Matokeo ya Uchaguzi Mbeya

Wewe nawe na huo uzanzibari wako feki wa JF unaboa kila kitu "mie mzanzibari" sound una legitimate kitu kwa nguvu.

Ushauri wa bure: U can still propagate Chadema yako bila ya kulazimisha "uzanzibari"
 
Wizi mtupu

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, aliyejulikana kwa jina la Fidelian Mkomola anayetuhumiwa kuhifadhi masanduku ya kura katika nyumba ya mjumbe wa nyumba kumi wa CCM, akisindikizwa na polisi kuelelea kituo cha polisi cha Mbalizi Mbeya Vijijini , baada ya kukamatwa na masaduku hayo usiku wa kuamkia jana.
Masanduku shaghalabaghala, mwanafunzi abambwa nalo

Emmanuel Herman na Brandy Nelson, Mbeya

UCHAGUZI mdogo wa Mbeya Vijijini jana asubuhi ulianza kwa vituko baada ya kubainika kuwa baadhi ya masanduku ya kura yalihifadhiwa katika nyumba za watu, huku yakitutuswa kiholela kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku vituo vingine vikichelewa kubadikwa majina ya wapiga kura.

Katika tukio mojawapo mwanafunzi, Severine Gama wa shule ya msingi alikutwa akiwa mebeba sanduku la kupigia kura na alikuwa hana msimamizi wala polisi wakati akipeleka sanduki hilo katika kituo cha kupigia kura cha eneo la Mbalizi katika Kata ya Utengule Usongwe.

Mwanafunzi huyo alikamatwa na viongozi wa CUF, waliokuwa wakifanya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya kupigia kura na kuanza kumhoji .

Alipohojiwa ni wapi alikuwa anapeleka sanduku hilo, kijana huyo alisema yeye alipewa sanduku hilo na msimamizi wa uchaguzi ili alipeleke katika moja ya kituo cha kupigia kura katika eneo la Mbalizi.

Kutokana na majibu ya kijana huyo ambayo yaliyoonyesha kutowaridhisha viongozi wa CUF ndipo walipomchukua na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kwa ajili kuendelea kuhojiwa na sanduku hilo lilirudishwa na kupelekwa katika kituo cha kupigia kura.

Tukio hilo lilitokea wakati vituo vingine vikiwa vimechelewa kubadikwa majina ya wapiga kura.
 
Uchaguzi ulio fanyika Jana tr 25/01/2009 kumchagua mbunge wa Mbeya vijijini umekubikiwa na kasoro kadha huku ikionyeshwa wananchi kususia uchaguzi kwa kile kinacho onekana demokrasia bado haijachukua mkondo wake ndo maana wapiga kura kujitokeza wachache sana ukilinganisha na waliojiandikisha.
Vituo vingi viliandikisha wapiga kura zaidi ya 300 maeneo ya Tunduma road lakini walio jitokeza jana ni idadi ndogo sana ni kituo kimoja tu kilicho kuwa na wapiga kula zaidi ya 100 vingine ni chini ya 100.
Mpaka sasa Mgombea wa CCM ndiye anaye ongeza lakini kwa kura kiduchu sana ukilinganisha na walio jiandikisha.Kuna sakata la Msaidizi wa msimamizi kuwa uchaguzi kuhifadhi masanduku ya kupigia kura kwa mjumbe wa nyumba kumi bila ulinzi wowote ule,kijana mwanafunzi wa shule ya msingi kubeba sanduku la kupigia kura bila ulinzi wowote kupeleka kituoni,wananchi wengine wanadai card zai za kupigia kura zimechukuliwa na serikali za vijiji kama vocha ya mgao wa mbolea za ruzuku.
Kuna matukio kadhaa wa kadha yaliyo jitokeza more update to come.
 
Last edited:

Kuboresha daftari ni pamoja na kuondoa majina ya waliokufa. Ingawa taarifa za waliokufa uenda zisipatikane mapema lakini moja ya sifa za uboreshaji ni pamoja na kuondoa majina ya wasiohitajika kwenye daftari
 
Roughly waliojitokeza kupiga kura ni kama 10% ya waliojiandikisha,na kati ya hao kama90% ya kula CCM wamezivuna.
Kwa hiyo 90% ya waliojiandikisha hawakujitokeza kupiga kura.
Alafu unaambiwa CCM imeshinda,Democrasia iko wapi?
Wizi mtupu
 
hAIDI SAA 11 JIONI MATOKEO YALIKUWA BADO KUTANGAZWA, NDIO KWANZA WALIKUWA KWENYE SANDUKU LA TATU KATI YA MASANDUKU 395 WAKIJUMLISHA KURA.

