Matokeo ya Simba nje ya Dar

canfi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,368
Reaction score
1,477
Msimu uliyopita Simba hakupata ushindi kwenye mechi nane (8) za ugenini dhidi ya; Mbeya city, Mbeya Kwanza, Prisons, Mtibwa, Azam, Kagera, Geita, Biashara na Polisi. Lakini kwa Mkapa alipata matokeo mazuri zaidi kuliko Yanga.

Simba hakushinda mechi mbili tu, dhidi ya Yanga na Coastal. Ikumbukwe Yanga haikupata matokeo mazuri kwenye mechi tatu pale kwa Mkapa, dhidi ya Simba, Prisons na Mbeya city.

Kwa upande mwingine, Yanga alishinda mechi karibu zote za nje ya Mkapa stadium. Alikosa ushindi kwenye mechi mbili tu, dhidi ya Mbeya City na Biashara.

Mwaka huu rekodi zimeanza kujirudia. Yanga wameshacheza mechi tano ugenini na wameshinda zote. Simba wao wamecheza mechi tatu na wameweza kushinda mechi moja tu.

Mwenye kuweza kuchambua kwa kina sababu zinazoweza kuwa nyuma ya mwenendo huu anakaribishwa.
 
Shida ya Simba naiona katika ukosefu wa wachezaji bora wa kutosha. Ndani ya Simba kuna wachezaji wachache sana wenye quality, ukimtoa Chama, Inonga, Kanoute, Onyango, Kapombe, Tshabalala, Mzamiru Yassini, Sakho, Phiri, wengine wote waliobakia ni avarage players au rubbish tu.

Kibu Denis hatakiwi kwasasa hata akae bechi , Kyombo ni wa hivyo sana. Tunahitaji kusajili wachezaji wataoweza badili mchezo.

Lingine kocha, hamna kitu anabebwa tu na ubora wa baadhi ya wachezaji. Mechi ya leo kipindi cha pili Mbeya city walikuwa wanashambulia kwa kustukiza na kuizidi Simba kiungo. Nilitegemea kocha angeingiza Akpan azuie eti namuingiza Kibu D.
 
Nakurekebisha kidogo yanga kashinda mechi 6 zote alizocheza mpaka sasa na sio mechi 5 kama nilivyokunukuu, kwaiyo mechi 6=18 points
 
Mbona umetaja karibu timu nzima?
 
Nakurekebisha kidogo yanga kashinda mechi 6 zote alizocheza mpaka sasa na sio mechi 5 kama nilivyokunukuu, kwaiyo mechi 6=18 points
Sawa lkn ile ya Ruvu shooting ilichezwa Kwa Mkapa. Zilizochezwa nje ya Dar ni mechibdhidibya Polisi, Coastal, Kagera, Geita na Dodoma jiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…