Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Jamani huko Iringa Prof. Msola, Kandoro na Lukuvi vipi? sioni wakitajwa

Lukuvi ameshinda Isimani,Kandoro kaanguka,kilolo kuna vurugu mpaka dakika hii matokeo bado kuna vituo hawajapiga kura,
Mungai aanguka,Malangalila Anguka ,yono kivela nje, Makweta nje Mwalyosi nje,mbega nje
 
hatunMkuu TUNA kila sababu ya kumlaumu Mkapa. Yeye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Chama na alijua fika kuwa tunavaa mkenge. Yeye na Mangula wakiwa ni mwenyekiti na Katibu walikuwa na uwezo mkubwa wa kudeal na issue. Siamini kama wangeshindwa kumshughulikia JK.Mkuu huwezi kusema eti kwa kuwa watoto wote wanataka kitu fulani ambacho kina madhara uwaruhusu, wewe utakuwa si baba. Unapokuwa Baba na unajua kuwa kitu hicho ni hatari kwa watoto hata wakililia vipi ni vema usiwape, bora ulalamikiwe kuliko kuacha waangamie. Look at us now, uchumi unaona mwenyewe unavyoporomoka, utawala bora ambao Mkapa alijaribujaribu unazidi kuporomoka, everything is falling into pieces. Mkapa hawezi kukwepa hili, ni yeye ametuletea matatizo haya. Alitutupa mikononi mwa mafisadi.

Mkuu inabidi uelewe kuwa CCM huwa ina sura mbili....on the surface and underneath....hiyo ya kwanza ndio Mwenyekiti na katibu...hiyo nyingine ndio inayoleta mizengwe...Nyerere mwenyewe ilimbana 1985 na 1995 kwa Salim huyohuyo.....sitashangaa Mkapa kukutwa na hilo..BTW yeye ndio alikuwa mtu wa mwisho nadhani kuongea na Nyerere...pengine alimwambia amsimamishe Salim 2005 na sio Kikwete...kukosekana Mangula au mtu wa aina yake ndio kunayumbisha CCM kwa sasa...Makamba?...kandambili kwa kiatu....
 
Hayo maneno nimeyafurahia sana mkuu...km hiyo ndiyo kumfuata mtu kwa karibu basi........tehe tehe tehe....nafurahia ushindi wa mwakyembe...
Matokeo yaliyoanza kuja kwa kura za maoni jimbo la Kyela;

Tawi la Bondeni-Kyela Mjini;Dr Mwakyembe 220 anayemfuatia kwa karibu Elias Mwanjala kura 6

Tawi la Mikumi-Kyela mjini;Dr Mwakyembe 176,wa pili Elias Mwanjala kura 4

Tawi la Bwawani-Kyela mjini;Dr Mwakyembe 95 mpinzani wake wa karibu Elias Mwanjala kapata 15

Matokeo mengine Afande Samwel atazidi kuyaleta!
 
Lukuvi ameshinda Isimani,Kandoro kaanguka,kilolo kuna vurugu mpaka dakika hii matokeo bado kuna vituo hawajapiga kura,
Mungai aanguka,Malangalila Anguka ,yono kivela nje, Makweta nje Mwalyosi nje,mbeha nje
Eeeh huko Iringa patamu. hebu tupe data zaidi, nani ameshida Njombe kaskazini, Kusini na magharibi?
 
L.......Yono Kivela nje, ........
Wacha wamtose akaanze rasmi kazi ya kuwapiga chapa usoni wenye virusi vya UKIMWI kama alivyoshauri.
Samahani, hili oni hata mimi lilinikela na kuniudhi sana
 
Najaribu kupiga simu kupata matokeo ya SIKONGE ila nimekwama kabisa. Kwa sasa nipo safari Geita. Ikitokea mtu akapata matokeo haraka basi aturushie hapa.

Pia kama kuna mtu anafahamu matokeo kati ya John Komba na mpinzani wake Daniel Mangweha.
 
Kwanza hongera zako kushinda udiwani, pili hongera kwa Bashe kumshinda mpiganaji Seleli hata kama ni kwa kutumia masalia/mabaki ya Kagoda.

Wapenzi wa Selelii wasiwe na shaka, hata kama Bashe angeshinda kwa asilimia 99% na Selelii asilimia 01%, bado CCM itampitisha Selelii na kumtosa Bashe, kuna secret agreement kwa wabunge makamanda waliahidiwa kupitishwa no matter what, nao ndio wakakubali kuitosa CCJ.

Hivyo kama wana CCM wa Nzega, wanawakilisha wakazi wote wa Nzega, na chaguo lao ni Bashe, basi atakayekwenda upinzani na awe Bashe, asimame na Selelii kwenye sanduku la kura, hivyo Jimbo la Nzega tuanze kulihesabu upinzani.

Kama na kuchekelea ushindi, kambi ya Bashe, chekeni sana, mkisubiria panga la NEC na mtalia sana, piga ua CCM haiwatemi makamanda wake, almanusura waimege ikatike vipande viwili, wakakubali kuinusuru CCM, sasa ni zamu ya CCM kuwanusuru.

Bashe ajiandae kwa safari, the only choice ni Chadema, tatizo langu kwake ni jee Chadema itawakubali hawa makuwadi wa RA?. Jee itafungua milango yake kuwakaribisha nyoka?.

Mwito wangu kwa Chadema, acha milango wazi kwa yoyote ajaye bila kujali alikuwa akimtumikia nani, concetration yao kwa sasa, iwe ni idadi ya viti vingi bungeni.
Kama hayo hapo juu ni kweli,Karne ya 21 Salelii anaamini kuna secret Agreement kwenye siasa sio kwamba tu hajui siasa but he doesnt use common sense as well.
Secret agreement litafuatwa pale utakapokuwa na nguvu kisiasa kuliko uliongia nao makubaliano ambayo chance ni sawa na ziro
 
Mramba kapita tena sanaaaa...Mzee pesa mbili alifanikiwa kupeleka na kujipatia maendeleo! Killed two birds with one stone, tusikilizie kesi kama inaweza kuwa influenced na kura...or vice versa
 
Jamani kama kuna mwenye taarifa/matokeo kura za maoni mkoani Iringa hasa wilayani Njombe
 
mramba kapita tena sanaaaa...mzee pesa mbili alifanikiwa kupeleka na kujipatia maendeleo! Killed two birds with one stone, tusikilizie kesi kama inaweza kuwa influenced na kura...or vice versa

yesuuuuuuuuuuuuuuu na mariaaaaaaaa na yosepf mtakatifu yaniiiiiiii bado unaamini kuna kesi paleapawomi
 
wabunge wote wawili wa karagwe (blandes- karagwe na katagila - kyerwa) wameshinda kura za maoni na hivyo watatetea majimbo yao.

nani kakwambia hapo ni mwanzo kuna vikao vya kupaka na kupakua wasubiri humo hiyo ndio ccm sasa sijui kura za nini??
 
Back
Top Bottom