MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

mwaka 2008, Shule moja inayoitwa High view sec school inayomikiwa na mmoja ya mfanya biashar mkubwa visiwani Zanzibar iliongoza Zanzibar kwa kufanya vizuri yaani ilitoa div 1 zaidi ya 15, div 2 za kumwaga kati ya watoto wsiozidi 50. hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutoa idadi kubwa wanafunzi. nadhani hata Baraza la Mitihani la Taifa Necta ilishtuka, iljihoji na ilitaka kujua haya ni matokeo ya Kweli?
Mwaka uliofuta NECTA ilituma ujumbe mzito katika shule hiyo, kwa maneno ya vijana iliwabana vijana sana vijana shule hiyo kwa kuweka Ulinzi mkali kwa usimamizi, ufanyaji wa mitihani, baadhi ya wajumbe kutoka NECTA Makao makuu Walishiriki kikamilifu kusimamia exam shuleni hapo. nasema walishiriki kusimamia, kuchunguza na kuzuia kila aina ya Ujanja, walifikia hata kuwasachi kabla ya exam. matokeo yake wanafunzi waliofanya Exam matukio yao sio mazuri.(naamini hata NECTA kwa hili hawatakanusha).
lKN sijui kama NECTA hufanya mkakati kama huu ktk shule ambazo huwa zinaongoza hasa za seminary? sijui kama wanshtuka kama walivyoshtuka High view? sijui hutumia mkakati kama walivyotumia huko Zenj?

LKN cha kujiuliza jee hawa ndio wanaopta first class Vyuo vikuu? au ndio bogas

Huo ushahidi uko wapi? wewe badala ya kuhamasisha watu wasome unadanganya watu. unatupotezea muda hapa.
 
Wakati mwingine ni busara kutokuanzisha thread au kuposti kitu chochote!

Hawa wote ni wadogo zetu hamna cha kufurahisha hapo!

Inabidi ifike mahala shule za Kikristo ziruhusu na waislam kusoma angalau kuwe na uwiano sio kila siku wanafaulu wao tu.
 
Mkuu post yako imekaa kidini dini.
Labda kama wewe ni muislam sawa lakini wakristo hatuna tabia ya kujigamba bali hujibu pale mtu anapopotosha ukweli,
kazi yetu ni kufanya kile tunapaswa kufanya tena kwa ufasaha
 
Wakati mwingine ni busara kutokuanzisha thread au kuposti kitu chochote!

Hawa wote ni wadogo zetu hamna cha kufurahisha hapo!

hmedhod, hizi mada ni muhimu kuwepo janvini kwani zinztupa changamoto nyingi: kwanini waliosoma shule zenye misalaba waongoze: kwanini waliosoma kwenye shule zenye minara ya mwezi na jua wasiongoze. Kwa nini watoto wa shule hizi wamefanya vizuri katika somo la dini ya kiislam na kushindwa haya na masomo ya lugha na sanaa?, hii inatia mashaka lakini iko wazi kuwa uwezo wanao isipokuwa muenendo wa utoaji mafunzo unatia walakini. Ni kwanini miaka yote shule hizi za kiislam hazifurukuti, je, kuna mtu au taasisi inayo wazuia kufanya vizuri?
 
Wewe umeshawahi kufika Seminari? Wanasoma kuliko maelezo, wana sheria kali za kuhakikisha kuwa kila mtu anasoma. Waalimu wapo, wazazi wanashiriki kikamilifu kuhakikisha kuwa wanapatikana, wanawapa motisha kila mara wanapofanya vizuri. Hivi umeshasikia wanalalamikia ukosefu wa walimu?
 