MATOKEO KUTANGAZWA USIKU
 
Katika low turnout kama hii, kwa nini tume inashindwa kutangaza matokeo mapema, mambo yaishe watu wakaendelee na kilimo!!!!!
 
Chama cha Mapinduzi kimeweza kulitetea Jimbo la Mbeya Vijijini katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana kuziba nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Richard Nyaulawa. Ushindi ambao ulitarajiwa baada ya mgongano kati ya vyama vya upinzani kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuenguliwa kutokana na mgombea wake kutofuata masharti ya viapo kwa anayetaka kuwa mgombea wa Ubunge. Chama cha Wananchi (CUF) kimeelekea kukubali ukweli huo wa ushindi wa CCM licha ya kuwa na malalamiko ya kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi.
Akizungumza na KLHN jana jioni kiongozi wa CUF Bw. Mazee alielezea kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa wazi wa taratibu hizo za uchaguzi ambapo watu kadhaa ambao alidai ni viongozi na mashabiki wa CCM wamefikishwa kwenye kituo cha polisi. Habari hizo pia zilitangazwa katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku jana kuhusu ukiukwaji huo.

Ushindi wa CCM kwenye jimbo la Mbeya Vijijini umefuatia kampeni nzito iliyoongozwa na aliyekuwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. John Samwel Malecela (Mtera) ambaye aliitwa kuongeza nguvu kwenye jimbo hilo. Ushindi huo unaendeleza mwelekeo wa kila chama kilichokuwa na kiti cha ubunge wazi kimeweza kukitetea kiti hicho katika uchaguzi mdogo.

Chaguzi nyingine mbili zinatarajiwa mwaka huu nazo ni Jimbo la Mwibara na Biharamulo ambapo washindi wake walitengeliwa na maamuzi ya mahakama.

Habari rasmi za matokeo ya uchaguzi huo zinatarajiwa kutangazwa muda wa wote kuanzia sasa (saa nne za asubuhi). Hata hivyo haijajulikana kama CUF au chama kingine kitafungua kesi ya kupinga ushindi huo hasa pia ikizingatiwa kuwa idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni kidogo sana kuliko ilivyotarajiwa. Baadhi ya vituo vya uchaguzi ambavyo vilikuwa na watu 450 waliojiandikisha ni watu chini ya 50 tu waliojitokeza kupiga kura.
 
Asha na wana JF wengine,

Si kweli kwamba Kenya haipashwi kuwa mfano wa vyama kuungana labda kama tunasahau haraka. Ili kukiondoa chama tawala madarakani, kina Kibaki na Odinga na vyama vingine vidogo ilibidi viungane vimsimamishe mtu mmoja kugombea urais na ndipo Kibaki aliweza kumshinda mtoto wa Kenyatta aliyekuwa amesimamishwa na KANU kilichokuwa chama tawala.

Huu mkorogano mwingine wa PNU na Orange umekuja baadae lakini na ndivyo vyama vyetu vinapashwa kufanya. Viondoe kwanza CCM madarakani kwa kushirikiana na baadae sasa kila chama kinaweza kikasimama kivyake vyake.

Sikubaliani na wanaosema Muungano wa vyama hauwezi kusaidia kuiondoa CCM madarakani. Na hapa Muungano tunaousema si wa kuvunja vyama vingine na kuunda kingine kipya, la ni pale vyama kukaa vikakubaliana kati yao nani agombee urais na mtu yupi kutoka chama kipi asimame kwenye uchaguzi wa Ubunge kwa kila jimbo. Kwa mtindo huu inawezekana kukawa na mafanikio lakini vinginevyo ni ndoto za alinacha kuiondoa CCM madarakani kwa mtindo huu wa sasa.

