MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

mwaka 2008, Shule moja inayoitwa High view sec school inayomikiwa na mmoja ya mfanya biashar mkubwa visiwani Zanzibar iliongoza Zanzibar kwa kufanya vizuri yaani ilitoa div 1 zaidi ya 15, div 2 za kumwaga kati ya watoto wsiozidi 50. hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutoa idadi kubwa wanafunzi. nadhani hata Baraza la Mitihani la Taifa Necta ilishtuka, iljihoji na ilitaka kujua haya ni matokeo ya Kweli?
Mwaka uliofuta NECTA ilituma ujumbe mzito katika shule hiyo, kwa maneno ya vijana iliwabana vijana sana vijana shule hiyo kwa kuweka Ulinzi mkali kwa usimamizi, ufanyaji wa mitihani, baadhi ya wajumbe kutoka NECTA Makao makuu Walishiriki kikamilifu kusimamia exam shuleni hapo. nasema walishiriki kusimamia, kuchunguza na kuzuia kila aina ya Ujanja, walifikia hata kuwasachi kabla ya exam. matokeo yake wanafunzi waliofanya Exam matukio yao sio mazuri.(naamini hata NECTA kwa hili hawatakanusha).
lKN sijui kama NECTA hufanya mkakati kama huu ktk shule ambazo huwa zinaongoza hasa za seminary? sijui kama wanshtuka kama walivyoshtuka High view? sijui hutumia mkakati kama walivyotumia huko Zenj?

LKN cha kujiuliza jee hawa ndio wanaopta first class Vyuo vikuu? au ndio bogas
Tatizo mlilonalo ni moja tu, kama mki-focus kwenye elimu mtalitatua.......!!!
 
Nashindwa kuelewa inakuwaje wanafunzi/shule ikifanya vizuri inafatiliwa eeh hadi kuhisi kama kuna mchezo umefanyika. Isipofanya vizuri hakuna kinachofanyika.
Kwani lengo la NECTA wanafunzi wafeli au?
 
duh siku hizi madogo hata kupata div 3 imekuwa shida hivi??siku zile hatukuwa tunaulizana div,tulikuwa tunaulizana 'una one ya points ngapi?
 
awali ya yote ningependa kuwapongeza wanafunzi waliokuwa kwenye seminari za kikristo kwa kufanya vizuri, hii sio kwamba waliosoma kwenye shule hizo ni wakristo peke yao humo kuna waislam, wahindu na wabudha pia , so mafanikio ni ya taasisi na wanafunzi bila kujali dini zao
ni ukweli usiopingika kuwa ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri kuna mazingira yanayohitajika ili aweze kufaulu kama vile, uwepo wa walimu wa kutosha na wenye ubora na walio na morali ya kazi, uwepo wa vitendea kazi/zana za elimu k.v vitabu vya ziada,kiada na rejea,uwepo wa maktaba, uwepo wa maabara, mazingira rafiki ya elimu, standi za kufundishia, na kadhalika wa kadhalika

kitu kimoja kizuri kwenye shule za kikristo ni mfumo wao wa kutoa elimu kwani bahati nzuri nyingi ya shule hizi huwa wana karibu vitu vyote vilivyotajwa hapo juu, maana aidha shule hizi huanzishwa na makanisa yenye sadaka kubwa, misaada toka nje ya nchi au huwa wanatoza ada kubwa kwa ajili ya kumudu gharama za uendeshaji na pia idadi ya wanafunzi katika shule hizi huwa haizidi 100 kwa kidato aghalabu 50 hivi. bahati mbaya kwa shule za kiislamu huendeshwa kwa shida zikikabiliwa na changamoto nyingi za uendeshaji na ukosefu wa fedha,lakini hili hutokea zaidi kwa kuwa shule hizi zinatoza ada ambayo ni kidogo sana ukilinganisha na shule za kikristo maana zinafahamu hali ya maisha ya watanzania na kwa kuwa ada huwa ndogo hupelekea wanafunzi kuwa wengi kwenye shule hizi kitu ambacho hukompromise ubora wake
pamoja na hayo tujiulize mbona kuna seminari au shule zenye majina ya 'watakatifu' wa kikiristo na bado zafanya vibaya?zingine zipo dar hapohapo na zingine zipo huko mikoani? mtu aangalie shule mfano ST PAUL'S LIULI, DAR ES SALAAM CHRISTIAN SEMINARY, DAR ES SALAAM BAPTIST SECONDARY, BANGALA LUTHERAN JUNIOR SEMINARY, ANGALIA SHULE KAMA HII