Waziri wa Elimu katika serikali ya awamu ya tatu, Joseph Mungai, amesema matokeo mabovu yamesababishwa na Serikali ya awamu ya nne, kuyatupa baadhi ya mambo mazuri yaliyokuwemo kwenye Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) uliobuniwa na Serikali ya awamu ya tatu.
Mungai alisema moja ya mambo mazuri yaliyokuwemo kwenye MMES ni mizania kati ya upanuzi wa elimu ya sekondari na upanuzi wa mafunzo ya walimu wa sekondari.
”Nafikiri haya matokeo ya sekondari yanatokana na kupanua elimu ya sekondari bila kufuata mpango wa elimu ya sekondari,” alisema Mungai na kuongeza:
“Kulikuwa na mpango wa MMES niliuacha pale (Wizara ya Elimu) tulikuwa tumepanga mambo mengi na yalikuwa yaende hatua kwa hatua.
“Moja ni kwamba ilikuwa baada ya miaka mitano, kuanzia mwaka 2005, idadi ya wanafunzi wanakwenda elimu ya sekondari ndiyo wafikie asilimia 50, lakini serikali ya awamu ya nne ilifanya mabadiliko na kutaka wanafunzi wote wanaohitimu darasa la saba waende sekondari na hapo ndipo tatizo lilipoanzia,” alisema.
Alisema baada ya mafanikio makubwa katika elimu ya msingi kutokana na utekelezaji wa Mpango wa Elimu ya Msingi (MMEM) ulitengenezwa MMES ambao ulipaswa kuanzia mwaka 2005 na mwaka huo ndipo vilianzishwa vyuo vikuu vya elimu vya Mkwawa na Chang’ombe kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa walimu wa sekondari.
Alisema Mkwawa na Changómbe vilianzishwa kwa lengo la kuweka mizania kati ya upanuzi wa elimu ya sekondari na upanuzi wa mafunzo ya walimu wa sekondari.
Aliongeza kwamba wizara ilizungumza na vyuo hivyo baada ya kuanzishwa, kwamba wanafunzi wa mwaka wa kwanza wafundishwe zaidi mbinu za ufundishaji ili baada ya mwaka huo waende kusaidia kufundisha sekondari kupunguza uhaba wa walimu.
“Tulitaka wanafunzi walioingia mwaka wa kwanza wakati vyuo hivyo vinaanzishwa, mkazo uwekwe zaidi kwenye mbinu za ufundashaji ili wapate Diploma in Education (Stashahada za Elimu) ili waende wakafundishe …Programu kama hiyo tuliingiza pia katika Chuo cha Ualimu cha Mtwara, lakini sijui nini kilitokea mpango huo ukafutwa,” alisema Mungai.
Alisema baada ya mpango huo kufutwa, serikali ilianzisha mpango wa kujenga shule ya sekondari kila kata huku zikikabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu.
Alisema kuna baadhi ya shule katika kata zina mwalimu mmoja au wawili na kwamba ilifika wakati wizara ililazimika kuanza kupanga upya walimu.
“Haikuwa mbaya, tatizo ni kwamba baadhi ya shule zilikuwa zinafanya vizuri, lakini walimu wake walipoondolewa na kuhamishiwa sehemu nyingine, shule hizo ziliathirika pia,” alisema.
Tatizo lingine alisema ni mrundikano, huku baadhi ya masomo yakiwa yanafundishwa hovyo hovyo kutokana na kutokuwa na walimu wanaoyamudu.
“Tulitengeneza programu ya kupunguza wingi wa masomo katika shule za sekondari tukaondoa masomo ya michepuo kama Ufundi, Kilimo na Biashara na tukaweka mkazo kwenye Hisabati na tukataka somo la Hisabati liwe na hesabu za biashara…hilo nalo liliondolewa,” alisema.
Alisema ili kuboresha elimu ya sekondari, kuna haja ya kufanya marejeo ya MMES pamoja na kuweka mkazo kwamba shuleni ni mahali pa mwalimu kufundisha na mwanafunzi kusoma.
 
Matokeo ya Form Four Yametoka, Kwa Mara Nyingine tena Zaidi ya Aslimia 80 Wamefeli. Tuyaangalie haya Matokeo katika Mtindo Mwingine ambao uko Tofauti na Mtindo ambao NECTA wametumia kuyawakilisha haya Matokeo kwa Jamii ya Watanzania, Mtindo ambao NECTA walitaka tuamini kwamba waliofaulu ni 50.4%


Note: Idadi ya Wanafunzi waliofanya Mtihani ( Ukijumlisha Students and Private Candidates) walikuwa ni 441,271. Naomba niwazungumzie Only Student Candidates
Jumla ya Wanafunzi waliofanya Mtihani ni 352840


Divisheni One + Two + Three = 42,014 == 11.9%
Divisheni Four = 135,826 =========== 38.5%
Divisheni Zero = 175,000 =========== 49.6%
Kwa hiyo Divisheni Four + Divisheni Zero Jumla yake ni 310,826 ====== 88.1%


Tukae Tujiulize hivi hawa Zero&Four 300,000+ Ni nini Hatima yao? Kinachouma Zaidi ni kwamba Zaidi ya Asilimia 90 yao ni Watoto wa Wazazi wanaishi katika Lindi la Umaskini huku Pesa Zao zikienda Kufanya Shopping Dubai, Kosa lao nini hawa hadi Kustahili matokeo haya? Je Hii ni ndiyo Zawadi ya kuimba Nambari one eeeee eee Nambari one ni CCM? Je Tuendelee kulalamika hivi hivi kama Mwaka jana? Watanzania ni watu wa kusahahu hivi tunakumbuka mwaka Jana?


Ngoja Niwakumbushe Kidogo

MATOKEO ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne kwa mwaka 2009 yametangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) huku yakionyesha shule za serikali zikiendelea kufanya vibaya kwa kushindwa kuwemo kwenye shule 10 bora huku kiwango cha ufaulu kikizidi kupungua.


Aidha, matokeo ya mtihani huo uliofanyika Oktoba mwaka jana yanaonyesha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa asilimia 11.2 kwani mwaka 2008 kilikuwa asilimia 83.69 wakati mwaka huu kikishuka hadi kufikia asilimia 72.51


Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es salam kwenye ofisi za baraza hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako, alisema watahiniwa 351,152 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, kati yao wasichana ni 167,591 sawa na asilimia 47.73 na wavulana 183,561 sawa na asilimia 52.27 wakati mwaka 2008 watahiniwa 241,472 walisajiliwa


Alibainisha kuwa watahiniwa 42,672 sawa na asilimia 17.85 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ambapo wasichana ni 13,788 sawa na asilimia 12.47 na wavulana 28,884 sawa na asilimia 22.48.




