nabii7y7
New Member
- Jun 12, 2023
- 3
- 3
UTANGULIZI
Jamii asilila ni kikundi au mkusanyiko wa watu wanaoishi kwa pamoja katika eneo la kijiografia moja wakitambulika na kuunganishwa na historia na utamaduni unaofanana wakiishi katika misingi na utaratibu waliojiwekea, mfano wa jamii ya watu asilia Tanzania ni pamoja na Wamasai, Wakurya, Wasukuma, Wafipa, Wachanga nk. na bia kusahau kuwa jamii zote zinachimbuko lao asilia na maeneo yao asilia pia.
Bila kupoteza muda napenda kukusogeza moja kwa moja kwenye kiini cha mada hii nzuri sana.
Mikataba ya uchimbaji wa madini, ni makubaliano yanayofanyika baina ya serikali kupitia wizara ya madini pamoja na mtu binafsi au kampuni husika ambapo inaweza kuwa kampuni ya mzawa/wazawa au wawekezaji kutoka nje na madini yanaweza kuwa Dhahabu, Tanzanite Almasi, Kopa, Mafuta, nk. Na mfano wa makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini hapa Tanzania ni pamoja na Acacia, Barrick nk.
Pamoja na uwepo sheria za uchimbaji wa madini nchini ambazo zimekuwa zikiboreshwa mara kwa mara na kushuhudia mageuzi katika sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu na maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Lakini jambo ambalo bado linaonekana kuachwa katika mikataba mingi ya uchimbaji wa madini ni pamoja na kutokuthaminiwa kwa maslahi ya jamii asilila ambayo ndio inayoathirika kwa kiwango kikubwa na shughuli hizi uchimbaji wa madini.
Kwasababu tukiangalia kwa upana zaidi mikataba mingi tengenezwa na kusainiwa ni kwa kiasi kidogo sana inahusisha maoni na mapendekezo ya jamii inayopatikana katika eneo husika.
Kinachofanyika ni kwamba baada ya utafiti kukamilika na kudhibitika kuwa eneo husika lina madini asilimia kubwa wanaohusishwa huwa ni viongozi wa ngazi za juu na viongozi wa ngazi ya chini huwa kama mashuhuda tu maana maagizo yakishatoka kwenye ngazi za juu basi hakuna anaweza kupinga na akasikilizwa.
Kwa mfano: ni ipi nguvu ya diwani, mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kitongoji au wajumbe, pindi mikataba hii inapotengenezwa na kusainiwa?
Au ni nani kati ya viongozi hawa ambaye ana nguvu ya kupinga na kuzuia utekelezwaji wa mikataba hii pale inapoonekana kuwa na udhaifu kwa jamii husika?
Tukumbuke kubwa kabla ya shughuli hizi kuanza jamii asilila pia inakuwa na maslahi na maeneo haya pia, kwa mfano: huenda maeneo haya yalikuwa yakitumika kwa shughuli za kilimo, uchimbaji mdogo mdogo au hata makazi kwa watu. Lakini baada ya uchimbaji kuanza jamii husika hupoteza kila kitu chao kwa mwekezaji kwasababu mwekezaji huchukua maeneo makubwa sana.
Swali la msingi la kujiuliza ni kwamba je! Jamii hizi hutendewa sawa na inavyotakiwa kwa mjibu wa sheria za kimataifa?
Na je! Kipimo kile kile wanachokitumia makampuni haya kuwafidishia jamii zetu hizi katika ulimwengu wa tatu ndio kinachotumika kuwafidishia wananchi katika mataifa yao wanapofanya shughuli hizi?
Mimi katika maeneo ninayotoka nimeshuhudia unyanyasaji mkubwa sana kwa jamii yetu, kwa mfano wakati utafiti ulipofanyika na kugundulika kuwa kuna kiwango kikubwa cha madini ya Dhahabu wananchi waliahidiwa mambo mengi sana ambayo waliamini kubwa yangeweza kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yetu lakini imekuwa tofauti kabisa. Na tunachoshuhudia ni makampuni kubadilishana umiliki tu.
