Njimba Nsalilwe
JF-Expert Member
- Mar 23, 2008
- 252
- 3
Naam waungwana, matokeo rasmi ya jimbo la nzega kwa wagombea wawili waliokuwa wakichuana sana ni kaam nilivyoandika hapo juu, japo najua kwa kufanya hivi nitaporomoshewa matusi ya kumwaga ila ukweli ndio huo nami binafsi nimeongoza kwa kishindo kura za maoni nafasi ya udiwani
Keil,
Naliongelea kuhamia CHADEMA kwa sababu moja kubwa kuwa tayari atazoa baadhi ya watu wake na ahame nao CHADEMA. Chadema tayari watakuwa na wajumbe wengi ambao ni PRO Mwakalinga na si Pro CCM.
Hii zaidi ipo kama njia ya kusaidia KULINDA kura za Slaa kwenye uchaguz wa RAIS.
Kwa hali ilivyo sasa, sidhani kama atataka tena kurudi kwenye SIASA. Sintashangaa akirudi zake UK na kwenda kubeba Box za Kichina kama watamhitaji au abadili kazi kabisa. Kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Familia yake itakuwa upande fulani happy kuwa baba KARUDI.
Anyway, kwenye maisha huwa kuna kushinda MAPIGANO na kushinda VITA. Only God knows nani atakuwa mshindi wa VITA. Ndiyo maana huwa wanasema "Mchekaji, ni yule anacheka wa MWISHO."
Ngoja tusubiri matokeo ya SIKONGE sasa na DR. SLAA kivumbi kikianza.
Mgombea tiketi ya Ubunge kupitia CCM jimbo la Kawe, Kippi Warioba amempita mgombea wa pili Angela Kizigah kwa kura 700. Fisadi Adamjee kaangukia pua! Eric Suma nae chali!
Sitegemei kuna mtu atashindana na Mwandosya kule kwa sasa, hata wapinzani wanakiri Mwandosya ni maji marefu. Ni sawa na kutaka kushindana na Magufuli jimboni kwake, unatakiwa kufanya miujiza. Mwandosya japo yuko DSM karibu kila mwezi anapita jimboni kwake kuhimiza maendeleo na anajitolea sana. Sio msemaji sana lakini ni mtendaji mahiri, sayansi kweli anaitumia vizuri.
Mgombea tiketi ya Ubunge kupitia CCM jimbo la Kawe, Kippi Warioba amempita mgombea wa pili Angela Kizigah kwa kura 700. Fisadi Adamjee kaangukia pua! Eric Suma nae chali!
Kutoka Njombe, Makweta ameanguka vibaya, akishika nafasi kama ya tatu hivi. Matokeo ya awali yanaonyesha Deo Sanga anaongoza, akifuatiwa na Alatanga Nyagawa.
Mwakaluinga na kundi lake la mafisadi chali mbaya
Kwanza hongera zako kushinda udiwani, pili hongera kwa Bashe kumshinda mpiganaji Seleli hata kama ni kwa kutumia masalia/mabaki ya Kagoda.Naam waungwana, matokeo rasmi ya jimbo la nzega kwa wagombea wawili waliokuwa wakichuana sana ni kaam nilivyoandika hapo juu, japo najua kwa kufanya hivi nitaporomoshewa matusi ya kumwaga ila ukweli ndio huo nami binafsi nimeongoza kwa kishindo kura za maoni nafasi ya udiwani
Kwanza hongera zako kushinda udiwani, pili hongera kwa Bashe kumshinda mpiganaji Seleli hata kama ni kwa kutumia masalia/mabaki ya Kagoda.
Wapenzi wa Selelii wasiwe na shaka, hata kama Bashe angeshinda kwa asilimia 99% na Selelii asilimia 01%, bado CCM itampitisha Selelii na kumtosa Bashe, kuna secret agreement kwa wabunge makamanda waliahidiwa kupitishwa no matter what, nao ndio wakakubali kuitosa CCJ.
Hivyo kama wana CCM wa Nzega, wanawakilisha wakazi wote wa Nzega, na chaguo lao ni Bashe, basi atakayekwenda upinzani na awe Bashe, asimame na Selelii kwenye sanduku la kura, hivyo Jimbo la Nzega tuanze kulihesabu upinzani.
Kama na kuchekelea ushindi, kambi ya Bashe, chekeni sana, mkisubiria panga la NEC na mtalia sana, piga ua CCM haiwatemi makamanda wake, almanusura waimege ikatike vipande viwili, wakakubali kuinusuru CCM, sasa ni zamu ya CCM kuwanusuru.
Bashe ajiandae kwa safari, the only choice ni Chadema, tatizo langu kwake ni jee Chadema itawakubali hawa makuwadi wa RA?. Jee itafungua milango yake kuwakaribisha nyoka?.
Mwito wangu kwa Chadema, acha milango wazi kwa yoyote ajaye bila kujali alikuwa akimtumikia nani, concetration yao kwa sasa, iwe ni idadi ya viti vingi bungeni.
Kwa nini kippi naye asiitwe Fisadi Kippi Warioba?