S0983 TUMAINI LUTHERAN SEMINARY <H3>DIV-I = 0 DIV-II = 3 DIV-III = 3 DIV-IV = 44 FLD = 30

SASA tatizo hapa ni nini? ni ubora wa wanafunzi au kukosekana kwa mazingira bora ya kielimu? maana hii pia ni shule ya kanisa

binafsi watanzania tuache kulumbana na kujisifu kwamba eti shule ya dini/dhehebu fulani ni nzuri kuliko ya dini/dhehebu jingine ilhali wanaosoma kwenye shule hizo wengi wao ni watoto wa watanzania wenye kipato cha kati na sio watanzania wenye kipato cha chini, hivi tujiulize mwanafunzi kutoka kule interior kabisa nkasi, nachingwea, kibondo, ludewa, ikunguluyabashashi, kilolo, kieto huko zoisa banyibanyi, kilosa kule ureling'ombe au tanganganyika masagati ifakara je anaweza mudu shule hizo mnazojisifia nazo? ndio maana serikali imekuwa ikiwaomba wamiliki wa shule wapunguze ada. kumbukeni wanaosoma shule hizi ni watanzania na wanaofeli ni watanzania wote pasi na kujali dini zao kwani wakristo kwa waislamu

lakini swali langu dogo ni kuwa kwanini seminari siku zote hazishiki namba kwenye mitihani ya kidato cha sita??? sikuzote kumi bora zimekuwa zikitawaliwa zaidi na shule za serikali kama vile ilboru, kibaha, mzumbe, kilakala, dakawa, msalato and the like?? kwa nini hawa wanaseminari huongoza kidato cha nne na hushindwa kidato cha sita? na mbona wanaseminari hawa pindi wajapo huku kwenye shule zetu za serikali huwa tunawaburuza mbaya kwenye performance darasani kama wao ni vichwa ile mbaya?
kwa hiyo mazingira rafiki huwasaidia wanafunzi wa seminari lakini haithibitishi kwamba wao ni bora sana kuliko wanafunzi walioko kwenye shule za kawaida


</H3>
acha wongo wewe zile shule za seminary zenye A level huwa zinafanya vizuri pia hata A level! na suala la mwanafunzi kutofanya vizuri chuoni sidhani kama kuna ukweli hapo! na hata kama inatokea basi ni suala binafsi la mwanafunzi huyo labda kuacha kuzingatia masomo na si ati seminary hutoa wanafunzi bogus kama unavyotaka kumaanisha!
 
cha ajabu hata mwanae Mwamvita Makamba hajawahi saidia hiyo shule hata madawati kumsitiri babake though yuko Vodacom na anashughulika na mambo ya Corporate Social Responsibility (CSR)
 
Matokeo ya kidato cha nne 2010 yanatishia hatima ya nchi yetu,na tusipobadilika na kuona umuhimu wa elimu bora katika zama hizi za ubepari,basi kama taifa tumekwisha.
Hebu angalia matokeo ya Shule ya Sekondari Lufyilo ambayo ipo katika wilaya ya Rungwe,Lufilyo ndio nyumbani kabisa kwa Prof:Mark Mwandosya,waziri wa maji.

Summary ya matokeo ni kama ifuatavyo;

DIV-1=0
DIV-2=0
DIV-3=2
DIV-4-47
FLD- 73

Hayo ndiyo mazao ya fikra za ccm katika kuendesha nchi. Ukisoma hotuba za viongozi wa chama na serikali unaweza kudanganyika kwamba kweli nchi imepiga hatua katika elimu kumbe hatua inayoongelewa ni idadi ya shule zilizoongezeka na wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari na siyo ubora wa elimu inayotolewa kwa wanafunzi hata kama ni wachache. Kwa maneno mengine, viongozi wa ccm na serikali yao wanajisifu kwa UWINGI (quantity) wa wanafunzi na siyo UBORA (quality) wa elimu. Safari bado ni ndefu sana.
 
Sasa ulitaka afanyaje ili kuboresha hayo matokea? Au awape majibu? Au awe anaenda kuwafundisha?
 
mshahara wa dhambi ni mauti, hayo ndio matokeo sahihi ya dhambi ya wananchi kuichagua CCM.
 