Kwa mfano: kulikuwa na mto mkubwa tu ambao ulikuwa na uwezo wa kuhifadhi maji mwaka mzima na jamii iliweza kupata kitoweo cha samaki ndani ya mto huu. Lakini baada ya uchimbaji wa madini ya Dhahabu kuanza miaka michache tu mto umejaa michanga pamoja na mawe makubwa hivyo kupelekea vina virefu vya maji kujaa mawe na mchanga kwa hali hii basi maji yakijaa yatoka nje ya mkondo wake na kusomba mazao kwasababu hawezi kutuama tena kama zamani na kuhimili muda wa mwaka mzima
Sasa ninajiuliza hizi wizara husika haziyaoni haya kweli? Maana nachokiona kwa wingi ni askari tu ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya mwekezaji tu, licha ya wananchi kulalamika mara kwa mara kusuhu hali hii ikiwepo kuvunja kwa maji yanayosemekana kuwa na sumu kutoka mgodini lakini maslahi ya wananchi hayapewi kipaumbele cha kutosha kabisa katika hili.
Vipi pale wananchi katika maeneo haya wanaposhuhudia maji hayo yakikausha nyasi na mimea mingineo, na inasemekana pia kuna wakati watu waliwahi kuathirika na maji haya na bado mbaka sasa jamii hii haina maji safi na salama kwa matumizi yao binafsi na wanyama wao pia.
Kitu cha kushangaza ni kamati zinazoundwa kila siku na kuleta majibu ambayo hata mtoto mdogo hawezi kuyapokea maana uhalisia unapotezwa kabisa. Na kitu kibaya zaidi wanachofanya viongozi wetu ni wanapokuja kutatua changamoto hizi wao wanaenda moja kwa moja migodini na wanatumia muda mwingi wakiwa ndani ya mgodi badala ya kuzungumza na jamii inayoathirika na wakija kwa jamii wanatuambia kamati ya uchaguzi itaundwa ili kuchunguza swala hili na hapo inaisha hivyo hivyo.
Mimi naitazama serikali na viongozi wetu kama watu wasiojali maslahi ya wananchi kwa nyaja hii, na sauti ya jamii asilia imemezwa na imegeuka kuwa adui kwa viongozi katika nyadhifa na ndio maana kuna mahusiano ambayo siyo mazuri sana baina ya jamii na mwekezaji katika sekta hii.
HITIMISHO
Ninaiomba mamlakani husika katika nyanja hii kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao kwa jamii husika na kujali na kuthamini maslahi ya jamii asilia kuanzia hatua ya mwanzo katika mikataba hii ili kupunguza migogoro kati ya jamii na wawekezaji. Maana ni kitu kibaya pale wananchi wanaposema kuwa ni bora kufidishiwa na kampuni husika bila viongozi wa serikali kuingilia maana wao huja na ajenda zao za kuwakandamiza Watanzania wenzao ili kuwanyang'anya stahiki zao.
Hivyo naamini imefika wakati serikali kujitathmini umuhimu wake kwa jamii angalau kulinda maslahi ya wananchi wake ambao imeonekana kusahaulika pindi mikataba hii inapotengenezwa, kwasababu inaumiza jamii na kujikuta haina pa kushika kabisa.
Mimi natamani sana kuona sheria ya umiliki wa ardhi Tanzania ikibadilishwa kutoka mfumo wa sasa ambao unainyima jamii asilia haki ya mamlaka katika umiliki na maamuzi ya uendeshaji wa ardhi. Napendekeza tuchague mfumo mwingine ambao sasa jamii itakuwa na maamuzi sahihi na kamili badala ya huu sasa ambao mwamuzi ni kiongozi wa juu.
Na mwisho ninaomba wizara ya madini na wizara ya ardhi kufikiria upya umuhimu wa kubadili sheria hizi zilizopitwa na wakati pamoja na kurejelea katika kutathimini mikataba waliyoingia na makampuni ya uchimbaji wa madini ambayo haikujumuisha maslahi ya jamii husika na kwa kufanya hivyo basi Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi pendwa zaidi na wananchi wake badala ya kuishia kusifiwa kutoka nje huku ndani moto unawaka.
Asanteni sana jamii Forum kwa kuanzisha kipindi hiki kwa sasa tunaweza kufikisha ujumbe kwa wahusika na kwa jamii pia.

Upvote
0