Naomba kuwasilisha.
 
hAIDI SAA 11 JIONI MATOKEO YALIKUWA BADO KUTANGAZWA, NDIO KWANZA WALIKUWA KWENYE SANDUKU LA TATU KATI YA MASANDUKU 395 WAKIJUMLISHA KURA.

MATOKEO KUTANGAZWA USIKU

Kujumlisha masanduku yalishamaliza toka jana usiku. Leo wanajumlisha matokeo tu ya kila kituo kwa kata. Kazi hii imechelewa kwa kuwa kuna kata wanasema zilikuwa za mbali sana. Ila kwa taarifa za matokeo ya kutoka kwenye kata ni kuwa CCM imeshashinda kwa hao wapiga kura wachache waliopiga hivyo kinachosubiriwa ni kutangazwa rasmi tu.

.........ndiyohiyo
 
hAIDI SAA 11 JIONI MATOKEO YALIKUWA BADO KUTANGAZWA, NDIO KWANZA WALIKUWA KWENYE SANDUKU LA TATU KATI YA MASANDUKU 395 WAKIJUMLISHA KURA.

MATOKEO KUTANGAZWA USIKU

Jumla ya kura zilizopigwa ni takribani elfu 30 tu, kati ya watu laki 1 na elfu 20 ambao walijiandikisha kupiga. Waliopiga kura ni close tu 25%. Tusubiri matangazo rasmi

.....ndiyohiyo
 
Wewe nawe na huo uzanzibari wako feki wa JF unaboa kila kitu "mie mzanzibari" sound una legitimate kitu kwa nguvu.

Ushauri wa bure: U can still propagate Chadema yako bila ya kulazimisha "uzanzibari"

Yani mie kutangaza kugombea kupitia Zanzibar ishakuwa shari. Naipenda Zanzibar kama ninavyoipenda Tanzania. Umeruka hoja zangu zote humu umeanza kuzusha vioja. Kama wataka mipasho karibu jamvini kwangu bonyeza hapa kwenye Urojo wa Pweza hapa niyaache ya kanda2.

Asha
 
Haya mambo ya kuungana hayana mpango kuna mmoja wetu amesema Pemba wameiangusha CCM bila ya kuungana na Chama chochote,hivyo inaonekana kuna mwanya baina ya wananchi na uelewa bado hawajaguswa na ukali wa maisha hasa wa huko mikoani na vijijini maana muhogo ,mahindi yapo na vyakula vingine vya kuokotea okotea kama maembe na matunda mengine ,umeme haumshugulishi maana hata ukiwepo hawezi kuulipia na maji wanatumia ya mito na wengine visima matibabu waganga wa kienyeji na miti shamba kibao ,hata hajui maendeleo ni kitu gani hivyo ipo kazi kubwa sana hata wananchi waamke.
 
CCM yarejesha kiti Mbeya Vijijini
Faraja Mgwabati na Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Monday,January 26, 2009 @21:15

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini kwa kupata asilimia zaidi ya 70 ya kura zilizopigwa na kuvishinda vyama vya CUF na SAU katika uchaguzi uliofanyika juzi.

Hadi tunakwenda mitamboni jana saa mbili usiku, maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wawakilishi wa vyama walikuwa wanaendelea kuhakiki kura zilizopigwa, lakini taarifa za awali zinadai kuwa mgombea wa CCM, Mchungaji Luckson Mwanjale ameibuka mshindi kwa kupata asilimia 73.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame alikaririwa jana jioni akisema kwamba walikuwa wakiendelea na kujumuisha matokeo hayo baada ya kupatikana kutoka katika kata mbalimbali za jimbo hilo lenye kata 17.

“Unajua siyo kuwa kura zikija zinajumuishwa tu…kuna taratibu mbalimbali zikiwamo za kujua ni watu wangapi walipiga kura katika vituo husika na kisha kujumuisha kura hizo. Tunategemea matokeo yatatangazwa leo (jana),” alisema Jaji Makame alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana majira ya saa moja usiku.

Katika uchaguzi huo uliokuwa na idadi ndogo ya wapiga kura, mgombea wa CUF Daud Mponzi imeelezwa kuwa ameibuka na asilimia 26 ya kura zilizopigwa huku mgombea mwanamama kutoka SAU, Subi Mwakapiki akiambulia asilimia moja. Hata hivyo, chama cha CUF kimetishia kukata rufaa kupinga matokeo hayo kwa kile walichodai kuwa na kasoro nyingi katika uchaguzi huo ambazo zimesababisha mgombea wao kushindwa.

