MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Tatizo mlilonalo ni moja tu, kama mki-focus kwenye elimu mtalitatua.......!!!
 
Nashindwa kuelewa inakuwaje wanafunzi/shule ikifanya vizuri inafatiliwa eeh hadi kuhisi kama kuna mchezo umefanyika. Isipofanya vizuri hakuna kinachofanyika.
Kwani lengo la NECTA wanafunzi wafeli au?
 
duh siku hizi madogo hata kupata div 3 imekuwa shida hivi??siku zile hatukuwa tunaulizana div,tulikuwa tunaulizana 'una one ya points ngapi?
 
acha wongo wewe zile shule za seminary zenye A level huwa zinafanya vizuri pia hata A level! na suala la mwanafunzi kutofanya vizuri chuoni sidhani kama kuna ukweli hapo! na hata kama inatokea basi ni suala binafsi la mwanafunzi huyo labda kuacha kuzingatia masomo na si ati seminary hutoa wanafunzi bogus kama unavyotaka kumaanisha!
 
cha ajabu hata mwanae Mwamvita Makamba hajawahi saidia hiyo shule hata madawati kumsitiri babake though yuko Vodacom na anashughulika na mambo ya Corporate Social Responsibility (CSR)
 

Hayo ndiyo mazao ya fikra za ccm katika kuendesha nchi. Ukisoma hotuba za viongozi wa chama na serikali unaweza kudanganyika kwamba kweli nchi imepiga hatua katika elimu kumbe hatua inayoongelewa ni idadi ya shule zilizoongezeka na wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari na siyo ubora wa elimu inayotolewa kwa wanafunzi hata kama ni wachache. Kwa maneno mengine, viongozi wa ccm na serikali yao wanajisifu kwa UWINGI (quantity) wa wanafunzi na siyo UBORA (quality) wa elimu. Safari bado ni ndefu sana.
 
Sasa ulitaka afanyaje ili kuboresha hayo matokea? Au awape majibu? Au awe anaenda kuwafundisha?
 
mshahara wa dhambi ni mauti, hayo ndio matokeo sahihi ya dhambi ya wananchi kuichagua CCM.
 
Utitiri wa shule za Vodafasta uendane na ubora ktk elimu. Waliopo madarakani wanajisifia elimu imepanda kwa kuangalia idada ya vyumba vya madarasa!
 
kuna link gani kati ya majibu ya shule na Waziri anapotoka?

Nimeamua kupost thread hii kwa makusudi,kwanza ni kawaida kabisa na ni suala la wazi kwamba mbunge anapopata uwaziri,anafanya kila awezalo kunufaisha kwao jambo ambalo ni zuri na ni baya kwa upande mwingine.Mtu anapokuwa waziri anatakiwa kuwa a national leader na si vinginevyo.Mwandosya amejitahidi sana kupendelea kwao,na shule hiyo ina nafuu kwa majengo,walimu,vitabu na mengineyo kuliko shule nyingine za kata huko Rungwe Mashariki.NI MUHIMU SANA TUKATHAMINI MUUNDO WA ELIMU YETU KWA PAMOJA KAMA TAIFA
 
WAKATI mwingine unaweza kusema tumerogwa na hatujui tufanyalo, lakini ukweli ni kuwa kuna kundi la watu wachache hapa nchini ambao wameamua kuitawala nchi kwa mfumo wa kinyonyaji.

Nasema viongozi wetu wamegeuka wakoloni kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele kujali masilahi yao kuliko ya wananchi waliowapa nafasi ya kuingia madarakani.

Leo hii tukiangalia mishahara na marupurupu ya wabunge, mawaziri na watendaji wengine wa serikali utakubaliana nami kuwa nchi yetu si maskini bali wananchi ndio waliolazimishwa waamini hivyo.

Mwalimu wa sekondari aliyeajiriwa na serikali mshahara wake kwa mwezi hauzidi sh laki tano lakini mbunge mshahara na marupurupu yake si chini ya sh milioni saba.

Mbunge huyu kila anapokwenda analala kwenye nyumba, hoteli nzuri tena anakopeshwa gari lakini mwalimu anayebeba jukumu la kuwatoa tongotongo za ujinga wanafunzi hana hata baiskeli.

Leo hii tukiangalia shule za kata hazina walimu, madawati na vifaa mbalimbali vya kujifunzia na kufundishia lakini kila kukicha serikali yetu imekuwa ikinunua magari ya kifahari, matumizi ya anasa na mengineyo.

