Wizi mtupu
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, aliyejulikana kwa jina la Fidelian Mkomola anayetuhumiwa kuhifadhi masanduku ya kura katika nyumba ya mjumbe wa nyumba kumi wa CCM, akisindikizwa na polisi kuelelea kituo cha polisi cha Mbalizi Mbeya Vijijini , baada ya kukamatwa na masaduku hayo usiku wa kuamkia jana.
Masanduku shaghalabaghala, mwanafunzi abambwa nalo
Emmanuel Herman na Brandy Nelson, Mbeya
UCHAGUZI mdogo wa Mbeya Vijijini jana asubuhi ulianza kwa vituko baada ya kubainika kuwa baadhi ya masanduku ya kura yalihifadhiwa katika nyumba za watu, huku yakitutuswa kiholela kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku vituo vingine vikichelewa kubadikwa majina ya wapiga kura.
Katika tukio mojawapo mwanafunzi, Severine Gama wa shule ya msingi alikutwa akiwa mebeba sanduku la kupigia kura na alikuwa hana msimamizi wala polisi wakati akipeleka sanduki hilo katika kituo cha kupigia kura cha eneo la Mbalizi katika Kata ya Utengule Usongwe.
Mwanafunzi huyo alikamatwa na viongozi wa CUF, waliokuwa wakifanya ukaguzi katika vituo mbalimbali vya kupigia kura na kuanza kumhoji .
Alipohojiwa ni wapi alikuwa anapeleka sanduku hilo, kijana huyo alisema yeye alipewa sanduku hilo na msimamizi wa uchaguzi ili alipeleke katika moja ya kituo cha kupigia kura katika eneo la Mbalizi.
Kutokana na majibu ya kijana huyo ambayo yaliyoonyesha kutowaridhisha viongozi wa CUF ndipo walipomchukua na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kwa ajili kuendelea kuhojiwa na sanduku hilo lilirudishwa na kupelekwa katika kituo cha kupigia kura.
Tukio hilo lilitokea wakati vituo vingine vikiwa vimechelewa kubadikwa majina ya wapiga kura.