Utitiri wa shule za Vodafasta uendane na ubora ktk elimu. Waliopo madarakani wanajisifia elimu imepanda kwa kuangalia idada ya vyumba vya madarasa!
 
kuna link gani kati ya majibu ya shule na Waziri anapotoka?

Nimeamua kupost thread hii kwa makusudi,kwanza ni kawaida kabisa na ni suala la wazi kwamba mbunge anapopata uwaziri,anafanya kila awezalo kunufaisha kwao jambo ambalo ni zuri na ni baya kwa upande mwingine.Mtu anapokuwa waziri anatakiwa kuwa a national leader na si vinginevyo.Mwandosya amejitahidi sana kupendelea kwao,na shule hiyo ina nafuu kwa majengo,walimu,vitabu na mengineyo kuliko shule nyingine za kata huko Rungwe Mashariki.NI MUHIMU SANA TUKATHAMINI MUUNDO WA ELIMU YETU KWA PAMOJA KAMA TAIFA
 
WAKATI mwingine unaweza kusema tumerogwa na hatujui tufanyalo, lakini ukweli ni kuwa kuna kundi la watu wachache hapa nchini ambao wameamua kuitawala nchi kwa mfumo wa kinyonyaji.

Nasema viongozi wetu wamegeuka wakoloni kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele kujali masilahi yao kuliko ya wananchi waliowapa nafasi ya kuingia madarakani.

Leo hii tukiangalia mishahara na marupurupu ya wabunge, mawaziri na watendaji wengine wa serikali utakubaliana nami kuwa nchi yetu si maskini bali wananchi ndio waliolazimishwa waamini hivyo.

Mwalimu wa sekondari aliyeajiriwa na serikali mshahara wake kwa mwezi hauzidi sh laki tano lakini mbunge mshahara na marupurupu yake si chini ya sh milioni saba.

Mbunge huyu kila anapokwenda analala kwenye nyumba, hoteli nzuri tena anakopeshwa gari lakini mwalimu anayebeba jukumu la kuwatoa tongotongo za ujinga wanafunzi hana hata baiskeli.

Leo hii tukiangalia shule za kata hazina walimu, madawati na vifaa mbalimbali vya kujifunzia na kufundishia lakini kila kukicha serikali yetu imekuwa ikinunua magari ya kifahari, matumizi ya anasa na mengineyo.

Katika mazingira kama haya kamwe shule za kata haziwezi kutoa elimu bora bali zitabakia kuwa kijiwe cha watoto masikini kukutana na kubadilishana michezo na mawazo
Matokeo ya kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni ndiyo yamethibitisha kuwa shule hizo ni sawa na vijiwe, kwani wanafunzi wake wamefeli kwa zaidi ya asilimia 80 wakati zile za wenye uwezo wa kifedha ndizo zilizoongoza kwa kufanya vizuri zaidi.

Nilisoma matokeo yale yalinionyesha kuwa shule ya mtakatifu fulani, waliopata daraja la kwanza ni 40, daraja la pili 28 daraja la tatu 15, daraja la nne na sifuri hakuna mwanafunzi aliyepatikana.

Nilipoangalia kwenye shule za kata ambazo ndizo watoto wa walalahoi wengi wanakosoma niliona daraja la kwanza 0, daraja la pili 0, daraja la tatu 10, daraja la nne 20 na waliopata sifuri ni 30.

Kimsingi leo hii ukitaka mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yake ni lazima umpeleke katika shule za mtakatifu fulani ambazo ndizo zenye kutoa wahitimu bora kila mwaka.

Sababu ya shule hizo kutoa wahitimu bora ni kuwa zina mazingira mazuri ya ufundishaji, zinawalipa vizuri walimu, zina vifaa vya kujifunzia na kufundishia
Mlalahoi wa Tanzania hawezi kumudu gharama za shule hizo hivyo katika mazingira ya kawaida ni kwamba sasa kunaanza kujengeka matabaka ya kielimu ambayo nina hakika huko tuendako yatakuja kuleta machafuko.

Watawala wetu hawataki kurekebisha na kuboresha mfumo wa elimu kwa hofu kuwa idadi kubwa ya wahitimu watakapopata elimu bora watakuwa wa kwanza kudai haki na mgawanyo sawa wa rasilimali za taifa.