Mratibu wa Kampeni za Chama hicho, Mazee Rajabu Mazee, alisema wamekusudia kukata rufaa baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi na kwamba watahakikisha haki inapatikana, ingawa hakutaja kasoro hizo zilizojitokeza. Taarifa zinasema kati ya watu 127,000 waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo ni watu zaidi ya 35,000 sawa na asilimia 27.6 tu ndio waliojitokeza kupiga kura huku watu 92,000 sawa na asilimia 72.4 wakishindwa kujitokeza.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na ‘HabariLeo’ walidai kutojitokeza kwa watu kupiga kura kunatokana na kuenguliwa kwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, wakiamini kuwa bila ya kuwapo kwa chama hicho, CCM itashinda. “Unajua wananchi wengi waliamini kuwa upinzani utakuwa kati ya CCM na Chadema, lakini baada ya Chadema kuenguliwa wengi waliamini CCM itashinda na kuamua kutopiga kura,” alisema mfanyabiashara wa Mbalizi, John Ndele.

Naye Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe, Jacob Mwakasole aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kampeni za kumnadi mgombea wa CCM, alisema kutokujitokeza kwa wananchi kunatokana na ukosefu wa elimu ya uraia kwa wananchi wengi wa jimbo. Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini umefanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wake Richard Nyaulawa aliyefariki Novemba 9, mwaka jana kwa saratani ya utumbo na kuzikwa Novemba 13, kijijini kwake Inyala.
 
Tiba,
Ukiangalia kwa undani sana kilichounganishwa kwa wenzetu KENYA ni MAKABILA sio vyama. Siasa za wenzetu zinaegemea zaidi kwenye UKABILA.
 
HATA WAungane MAra MIA moja hawawezi kuishinda TUME ya Uchaguzi, hapa hawapambani na CCM bali wanapambana na NEC.
 
Mbeya by-election: Low turnout explained

2009-01-27 10:40:21
By Guardian Team

A number of opposition party leaders have linked the low turnout in Sunday`s Mbeya Rural by-election partly to the demand that farmers present voters` identity cards to get fertiliser vouchers.

However, Political Parties registrar John Tendwa quickly suggested that some activities by a section of the opposition had also ``undermined`` the by-election.

Civic United Front (CUF) Chairman Ibrahim Lipumba claimed in a telephone interview with The Guardian yesterday that a big number of would-be voters reported having had their IDs taken away by village and ward executive officers as a condition for being given the vouchers.

``We have evidence and there is one such case at a police station and I must state in no uncertain terms that this is a blatant infringement of democracy. These people had been denied their constitutional right to vote,`` said the professor.

His Tanzania Labour Party counterpart, Augustine Mrema, meanwhile called on the government to form a commission to investigate why more than a half of the people registered as prospective voters did not turn up on polling day.

He said there was no need for the country to have a multiparty political system ``if democracy is repeatedly flouted with impunity``.

``This is so totally ridiculous because voters' IDs are the voters' property and there is no way a village executive officer or a cell leader could take it away and deny the people concerned their right to vote just like that,`` noted a visibly dejected Mrema.

The outspoken politician claimed that National Election Commission (NEC) officials were fully aware of the problem and ``had promised to work on it before polling day but cleverly defaulted``.

Prof Mwesiga Baregu of the University of Dar es Salaam said the decision by the electoral commission to disqualify one of the aspirants was wrong and made voters lose confidence in the whole process.

``The reason given for the disqualification of the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aspirant was very flimsy, at best,`` he pointed.

He added: ``I suspect NEC denied the voters an aspirant who they had probably prepared to vote for, so automatically these people lost confidence in the by-election and decided not to show up on polling day.``

Speaking from Mbeya, Tendwa admitted that it was quite possible that the Chadema aspirant`s disqualification adversely affected the turnout.

However, he added that Chadema`s own mobilisation campaign code-named Operation Sangara had undermined the by-election ``precisely in that its thrust was on sensitising people not to vote after its own aspirant was disqualified``.

