William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Inaonekana Kasheshe & Field Marshall mnawachukia sana CUF?
Naomba nifanye nukuu kutoka gazeti la NIPASHE, kichwa cha habari na sehemu ndogo ya maelezo.
Wananchi wasusa uchaguzi Mbeya
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini umeweka historia mpya nchini kufuatia wananchi 82,927 ambao ni sawa na asilimia 65 ya watu 127,780 waliojiandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kukataa kushiriki kupiga kura kutokana na sababu kadhaa, zikiwemo kwamba hakukuwa na mgombea wa chaguo lao.
Kutokana na msimamo huo, wananchi 44,855 ambao ni sawa na asilimia 35 ndio waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo ambao ulitawaliwa na kasoro kibao na hivyo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luckison Mwanjali, kuibuka mshindi kwa kupata kura 32,867 ambazo ni asilimia 73 ...
Basi ndugu zangu, kama hali yenyewe ndiyo hiyo,je, Mbunge huyu ni halali?
Licha ya kuwa maelezo mengine toka kwa Bosi wa NEC, anasema, katika orodha ya wapigakura yalikuwemo hata majina ya ndugu waliotutangulia mbele ya haki (marehemu), mimi hili haliniingii kichwani. Sijaridhika kabisa na idadi hiyo; Nionavyo mimi ni kweli kabisa kuwa wananchi wamesusia uchaguzi huo.
Nimeamua kuliweka hadharani tulijadili.
Kwasababu Dataz ni tamu ukiwa na flexibility ya denominator; Mimi naona jamaa kashinda kwa kupata asilimia 25.7 ya watu waliokuwa na uwezo wa kupiga kura. [32,867/127,780]*100%
KWELI PIGA UA GARAGAZA UONGOZI ULIKUA LAZIMA UPATIKANE
- JF bwana sometimes tunakuwa kama ze comedy, kwani sheria ya uchaguzi inasema nini kuhusu idadi ya wapiga kura?
-Kama wananchi hawaelewi umuhimu wa kupiga kura linaweza vipi kuwa tatizo la aliyeshinda? Unaposusia uchaguzi unayemuumiza ni nani hasa? Haya ni ya ajabu sana!
Kwa maana nyingine kakataliwa hata kwao. Huyu sio chaguo la wananchi, na ni wazi wananchi walisusisa, hawakutaka kubeba sime kama Tarime bali walitaka kuonyesha mgomo wa kistaarabu wa kuwakata wanafiki wa CCM na CUF.
Nimebahatika kumuona na kumsikiliza mgombea wa chadema aliyenguliwa, hakuwepo wa kupambana naye pale, ni kijana msomi, ana mvuto na uwezo mkubwa wa kushawishi. Lakini mbali ya hayo alishawaonyesha kwamba yeye ni mtoto wao aliyerudi nyumbani kuwatumikia kwani aliwatetea wananchi wa kijiji kimoja cha Isuto huko huko Mbeya Vijijini na kuigaragaraza serikali ambayo ilifikia hatua ya kuweka ndani diwani wao.
Duh... Hii Kali; sina hakika kuna mtu amezungumzia athari za kisheria kwa mshindi au mpiga kura. Kilichoonyeshwa hapo ni changamoto ya turn up ya wapiga kura.
Tupende tusipende... hicho ni kipima joto kwetu. People decided not to waste their time for whatever reasons na imeathiri uchaguzi kwa ujumla;
Wakuu zangu tusijenge sababu zetu wenyewe kujaribu kupotosha Umma..Hatuwezi kabisa kusema wananchi wamegoma kupiga kura ktk uchaguzi mdogo Mbeya vijijini kwa sababu ya mgombea wa Chadema.. Yawezekana kabisa vita kati ya vyama hivi (Upinzani) ndiyo sababu kubwa ya watu kutopiga kura ama sababu kubwa inayojulikana duniani kuwa siku zote Uchaguzi ndogo hutokea asilimia ndogo wa wananchi walioandikisha ktk daftari la wapiga kura..
Hapa canada majuzi tu kulitokea uchaguzi mdogo na asilimi chini ya 60 walijitokeza kupiga kura. Ni hesabu ndogo ktk historia ya nchi hii kltk chaguzi zote sasa sielewi kulikuwepo na mgombea gani ambaye walimtaka hakutokea..Tazma hesabu ya chaguzi zote ndogo utaona kuwa hesabu ya wapiga kura sio sawa na ile ya uchaguzi mkuu..
Chadema wamechemsha Mbeya hilo ni wazi na mimi naamini kabisa tumefanya kmakosa makubwa sana kuanzisha vita ambavyo nina hakika hatuwezi kushinda!..
-
- Katika historia ya by-election yoyote duniani haijawahi kutokea turn-out ya zaidi ya 40%, infact UK huwa haizidi hata 20% kwa hiyo huku Mbeya hakuna cha ajabu