Wabunge wetu nao wamelambishwa asali na wamebaini utamu wake, kila kukicha wanajiandalia mazingira mazuri ya kuvuna fedha, mara utasikia mfuko wa jimbo, mara bima ya afya, mara mafao ya pensheni na mengineyo.

Hawataki kujishughulisha na uhaba wa madawati katika shule za kata, hawataki kusikia uhaba wa nyumba za walimu, wameziba masikio juu ya kilio cha watoto wa masikini kutopatiwa mikopo ya elimu ya juu.

Wanataka idadi kubwa ya Watanzania iendelee kuwa chini kielimu ili waendelee kuwatawala lakini wanasahau kuwa uvumilivu una mwisho wake kama ilivyotokea kwa wenzetu wa Misri, Tunisia na kwingineko.

Leo hii gari moja analotembelea waziri ambalo ni zaidi ya sh milioni 100 linaweza kununua madawati lukuki, linaweza kujenga zahanati au kituo kimoja cha afya ambacho kitawahudumia watu wengi zaidi.

Kila waziri anapokwenda kufungua warsha au kongamano hulipwa laki saba (700,000) mpaka milioni moja (1,000,000) fedha hizo ni mishahara ya walimu watatu wa sekondari kwa mwezi lakini analipwa kiongozi kwa siku.

Wabunge wetu hivi sasa wanafundishwa kanuni za Bunge pamoja na kuelekezwa mambo wanayopaswa kufanywa wakiwa bungeni lakini kubwa zaidi kila siku huondoka na kiasi kisichopungua lakini moja.

Hivi ni sawa na haki katika nchi inayodaiwa maskini isiyo na walimu, madawati, vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika shule zake viongozi kuogelea katika dimbwi la mamilioni ya fedha kama hivi wafanyavyo viongozi wetu?

Viongozi wetu wanahubiri kupunguza matumizi lakini wanatenda kile wasichokihubiri, wapo mstari wa mbele kutafuna rasilimali za taifa kwa manufaa yao.

Kwa nini tuwe na shule za kata zisizo na walimu, madawati, vitabu na mahitaji mengine wakati tuna rasilimali kuluki zikiwemo dhahabu, almasi, tanzanite, mbuga za wanyama na nyinginezo?

Watawala lazima wajiandae kung’oka madarakani kama pengo kati ya walionacho na wasionacho litazidi kuongezeka, uvumilivu na amani tulivyonavyo leo hii vitatoweka kadiri umaskini utakavyotamalaki kwa wananchi.

Nina hakika shule za kata ndizo zitakazokuwa chanzo cha kuwang’oa madarakani viongozi wetu kwa sababu wanafunzi, wazazi na walezi hawatakubali kuendelea kuona shule hizo zikiwa duni kwa sababu ya kukosekana kwa walimu na vitendea kazi wakati viongozi wao wakiishi maisha ya anasa ya kubadilisha magari na hoteli kila siku.

Inasikitisha zaidi kuwa hivi sasa tayari wataalamu na viongozi wetu wameanza kuzungumzia jambo hilo na kuangalia kinachosababisha wanafunzi wa shule za kata wamefeli mitihani yao.

Mwaka jana walikutanika pale mkoani Dodoma kujadili matokeo mabaya ya kidato cha pili, hasa kwa shule za kata, hawakupenda kutumia akili zao kwenda kujifunza kwenye shule zilizofanya vizuri zaidi.

Nina imani kama wangetumia muda kwenda kwenye hizo shule za mtakatifu fulani na kuzungumza na walimu na wamiliki wao wangepata mwanga wa kile kinachoshindikana katika shule za kina Lowassa, Kikwete, Makamba na nyinginezo.

Wasingetumia fedha nyingi kama walivyokaa Dodoma, ambako walilipwa posho, walipangiwa kwenye hoteli za gharama kubwa na serikali pia iliingia hasara kwa kutumia fedha nyingi kwa jambo lililo wazi.

Nasema wazi kuwa serikali ilipata hasara kubwa kwa sababu matokeo ya mkutano wao ndiyo yameonekana kwenye mtihani wa kidato cha nne.

Bila shaka wataalamu wale waliamua kwenda kujifungia Dodoma ikiwa ni njia ya kuhalalisha ufujaji wa fedha za walalahoi ambao kila kukicha wanakamuliwa kupitia kodi mbalimbali.