``When we got here many Mbeya residents could be heard openly saying some Chadema officials had told them not to vote. The NEC intervened by saying it was completely against this but it is evident that the harm had already been done, and hence the low turnout,`` he explained.

Abere Amon, a resident of Chapakazi at Mbalizi in Mbeya, said Chadema aspirant Sambwee Shitambala`s disqualification left many people ``utterly disappointed``.

Contacted for comment, returning officer Juliana Malange admitted that the turnout was ``astonishingly low`` but noted that she did not know why it was so.
``It is true that very few people came to vote but I cannot explain why. I will have to investigate,`` she said.

Meanwhile, CUF has rejected results of the by-election announced yesterday and showing ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) candidate Luckson Mwanjale as the winner. Officials said they expected the final results to be ready by 9pm.

The opposition party claimed that the by-election was marred by irregularities, one being the missing of some names at a number of polling stations.

Prof Lipumba told reporters that they were still communicating with lawyers ``to see the measures to take to ensure justice is done``.

He claimed that the electoral commission had not supervised the by-election well enough ``to help wananchi elect a leader that is truly of their choice``.

He added that they were convinced that the by-election was, on the whole, neither free nor fair and they would not accept the results and concede defeat.

NEC Chairman Judge Lewis Makame explained that there were ``some problems`` in the permanent voters` register but the shortcomings would be rectified in June this year.

The holding of the by-election followed the death of former legislator Richard Nyaulawa last November.

More that 120,000 people registered to cast their ballots at 395 polling stations, at most of which less than half of the prospective voters actually voted.

The candidates were Rev Mwanjale, Subi Mwakipiki from Sauti ya Umma and David Mponzi from CUF.

SOURCE: Guardian
 
Mbeya by-election: Low turnout explained

2009-01-27 10:40:21
By Guardian Team

A number of opposition party leaders have linked the low turnout in Sunday`s Mbeya Rural by-election partly to the demand that farmers present voters` identity cards to get fertiliser vouchers.

However, Political Parties registrar John Tendwa quickly suggested that some activities by a section of the opposition had also ``undermined`` the by-election.

Civic United Front (CUF) Chairman Ibrahim Lipumba claimed in a telephone interview with The Guardian yesterday that a big number of would-be voters reported having had their IDs taken away by village and ward executive officers as a condition for being given the vouchers.

``We have evidence and there is one such case at a police station and I must state in no uncertain terms that this is a blatant infringement of democracy. These people had been denied their constitutional right to vote,`` said the professor.

His Tanzania Labour Party counterpart, Augustine Mrema, meanwhile called on the government to form a commission to investigate why more than a half of the people registered as prospective voters did not turn up on polling day.

He said there was no need for the country to have a multiparty political system ``if democracy is repeatedly flouted with impunity``.

``This is so totally ridiculous because voters’ IDs are the voters’ property and there is no way a village executive officer or a cell leader could take it away and deny the people concerned their right to vote just like that,`` noted a visibly dejected Mrema.

The outspoken politician claimed that National Election Commission (NEC) officials were fully aware of the problem and ``had promised to work on it before polling day but cleverly defaulted``.

Prof Mwesiga Baregu of the University of Dar es Salaam said the decision by the electoral commission to disqualify one of the aspirants was wrong and made voters lose confidence in the whole process.

``The reason given for the disqualification of the opposition Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aspirant was very flimsy, at best,`` he pointed.

He added: ``I suspect NEC denied the voters an aspirant who they had probably prepared to vote for, so automatically these people lost confidence in the by-election and decided not to show up on polling day.``

Speaking from Mbeya, Tendwa admitted that it was quite possible that the Chadema aspirant`s disqualification adversely affected the turnout.

However, he added that Chadema`s own mobilisation campaign code-named Operation Sangara had undermined the by-election ``precisely in that its thrust was on sensitising people not to vote after its own aspirant was disqualified``.

``When we got here many Mbeya residents could be heard openly saying some Chadema officials had told them not to vote. The NEC intervened by saying it was completely against this but it is evident that the harm had already been done, and hence the low turnout,`` he explained.

Abere Amon, a resident of Chapakazi at Mbalizi in Mbeya, said Chadema aspirant Sambwee Shitambala`s disqualification left many people ``utterly disappointed``.