Katika mazingira kama haya kamwe shule za kata haziwezi kutoa elimu bora bali zitabakia kuwa kijiwe cha watoto masikini kukutana na kubadilishana michezo na mawazo
Matokeo ya kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni ndiyo yamethibitisha kuwa shule hizo ni sawa na vijiwe, kwani wanafunzi wake wamefeli kwa zaidi ya asilimia 80 wakati zile za wenye uwezo wa kifedha ndizo zilizoongoza kwa kufanya vizuri zaidi.

Nilisoma matokeo yale yalinionyesha kuwa shule ya mtakatifu fulani, waliopata daraja la kwanza ni 40, daraja la pili 28 daraja la tatu 15, daraja la nne na sifuri hakuna mwanafunzi aliyepatikana.

Nilipoangalia kwenye shule za kata ambazo ndizo watoto wa walalahoi wengi wanakosoma niliona daraja la kwanza 0, daraja la pili 0, daraja la tatu 10, daraja la nne 20 na waliopata sifuri ni 30.

Kimsingi leo hii ukitaka mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yake ni lazima umpeleke katika shule za mtakatifu fulani ambazo ndizo zenye kutoa wahitimu bora kila mwaka.

Sababu ya shule hizo kutoa wahitimu bora ni kuwa zina mazingira mazuri ya ufundishaji, zinawalipa vizuri walimu, zina vifaa vya kujifunzia na kufundishia
Mlalahoi wa Tanzania hawezi kumudu gharama za shule hizo hivyo katika mazingira ya kawaida ni kwamba sasa kunaanza kujengeka matabaka ya kielimu ambayo nina hakika huko tuendako yatakuja kuleta machafuko.

Watawala wetu hawataki kurekebisha na kuboresha mfumo wa elimu kwa hofu kuwa idadi kubwa ya wahitimu watakapopata elimu bora watakuwa wa kwanza kudai haki na mgawanyo sawa wa rasilimali za taifa.

Wabunge wetu nao wamelambishwa asali na wamebaini utamu wake, kila kukicha wanajiandalia mazingira mazuri ya kuvuna fedha, mara utasikia mfuko wa jimbo, mara bima ya afya, mara mafao ya pensheni na mengineyo.

Hawataki kujishughulisha na uhaba wa madawati katika shule za kata, hawataki kusikia uhaba wa nyumba za walimu, wameziba masikio juu ya kilio cha watoto wa masikini kutopatiwa mikopo ya elimu ya juu.

Wanataka idadi kubwa ya Watanzania iendelee kuwa chini kielimu ili waendelee kuwatawala lakini wanasahau kuwa uvumilivu una mwisho wake kama ilivyotokea kwa wenzetu wa Misri, Tunisia na kwingineko.

Leo hii gari moja analotembelea waziri ambalo ni zaidi ya sh milioni 100 linaweza kununua madawati lukuki, linaweza kujenga zahanati au kituo kimoja cha afya ambacho kitawahudumia watu wengi zaidi.

Kila waziri anapokwenda kufungua warsha au kongamano hulipwa laki saba (700,000) mpaka milioni moja (1,000,000) fedha hizo ni mishahara ya walimu watatu wa sekondari kwa mwezi lakini analipwa kiongozi kwa siku.

Wabunge wetu hivi sasa wanafundishwa kanuni za Bunge pamoja na kuelekezwa mambo wanayopaswa kufanywa wakiwa bungeni lakini kubwa zaidi kila siku huondoka na kiasi kisichopungua lakini moja.

Hivi ni sawa na haki katika nchi inayodaiwa maskini isiyo na walimu, madawati, vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika shule zake viongozi kuogelea katika dimbwi la mamilioni ya fedha kama hivi wafanyavyo viongozi wetu?

Viongozi wetu wanahubiri kupunguza matumizi lakini wanatenda kile wasichokihubiri, wapo mstari wa mbele kutafuna rasilimali za taifa kwa manufaa yao.

Kwa nini tuwe na shule za kata zisizo na walimu, madawati, vitabu na mahitaji mengine wakati tuna rasilimali kuluki zikiwemo dhahabu, almasi, tanzanite, mbuga za wanyama na nyinginezo?

Watawala lazima wajiandae kung’oka madarakani kama pengo kati ya walionacho na wasionacho litazidi kuongezeka, uvumilivu na amani tulivyonavyo leo hii vitatoweka kadiri umaskini utakavyotamalaki kwa wananchi.

Nina hakika shule za kata ndizo zitakazokuwa chanzo cha kuwang’oa madarakani viongozi wetu kwa sababu wanafunzi, wazazi na walezi hawatakubali kuendelea kuona shule hizo zikiwa duni kwa sababu ya kukosekana kwa walimu na vitendea kazi wakati viongozi wao wakiishi maisha ya anasa ya kubadilisha magari na hoteli kila siku.

