidi kuchanganyikiwa baada ya kuona hali zao za maisha zikiendelea kuwa mbaya, Huduma za kijamii kuendelea kuzorota kutokana na ahadi hewa walizopewa na viongozi wao wakati wa uchaguzi.

Walipoona viongozi wao hawawasikilizi, wakaamua kutumia haki yao ya kikatiba kama ilivyoainishwa katika " Katiba nzuri " ya Kenya ya kufanya maandamano ya amani, kama kawaida ya POLISI wa Kenya, kuthibitisha kwamba demokrasia Kenya ni jambo linalotajwa ktk makaratasi pekee, wamewamiminia risasi waandamani na kukatisha maisha ya KIJANA mmoja na kujeruhi kadhaa.
R.I.P.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hapo mwenye makosa ni "katiba nzuri" au ni Polisi? CCM mnatetea udikiteta kwa point za kishenzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia akili wewe, katiba nzuri hupimwa kwa jinsi viongozi wanavyoshughulikia na kutatua kero za wananchi, jinsi wananchi walivyo na Uhuru wa kuonyesha hisia za bila kubughudhia, na jinsi vyombo vya dola vinavyowajibika kwa wananchi sio kwa viongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha, unataka wafe wangapi ndio neno kumimina risasi liwe limekamilika?. Unaweza kumimina risasi na asife hata mtu mmoja, inategemea na shabaha yako, na jinsi hao unaowamiminia risasi walivyoji - "position".

Sent using Jamii Forums mobile app
wamewamiminia risasi waandamani na kukatisha maisha ya KIJANA mmoja na kujeruhi kadhaa.
Ona sentensi ilivyoandikwa.. wamemiminiwa risasi waandamanaji akauawa mmoja. Maana yake ni nini? kama alilenga shabaha pembeni, hakuwamiminia risasi, alizimimina pembeni!
 
Back
Top Bottom