Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
Tume huru ya uchaguzi ya Afrika kusini (IEC) imetangaza matokeo ya mwisho ya NPE 2024 katika Kituo cha Kitaifa cha Uendeshaji wa Matokeo huko Midrand, Kura kutoka majimbo 19 na mikoa 9 zimekusanywa katika jumla ya vyama 18 vya siasa vilivyo shiriki uchaguzi huu.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa chama tawala cha ANC kimepoteza viti 71 katika Bunge, na chama kikuu cha upinzani DA kimeongeza (kupata) viti vipya 3, huku chama kipya cha MKP kikijinyakulia viti 58.
Idadi ya wapiga kura kwa uchaguzi huu wa mwaka 2024 ni sawa na asilimia 58.61% huku Kura halali zilizopigwa ni 16 025 199 na Kura zilizoharibika ni 212 518.
Tume ya uchaguzi IEC imetangaza kuwa uchaguzi huu mkuu wa saba wa Afrika kusini ulikuwa huru na wa haki.
Pia katika matokeo hayo yameonyesha kuwa chama cha ANC kimepata jumla ya asilimia 40% kitaifa, ikifuatiwa na DA yenye karibu asilimia 22%, huku chama cha MK Party kikipata asilimia 14.59% na chama cha EFF kimepata asilimia 9.5%.
Kwa matokeo hayo chama cha ANC hakitoweza kuuda serikali, hivyo kitaitaji ushirika (mseto) na chama kingine ili kiweze kuunda serikali, tayari chama cha EFF na DA kimeshaweka wazi kuwa wapo tayari kutegeneza mseto na ANC ili kuunda serikali.
Tuendelee kutazama nani atatengeneza mseto na ANC, je ni DA, EFF na MKP? Au ANC ataendelea kutunisha misuli ili uchaguzi urudiwe baada ya serikali ya muungano kushindikana ndani ya siku 40?
Mpaka sasa chama cha ANC kimeshasema kipo tayari kushirikiana hata na chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA), ambacho kimeongoza kwa ukosoaji wa ANC kwa miaka mingi lakini kinatazamwa na wachambuzi wengi kama chaguo thabiti zaidi la muungano na ANC kwa Afrika Kusini kuliko ANC kuungana na EFF na MKP.
Hata hivyo mpaka sasa chama cha DA kimeshasema kua wao hawatafanya muungano na vyama vya EFF na MK, na kuwaita kuwa "muungano na wao ni sawa na siku ya maangamizi" kwa Afrika Kusini.
Ndimi Comred Mbwana Allyamtu-CMCA