Mkuu FMES,
Katiba ya Zanzibar inamtaka rais wa ZnZ ateue angalau wawakilishi wawili kwenye toka CUF kwenye ZEK na Barazani baada ya majadiliano na uongozi wa CUF.
Baada ya uchaguzi 2005, CUF ikapeleka majina yake 4 kwa Karume ili achague mawili ya barazani. Karume akawaita CUF wajadiliane majina yapi, CUF wakakataa kwa kushikilia msimamo hawamtambua Karume.
Karume nae ni jeuri, kiburi, ukijumlisha na whisky kichwani, akagoma katakata kuteua. Just stalmate. Huku wawakilishi wa CUF wakiiingia barazani kushiriki vikao mpaka kuipongeza serikali ya Zanzibar kuwa ni De-Facto (serikali ya kinyume na sheria) na sio De-jure (Serikali kwa mujibu wa Sheria).
Hili tangazo la leo ndilo la kwanza la CUF kuithibitisha serikali ya Karume kuwa ni De-jure. Hivyo kauli ya jino kwa jino imefutika rasmi pamoja na zile kelele zao zote za kupokwa tonge mdomoni, yaani CUF wamekubali walishindwa na mshindi ni Karume, hivyo uhasama wote kwisha.
Mambo yangu yakiwa mazuri, next week natinga ZnZ, Pemba specifically kupima upepo wa impact ya utambuzi huu, na insha-allah nitawaletea nitakayo yashuhudia.