mwaka 2008, Shule moja inayoitwa High view sec school inayomikiwa na mmoja ya mfanya biashar mkubwa visiwani Zanzibar iliongoza Zanzibar kwa kufanya vizuri yaani ilitoa div 1 zaidi ya 15, div 2 za kumwaga kati ya watoto wsiozidi 50. hii ni mara ya kwanza kwa shule hiyo kutoa idadi kubwa wanafunzi. nadhani hata Baraza la Mitihani la Taifa Necta ilishtuka, iljihoji na ilitaka kujua haya ni matokeo ya Kweli?
Mwaka uliofuta NECTA ilituma ujumbe mzito katika shule hiyo, kwa maneno ya vijana iliwabana vijana sana vijana shule hiyo kwa kuweka Ulinzi mkali kwa usimamizi, ufanyaji wa mitihani, baadhi ya wajumbe kutoka NECTA Makao makuu Walishiriki kikamilifu kusimamia exam shuleni hapo. nasema walishiriki kusimamia, kuchunguza na kuzuia kila aina ya Ujanja, walifikia hata kuwasachi kabla ya exam. matokeo yake wanafunzi waliofanya Exam matukio yao sio mazuri.(naamini hata NECTA kwa hili hawatakanusha).
lKN sijui kama NECTA hufanya mkakati kama huu ktk shule ambazo huwa zinaongoza hasa za seminary? sijui kama wanshtuka kama walivyoshtuka High view? sijui hutumia mkakati kama walivyotumia huko Zenj?
LKN cha kujiuliza jee hawa ndio wanaopta first class Vyuo vikuu? au ndio bogas
Kwa kuwa NECTA hawajaenda huko shule za seminary kufanya hayo usemayo, hatuwezi kulizungumzia hilo kwa sasa. tuzungumzie tunayoyafahamu. shule zinazofanya vizuri ni kama vile tu timu za mpira zinazofanya vizuri, ni kama nchi zinazofaulu kiuchumi, ni kama hata akina wewe na mimi tunapojipanga vema mikakati, kimaisha unafanikiwa kwa namna fulani. haiwezekani baba mlevi, anatumia fedha ovyo, kuwe na amani na maendeleo nyumbani. nchi inayowekeza vizuri katika elimu, inakuwa na mipango mizuri na kuitekeleza, matokeo yataonekana. shule inayowekeza katika walimu wake, vifaa vya kufundishia, mipango makini inayotekelezwa, mafanikio yataonekana.
Lakini ni kweli pia kwamba shule ikishakuwa na historia ya kufanya vizuri, ni rahisi zaidi kuendeleza hali hiyo. kwa mfano, vijana wengi wanaofanya vizuri watakwenda kufanya interview katika shule zinazofanya vizuri, na kwa hiyo cream ya taifa inajazana sehemu hizo. kwa hiyo kama Interview wamefanya vijana 1,000 na wanaotakiwa ni 100, maana yake wakichukua the best 100, watakuwa wamechota cream tupu. sasa hapo kwa kuanzia vijana ni safi na kwa hiyo ukichanganya na mipango yao mizuri, kwa nini wasifanye vizuri? lakini ukianza kuwa na historia ya kufanya vibaya, basi hata wanafunzi unaopata ni wale walioshindikana sehemu nyingine, wavuta bangi, wakorofi, na hawana interest ya kusoma. hapo itakuwa ni vicious circle ya kufanya vibaya na vibaya zaidi. hapa shule itahitaji kufanya mkakati mkali sana wa kubadili mwelekeo huo. unaweza hata kuanza kwa kubadili jina, kubadili uongozi, kupaka rangi majengo, kuwekeza zaidi na kuleta vifaa zaidi, walimu wazuri zaidi kwa malipo mazuri zaidi. unaweza hata kwenda kukwapua walimu wazuri toka shule zinazofanya vizuri kwa malipo mazuri zaidi. hapo sasa ukianza kutoa matokeo mazuri, utapata vijana wazuri na utaanza mzunguko wa kuongezewa.
Kumbuka kwamba Seminari ni hasa kwa ajili ya Mapadri na wachungaji. lakini wanaojaa huko ni wale hasa wanaojiona kwamba wanao uwezo wa kufanya vizuri darasani na wanatumia seminari kama shule ya kawaida tu ili wasonge mbele. wanakwenda Seminari kwa sababu tu ya kufuata elimu nzuri na malezi mazuri. wazazi wengi wanapeleka watoto wao Seminari sio kwa sababu ya kutaka wawe wachungaji au mapadri, lakini ili wapate elimu nzuri ya huko.
nadhani tujikite kwenye mwelekeo kama huu, badala ya kunyooshea vidole wanaofaulu kwamba hawafai kufaulu, badala yake wale wanaofanya vibaya wajifunze kwa wale wanaofaulu kwamba wenzetu wanafanyaje? ili nao wafanye vizuri. kutafuta mchawi au visingizio haisaidii