Wapo Selelii, Mwapachu, Masilingi
Prof. Mwakyusa ana kazi nzito
Sitta, Mwakyembe, Dewji wapeta
Prof. Mwandosya hakamatiki
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura ya maoni kuchagua wana CCM wanaomba kuteuliwa kugombea ubunge na udiwani katika Jimbo la Chalinze Pwani jana. Rais Kikwete alipiga kura yake kijijini kwake Msoga wilayani Bagamoyo.
Baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana jioni walikuwa wanaongoza huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Profesa David Mwakyusa, akiwa amechwa nyuma katika matokeo ya awali ya kura za maoni za uteuzi wa udiwani na ubunge zilizopigwa jana nchini kote.
Matokeo ya awali, yanaonyesha kwamba, katika Jimbo la Rungwe Magharibi, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Profesa David Mwakyusa, alikuwa ameachwa nyuma na mpinzani wake, Richard Kasesela, aliyejizolea jumla ya kura 1,469 dhidi ya kura 840 alizokuwa amepata Profesa Mwakyusa.
Katika matokeo hayo, pia aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigamboni (CUF) mwaka 2000-2005, Frank Magoba, alikuwa anafanya vibaya katika kinyang'anyiro hicho.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, katika Kata ya Ikuti; Tawi la Lienje, Kasesela (44), Magoba (36), Profesa Mwakyusa (36) na Mwakandube (15); Tawi la Kiobo Juu, Kasesela (101), Profesa Mwakyusa (8), Magoba (6) na Mwakandube (1); Kiobo Chini, Kasesela (186), Profesa Mwakyusa (10), Magoba (7) na Mwakandube (1); Tawi la Ibungu, Kasesela (101), Profesa Mwakyusa (9), Magoba (5) na Mwakandube (2); Tawi la Ikuti, Kasesela (128), Profesa Mwakyusa (31), Magoba (15) na Mwakandube (3); na Tawi la Lumbe, Kasesela (81), Profesa Mwakyusa (21), Magoba (6) na Mwakandube (0).
Kata ya Malindo; Tawi la Kapugi, Profesa Mwakyusa (126), Magoba (77), Kasesela (73) na Mwakandube (15)
Kata ya Malimbo; Tawi la Ibungila, Profesa Mwakyusa (191), Kasesela (180), Magoba (20) na Mwakandube (12); Tawi la Igalamo, Profesa Mwakyusa (203), Kasesela (16), Magoba (9) na Mwakandube (0); Kata ya Kimo, Profesa Mwakyusa (102), Kasesela (455), Magoba (17) na Mwakandube (7), na Kata ya Swaya, Kasesela (101), Profesa Mwakyusa (103), Magoba (0) na Mwakandube (0).
Katika Jimbo la Kyela, mkoani Mbeya, Dk. Harrison Mwakyembe aliibuka mshindi, baada ya kuwabwaga wapinzani wake wanne kwa kujizolea jumla ya kura 7,457 na kufuatiwa na George Mwakalinga aliyepata kura 525, zili Mponda, alikataliwa kupiga kura kwa madai kuwa jina lake halikuonekana kwenye rejista ya wanachama iliyopelekwa na mjumbe wake.
Mosi mwenyewe alisema hizo ni njama za makusudi ambazo ziemefanywa na viongozi wa tawi hilo ili asipige kura kwa kuwa hampendi mgombea wanayemuunga mkono. "Huu uchaguzi wa kata ya Azimio ni kituko hakijawahi kutokea na kwa kweli kwa hili hata nikifukuzwa kwenye chama sijali, nitapigania haki yangu hadi mwisho ... haiwezekani mimi ni kiongozi na nina kadi zote kuanzia ya UWT, UVCCM nakataliwa kupiga kura kwa sababu za kijinga kabisa," alisikika akifoka kwa hasira.
"Mimi nimewasikia kwa masikio yangu wanasema watafanya kila wanaloweza kuhakikisha wanamweka mtu wao na njama zote hizo zimefanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa...wamefanya hila kila wanayeona hamuungi mkono mgombea wao wanamwondoa kwenye rejista ya wanachama na mimi jina langu lilikuwepo limekatwa mstari," alisema Mosi huku akifoka nje ya ofisi ya tawi hilo ambako kura zilikuwa zikiendelea kupigwa.
Katibu wa CCM tawi hilo, Badru Kichupa, alisema inawezekana jina la Mosi halikupelekwa kituoni hapo na mjumbe wake hivyo yeye hapaswi kulaumiwa.
CHANZO: NIPASHE