Fedha walizozitumia kwenye mkutano huo zingeweza kununulia madawati, kukarabati au kujenga nyumba za walimu, kununulia vitabu na vifaa vinginevyo. Kifupi ni kuwa hawakuwa na uchungu na matatizo ya elimu.

Hapa wanataka kuundwa kwa tume za kuchunguza jambo hilo, tume hizi ni ulaji tu, kwa sababu hakuna kisichojulikana juu ya matokeo mabovu kwa shule hizo.

Tunahitaji kuboresha mazingira ya kujifunzia na ufundishaji, kuwa na walimu wa kutosha pamoja na kuwalipa vizuri kama wanavyofanya wamiliki wa shule za mtakatifu fulani.

Mwalimu mwenye mshahara mzuri, nyumba nzuri, vitabu vya kiada na ziada, kwa vyovyote ataweza kufundisha kwa ufanisi mkubwa na hata matunda yake yataonekana.

Kama serikali isipofanya hayo, elimu yetu haiwezi kuwa bora. Unapopanda mahindi kamwe huwezi kuvuna karanga, tunahitaji kuangalia tulipojikwaa na si tulipoangukia.
 
Nimeamua kupost thread hii kwa makusudi,kwanza ni kawaida kabisa na ni suala la wazi kwamba mbunge anapopata uwaziri,anafanya kila awezalo kunufaisha kwao jambo ambalo ni zuri na ni baya kwa upande mwingine.Mtu anapokuwa waziri anatakiwa kuwa a national leader na si vinginevyo.Mwandosya amejitahidi sana kupendelea kwao,na shule hiyo ina nafuu kwa majengo,walimu,vitabu na mengineyo kuliko shule nyingine za kata huko Rungwe Mashariki.NI MUHIMU SANA TUKATHAMINI MUUNDO WA ELIMU YETU KWA PAMOJA KAMA TAIFA

Ulichotaka kutuambia kwamba ni mpendeleaji kumbe du! kazi tunayo mimi nilidhani unataka kutuelezea ubaya wa CCM kwa matokeo haya kumbe mwenzetu una Agenda nyingine sikuelewi ati! kwa hiyo mawaziri wengine wao hawakujenga nzuri kwao eeh au wao zimefanya vizuri na huku walikuwa watu safi hawakupendelea za kwao ni watu safi hahahahahaha mawazo yako yamenichekesha kweli mepesi!

Elimika kwamba CCM wana sera mbaya wadogo zetu wamefeli nchi nzima,wao wamejenga shule nyingi kwa sifa zisizo na quality yoyote na wala hakuna waalimu,Tuungane pamoja tuikate CCM achana na mambo ya Mwandosya usitupotoshe focus yetu yakuleta mabadiliko ya kweli na hatutaki umbeya hapa
 
Ulafi na ubinafsi wa fisi ndo unatawala!

nashangaa hakuna hata wa kutetea nchi hii kodi juu mishahara ya wafanyakazi level ya chini inakatwa wakati level ya juu inaongezwa wakitaka kuandamana wanapigwa mkwara sasa twende wapi jameni!
 
Hii inanikumbusha usemi usemao mwenye nacho ataongezewa
 
yeah ila sasa hawaangalii sekta ya Elimu ndiyo injini ya taifa taifa lisilo na elimu litakuwa finyu sana kimaendeleo na kiwango cha elimu kinategemea sana na uboreshaji wa miundombinu yake!

Hii inanikumbusha usemi usemao mwenye nacho ataongezewa
 
Nawasalimu wanamember wenzangu wadadavuaji wa mambo..yani cjui macho yangu yameona vibaya au ni vipi?ni hivi katika gazeti la jana la nipashe-28th january 2011 nimeona kama kuna picha la skuli ya makamba katika darasa mojawapo,je waungwana mazingira kama haya ni mazuri na yatachangia matokeo mazuri au mwenyejina YUSUPH MAKAMBA anaona fahari kwa hayo matokeo,na ningemwona mwenye busara kama hayo matokeo angetolea ufafanuzi kama anavyokuwa mwepesi wa kufafanua mambo huku akinukuu vifungu vya holy bible na holy quran...wanajf ninachoomba kwa mwenye gazeti la jana anipatie picha ya hlo darasa la makamba sec. school...nawasilisha mada

Shule hiyo imeanzishwa ili wapate ushindi wa kishindo kwa kura za wazazi wa watoto ktk kila uchaguzi
 
Back
Top Bottom