Jamani huko Iringa Prof. Msola, Kandoro na Lukuvi vipi? sioni wakitajwa
hatunMkuu TUNA kila sababu ya kumlaumu Mkapa. Yeye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Chama na alijua fika kuwa tunavaa mkenge. Yeye na Mangula wakiwa ni mwenyekiti na Katibu walikuwa na uwezo mkubwa wa kudeal na issue. Siamini kama wangeshindwa kumshughulikia JK.Mkuu huwezi kusema eti kwa kuwa watoto wote wanataka kitu fulani ambacho kina madhara uwaruhusu, wewe utakuwa si baba. Unapokuwa Baba na unajua kuwa kitu hicho ni hatari kwa watoto hata wakililia vipi ni vema usiwape, bora ulalamikiwe kuliko kuacha waangamie. Look at us now, uchumi unaona mwenyewe unavyoporomoka, utawala bora ambao Mkapa alijaribujaribu unazidi kuporomoka, everything is falling into pieces. Mkapa hawezi kukwepa hili, ni yeye ametuletea matatizo haya. Alitutupa mikononi mwa mafisadi.
Matokeo yaliyoanza kuja kwa kura za maoni jimbo la Kyela;
Tawi la Bondeni-Kyela Mjini;Dr Mwakyembe 220 anayemfuatia kwa karibu Elias Mwanjala kura 6
Tawi la Mikumi-Kyela mjini;Dr Mwakyembe 176,wa pili Elias Mwanjala kura 4
Tawi la Bwawani-Kyela mjini;Dr Mwakyembe 95 mpinzani wake wa karibu Elias Mwanjala kapata 15
Matokeo mengine Afande Samwel atazidi kuyaleta!
Eeeh huko Iringa patamu. hebu tupe data zaidi, nani ameshida Njombe kaskazini, Kusini na magharibi?Lukuvi ameshinda Isimani,Kandoro kaanguka,kilolo kuna vurugu mpaka dakika hii matokeo bado kuna vituo hawajapiga kura,
Mungai aanguka,Malangalila Anguka ,yono kivela nje, Makweta nje Mwalyosi nje,mbeha nje
Wacha wamtose akaanze rasmi kazi ya kuwapiga chapa usoni wenye virusi vya UKIMWI kama alivyoshauri.L.......Yono Kivela nje, ........
Kama hayo hapo juu ni kweli,Karne ya 21 Salelii anaamini kuna secret Agreement kwenye siasa sio kwamba tu hajui siasa but he doesnt use common sense as well.Kwanza hongera zako kushinda udiwani, pili hongera kwa Bashe kumshinda mpiganaji Seleli hata kama ni kwa kutumia masalia/mabaki ya Kagoda.
Wapenzi wa Selelii wasiwe na shaka, hata kama Bashe angeshinda kwa asilimia 99% na Selelii asilimia 01%, bado CCM itampitisha Selelii na kumtosa Bashe, kuna secret agreement kwa wabunge makamanda waliahidiwa kupitishwa no matter what, nao ndio wakakubali kuitosa CCJ.
Hivyo kama wana CCM wa Nzega, wanawakilisha wakazi wote wa Nzega, na chaguo lao ni Bashe, basi atakayekwenda upinzani na awe Bashe, asimame na Selelii kwenye sanduku la kura, hivyo Jimbo la Nzega tuanze kulihesabu upinzani.
Kama na kuchekelea ushindi, kambi ya Bashe, chekeni sana, mkisubiria panga la NEC na mtalia sana, piga ua CCM haiwatemi makamanda wake, almanusura waimege ikatike vipande viwili, wakakubali kuinusuru CCM, sasa ni zamu ya CCM kuwanusuru.
Bashe ajiandae kwa safari, the only choice ni Chadema, tatizo langu kwake ni jee Chadema itawakubali hawa makuwadi wa RA?. Jee itafungua milango yake kuwakaribisha nyoka?.
Mwito wangu kwa Chadema, acha milango wazi kwa yoyote ajaye bila kujali alikuwa akimtumikia nani, concetration yao kwa sasa, iwe ni idadi ya viti vingi bungeni.
labda wanafurahia kwa seleli
ndo tunamalizia kuhesabu 'kula'!...nadhani NITASHINDA!mpaka sasa naongozaJamani Ilembula je?
mramba kapita tena sanaaaa...mzee pesa mbili alifanikiwa kupeleka na kujipatia maendeleo! Killed two birds with one stone, tusikilizie kesi kama inaweza kuwa influenced na kura...or vice versa
wabunge wote wawili wa karagwe (blandes- karagwe na katagila - kyerwa) wameshinda kura za maoni na hivyo watatetea majimbo yao.
Jamani Ilembula je?