Inasikitisha zaidi kuwa hivi sasa tayari wataalamu na viongozi wetu wameanza kuzungumzia jambo hilo na kuangalia kinachosababisha wanafunzi wa shule za kata wamefeli mitihani yao.

Mwaka jana walikutanika pale mkoani Dodoma kujadili matokeo mabaya ya kidato cha pili, hasa kwa shule za kata, hawakupenda kutumia akili zao kwenda kujifunza kwenye shule zilizofanya vizuri zaidi.

Nina imani kama wangetumia muda kwenda kwenye hizo shule za mtakatifu fulani na kuzungumza na walimu na wamiliki wao wangepata mwanga wa kile kinachoshindikana katika shule za kina Lowassa, Kikwete, Makamba na nyinginezo.

Wasingetumia fedha nyingi kama walivyokaa Dodoma, ambako walilipwa posho, walipangiwa kwenye hoteli za gharama kubwa na serikali pia iliingia hasara kwa kutumia fedha nyingi kwa jambo lililo wazi.

Nasema wazi kuwa serikali ilipata hasara kubwa kwa sababu matokeo ya mkutano wao ndiyo yameonekana kwenye mtihani wa kidato cha nne.

Bila shaka wataalamu wale waliamua kwenda kujifungia Dodoma ikiwa ni njia ya kuhalalisha ufujaji wa fedha za walalahoi ambao kila kukicha wanakamuliwa kupitia kodi mbalimbali.

Fedha walizozitumia kwenye mkutano huo zingeweza kununulia madawati, kukarabati au kujenga nyumba za walimu, kununulia vitabu na vifaa vinginevyo. Kifupi ni kuwa hawakuwa na uchungu na matatizo ya elimu.

Hapa wanataka kuundwa kwa tume za kuchunguza jambo hilo, tume hizi ni ulaji tu, kwa sababu hakuna kisichojulikana juu ya matokeo mabovu kwa shule hizo.

Tunahitaji kuboresha mazingira ya kujifunzia na ufundishaji, kuwa na walimu wa kutosha pamoja na kuwalipa vizuri kama wanavyofanya wamiliki wa shule za mtakatifu fulani.

Mwalimu mwenye mshahara mzuri, nyumba nzuri, vitabu vya kiada na ziada, kwa vyovyote ataweza kufundisha kwa ufanisi mkubwa na hata matunda yake yataonekana.

Kama serikali isipofanya hayo, elimu yetu haiwezi kuwa bora. Unapopanda mahindi kamwe huwezi kuvuna karanga, tunahitaji kuangalia tulipojikwaa na si tulipoangukia.
 

Ulichotaka kutuambia kwamba ni mpendeleaji kumbe du! kazi tunayo mimi nilidhani unataka kutuelezea ubaya wa CCM kwa matokeo haya kumbe mwenzetu una Agenda nyingine sikuelewi ati! kwa hiyo mawaziri wengine wao hawakujenga nzuri kwao eeh au wao zimefanya vizuri na huku walikuwa watu safi hawakupendelea za kwao ni watu safi hahahahahaha mawazo yako yamenichekesha kweli mepesi!

Elimika kwamba CCM wana sera mbaya wadogo zetu wamefeli nchi nzima,wao wamejenga shule nyingi kwa sifa zisizo na quality yoyote na wala hakuna waalimu,Tuungane pamoja tuikate CCM achana na mambo ya Mwandosya usitupotoshe focus yetu yakuleta mabadiliko ya kweli na hatutaki umbeya hapa
 
Ulafi na ubinafsi wa fisi ndo unatawala!

nashangaa hakuna hata wa kutetea nchi hii kodi juu mishahara ya wafanyakazi level ya chini inakatwa wakati level ya juu inaongezwa wakitaka kuandamana wanapigwa mkwara sasa twende wapi jameni!
 
Hii inanikumbusha usemi usemao mwenye nacho ataongezewa
 
yeah ila sasa hawaangalii sekta ya Elimu ndiyo injini ya taifa taifa lisilo na elimu litakuwa finyu sana kimaendeleo na kiwango cha elimu kinategemea sana na uboreshaji wa miundombinu yake!

Hii inanikumbusha usemi usemao mwenye nacho ataongezewa
 

Shule hiyo imeanzishwa ili wapate ushindi wa kishindo kwa kura za wazazi wa watoto ktk kila uchaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…