Naona Nipashe katika website yao wameupdate matokeo -- soma hapa:
Tume ya Uchaguzi (Nec) imetangaza matokeo ya majimbo yote 238 ya urais na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ameibuka na jumla ya kura 4,911,057 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, aliyepata kura 2,028,177.
Nafasi ya tatu katika matokeo hayo ambayo ambayo yamekuwa yanatangazwa tangu Jumatatu wiki hii imekwenda kwa mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye amepata kura 618,406.
Kwa matokeo hayo sasa ni dhahiri Kikwete ametetea kiti chake, lakini idadi ya waliojitokeza kupiga kura ikiwa imeporomoka sana kulingana na idadi ya watu zaidi ya milioni 19 waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura mwaka huu.