Contacted for comment, returning officer Juliana Malange admitted that the turnout was ``astonishingly low`` but noted that she did not know why it was so.
``It is true that very few people came to vote but I cannot explain why. I will have to investigate,`` she said.

Meanwhile, CUF has rejected results of the by-election announced yesterday and showing ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) candidate Luckson Mwanjale as the winner. Officials said they expected the final results to be ready by 9pm.

The opposition party claimed that the by-election was marred by irregularities, one being the missing of some names at a number of polling stations.

Prof Lipumba told reporters that they were still communicating with lawyers ``to see the measures to take to ensure justice is done``.

He claimed that the electoral commission had not supervised the by-election well enough ``to help wananchi elect a leader that is truly of their choice``.

He added that they were convinced that the by-election was, on the whole, neither free nor fair and they would not accept the results and concede defeat.

NEC Chairman Judge Lewis Makame explained that there were ``some problems`` in the permanent voters` register but the shortcomings would be rectified in June this year.

The holding of the by-election followed the death of former legislator Richard Nyaulawa last November.

More that 120,000 people registered to cast their ballots at 395 polling stations, at most of which less than half of the prospective voters actually voted.

The candidates were Rev Mwanjale, Subi Mwakipiki from Sauti ya Umma and David Mponzi from CUF.

SOURCE: Guardian
 
Matokeo rasmi ya Uchaguzi Mdogo Jimbo la Mbeya Vijijini yametangazwa leo saa 2.30 asubuhi.

Idadi ya wapigakura, Jimbo la Mbeya Vijijini ni 127,780.
Wliopiga kura katika uchaguzi mdogo wa Januari 25, 2009 ni 44,855 ikiwa ni sawa na 35pc ya wapigakura wote jimboni humo.

Mch. Lackson Mwanjali wa CCM alipata kura 32,867 sawa na asilimia 73.27; Daud Mponzi wa CUF kura 10,578 swa na asilimia 23.57; Subi Mwakapiki wa SAU kura 496 sawa na asilimia 1.10; kura 914 sawa na asilimia 2.04 ziliharibika.

Kwa hesabu hizo ina maana kwamba wapiga kura 82,925 hawakujitokeza kupiga kura.

Mgombea wa SAU ameyakataa matokeo na hajasaini fomu. SAU inatarajia kwenda mahakamani kupinga matokeo, sababu ni kuwepo kwa kasoro nyingi na mgombea wao kutukanwa na diwani mmoja wa CCM wakati diwani huyo akihutubia mkutano wakampeni.

Mgombea wa CUF amayakubali makubali matokeo na kusaini fomu lakini inaonekana anawahohia viongozi wake hivyo kutokuwa tayari msimamo wake kuandikwa kwenye vyombo vya jabari.

Wakati anahojiwa na waandishi wa habari jana, Mgombea huyo- Mponzi alisema yeye haoni sababu ya kuendelea na malumbano hadi mahakamani kupinga matokeo, alikubali kushindwa lakini alipoulizwa iwapo maelezo hayo ni msimamo wake rasmi aliruka na kusema anasubiri viongozi wake watoe msimamo.

Hata hivyo CUF wameeleza wazi kutoyakubali matokeo hayo katika mkutano wa Prof Lipumba na waandishi wa habari katika mji wa Mbalizi.

Pamoja na kushinda, CCM wametoka na somo kwamba mambo sasa yamewageuka, kwamba wananchi hawawataki, kwani walikuwa wakielezwa wazi kwamba wanamtaka Sambwee Shitambala. Ugumu wa jimbo hilo hivi sasa kwa CCM ulielezwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho. Mzee Malecela alilazimika kuweka kambi Ilembo baada ya kubaini kuwa ni pagumu na kweli ni kata ya Ilembo na Utengule Usongwe zilizoongoza kwa kuwa na wapigakura wachache.

Kwa mfano, Utengule Usongwe ulimo mji wa Mbalizi, wapo wapigakura 25,354 lakini waliojitokeza ni 4117 tu!

hao ndio wapigakura wa Mbeya Vijijini, hawana kelele lakini wameonyesha msimamo wao
 
Vama vingine vya upinzani ni aibu sana!

SAU unapata kura 500 kati ya 44,000 (yaani 1%) halafu eti unataka kwenda mahakamani kupinga matokeo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…