Msimu uliyopita Simba hakupata ushindi kwenye mechi nane (8) za ugenini dhidi ya; Mbeya city, Mbeya Kwanza, Prisons, Mtibwa, Azam, Kagera, Geita, Biashara na Polisi. Lakini kwa Mkapa alipata matokeo mazuri zaidi kuliko Yanga.
Simba hakushinda mechi mbili tu, dhidi ya Yanga na Coastal. Ikumbukwe Yanga haikupata matokeo mazuri kwenye mechi tatu pale kwa Mkapa, dhidi ya Simba, Prisons na Mbeya city.
Kwa upande mwingine, Yanga alishinda mechi karibu zote za nje ya Mkapa stadium. Alikosa ushindi kwenye mechi mbili tu, dhidi ya Mbeya City na Biashara.
Mwaka huu rekodi zimeanza kujirudia. Yanga wameshacheza mechi tano ugenini na wameshinda zote. Simba wao wamecheza mechi tatu na wameweza kushinda mechi moja tu.
Mwenye kuweza kuchambua kwa kina sababu zinazoweza kuwa nyuma ya mwenendo huu anakaribishwa.