Alisema, watahiniwa waliopata daraja la nne ni 130,651 sawa na na asilimia 54.66 wakati waliopata sifuri ni 65,708sawa na asilimi 27.49 idadi inayoonekana kuongezeka tofauti na mwaka jana.
Kuna Mtu ameshawahi kujiuliza Hatima ya hawa 65,708 wa mwaka 2009? Hivi hawa walimkosea nini Mungu?

Ngoja niyaweke hivi ili Muelewe nini Nazungumzia


----------------------------------2009 ---------2010 ------------2011

Divisheni ( One, Two and Three)....42,672--------- 42,014 ------------
Disheni Four...............................130,651...................135,826
Divisheni Zero............................ 65,708 ....................175,000

Nauliza Tena Tuendelee kulalamika ili Mwaka huu tena yatukute kama haya?

Ningependa sana JF kama Jukwaa la Great thinker tulijadili hili Suala ambalo mimi naliita ni Janga la kitaifa, tusilifanye likwa ni la Kidini (maana nimeshaona Baadhi ya watu wa Dini moja wakiwacheka wenzao na wenzao wakilaumu Serikali kuipendelea Dini Nyingine). Unapaswa kuwa Mjadala wa kitaifa wenye Lengo la Kuonesha Suluhisho juu ya Tatizo hili kwa manufaa ya watoto zetu, wadogo zetu na Taifa kwa Ujumla

Wana JF Nimamua Kuchokonoa Huu Mjadala naomba Tuchangie tukiwa na Tunatambua kwamba Watoto wa Maskini bila Kujali Dini zao wala Makabila yao Maisha yao yako hatarini.

Karibuni sana
 
kuhusu mzizima sijui maendelea vipi kwan majukumu yamekuwa mengi.lakin kama miaka mitano nilisoma kwenye magazeti wamefanya vizuri
 
especially wakati wa kuajiriwa wanaposema wengine wanapendelewa wanataka kuwe na uwiano wa nusu kwa nusu.
Unajua hata mi ndo nashangaa kama matokeo ya mitihani ambayo ndo kiashirio cha kuendelea mbele uwiano haupo, sasa huko juu kwenye ajira utakuwepo kweli?
 
Ndugu yangu nimecheka sana kama unatumia style hii kumsaka mchawi!
Labda ujaribu mbinu nyingine.Umeshawahi kuona products za seminary au shule za misheni? Elewa kuwa mtihani wa siku moja au mbili hautoshi kukupa matokeo mazuri.Uliza hata hao wa dini ingine wanaosoma huko Marian au St Joseph Millenium Schools.Utapata jibu la uhakika. Usichanganye na shule nyingine binafsi za private zenye kufanya biashara zaidi na wakotayari kutumia mbinu chafu kujiweka sokoni kwa kufaulisha.
 
Mbona munakosa usingizi kwa kutaja waislamu? Sasa kama wamefeli sana si ndiyo furaha yenu mutapata ajira nyingi?

hebu tafuteni la maana la kuzungumza mutapata vidonda vya tumbo kwa kufikiria uislamu.
 
Hawa jamaa ndio wanaokuja kusumbua sana mitaani.

tatizo shule zao hawataki kujichanganya na ukienda ww mkristo utafanyiwa visa kama vya mbwa mdokozi.

Na tena watakulazimisha uwe Shaibu ili angalau weweze kukujali.

Sasa waacheni wakae na shule zao zitawasaidia angalau kujua kiarabu.:thinking:
 
Nadhan hili suala la shule za kiislam kufelisha sana tulichukulie serious kidogo.... Cdhan kama tatizo ni dini yao au imani yao... Nnadhan tatizo ni walimu wao pamoja na techniques wanazozitumia!...
 
Mbona munakosa usingizi kwa kutaja waislamu? Sasa kama wamefeli sana si ndiyo furaha yenu mutapata ajira nyingi?

hebu tafuteni la maana la kuzungumza mutapata vidonda vya tumbo kwa kufikiria uislamu.
Speculating......mh,
Eng Nsiande
 
Udini hautaisaidia nchi yetu tuachane nao. Dini iwe ya mtu na mungu wake na sio kero na usumbufu kwa watu wasio wa dini yako.
 
Kinachotakiwa ni kufanya Research yaani utafiti wa kisayansi zaidi kuliko kiimani. Mtafiti achague shule tofauti tofauti kutoka kila mkoa au wilaya kuzingatia seminari za dini zote, za serikali/kata na kuchunguza mbinu zinazotumika. Kwa ufupi tatizo kubwa ni waalim na masilahi yao, malezi nje ya madarasa,vitabu vya kiada na ziada, maabara, ufaulu wa wanafunzi (Darasa la saba) wanaokwenda katika shule za kulipia, mfumo wa kutoa elimu za dini n.k. Isitoshe shule nyingi za St. sio seminary ni majina tu ili kupata unafuu fulani au kuaminika lakini umiliki sio wa taasisi za kidini.
 
Back
Top Bottom