Matokeo ya Sensa na Vifo Vinavyozuilika Kwenye Jamii

Matokeo ya Sensa na Vifo Vinavyozuilika Kwenye Jamii

kevylameck

Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
18
Reaction score
19
3E53EAFE-B603-4535-8CFA-A687055E876B.jpeg

Na Kevin Lameck

Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 zilipitisha Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Lengo la tatu la ajenda hiyo lililenga afya bora na ustawi. Tangu wakati huo, WHO imekuwa ikisaidia mipango ya nchi na kufuatilia maendeleo kuelekea lengo hili.

Kufuatia hatua hiyo, Shirika la afya duniani limetoa ripoti yake inayofahamika kama "Tracking Universal Health Coverage in the WHO African Region, 2022"

Umoja wa Mataifa kupitia WHO katika ripoti yake linasema umri wa kuishi barani Afrika tena muhusika akiwa na afya bora umeongezeka.

Umri huo kwa waafrika umeongezeka kwa wastani wa miaka 10 kwa mtu mmoja ikiwa ni ongezeko kubwa kuliko ukanda mwingine wa shirika hilo duniani.

Sababu kubwa iliyotajwa na shirika hilo la kimataifa katika ripoti yake ya jana iliyozinduliwa huko Brazaville ni pamoja na kuimarika kwa huduma ya Mama na Mtoto.

"Kuimarika kwa huduma za msingi za afya,mafanikio katika afya ya uzazi hasa kwa wajawazito,watoto wachanga na afya ya mtoto ni sababu za msingi za Afrika kuibuka kinara", Imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inasema kwa wastani utoaji wa huduma za afya kwa wote imeongezeka kutoka asilimia 24 mwaka 2000 hadi asilimia 46 kufikia mwishoni mwa 2019.

Ripoti hiyo imemaliza kusema ingawa bado tuko nyuma ya wastani wa dunia, bado katika kipindi hicho hicho wastani wa kuishi duniani uliongezeka kwa miaka mitano pekee.

Upatikanaji wa ripoti hii hutokana na mambo mbalimbali ya kitakwimu hasa kuhusu takwimu za watoto wanaozaliwa,wanaofariki dunia baada ya kuzaliwa na ubora na upatikanaji wa huduma za Afya kwa nchi moja moja na bara zima.

Takwimu hizi hupatikana kwenye zoezi la sensa za watu na makazi ambayo ni sharti pia la Umoja wa Mataifa zoezi hilo liwe linafanyika kila baada ya miaka kumi.

Ukisoma madodoso ya Sensa na taarifa mbalimbali za mtakwimu Mkuu wa serikali amezungumzia maswali na Taarifa zitakazokusanywa wakati wa Sensa.

Miongoni mwake ni pamoja na kukusanywa kwa Taarifa za Uzazi na Vifo vilivyotokea ndani ya kaya husika itakayokuwa inahesabiwa.

Takwimu kuhusu idadi ya watoto waliozaliwa haj na ambao bado wanaishi na wale waliofariki zitaonesha hali ya uzazi na vifo hapa nchini

Takwimu za sensa zinasaidia katika kutathmini huduma za afya kwa watoto na kina mama.hii ni muhimu katika kuweka mikakati ya kupambana na vifo vya watoto na vifo vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi kwa akinamama.

Kuboreka kwa huduma za Afya na matibabu sambamba na kupatikana kwa mafanikio mbalimbali ya sekta ya afya kunatokana na Taarifa na Takwimu.

Takwimu na taarifa ndizo zitakazoisaidia Serikali katika kutathimini na kuboresha zaidi huduma za afya na uzazi kwa akina mama na watoto wanaozaliwa.

Inawezekana kwa nchi yetu kufikia wastani wa umri wa kuishi uliowekwa na Umoja wa Mataifa kama Serikali itafahamu vyema Takwimu kuhusu Uzazi na Vifo.

Sensa ya watu na makazi nchini Tanzania ni August 23/2022, Siku ya Jumanne.Tuboreshe na kutimiza Haki msingi ya watoto zetu kuishi na Kinamama kujifungua Salama.

#SensakwaMaendeleo
 
Back
Top Bottom