Naomba nifanye nukuu kutoka gazeti la NIPASHE, kichwa cha habari na sehemu ndogo ya maelezo.
Wananchi wasusa uchaguzi Mbeya
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini umeweka historia mpya nchini kufuatia wananchi 82,927 ambao ni sawa na asilimia 65 ya watu 127,780 waliojiandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kukataa kushiriki kupiga kura kutokana na sababu kadhaa, zikiwemo kwamba hakukuwa na mgombea wa chaguo lao.
Kutokana na msimamo huo, wananchi 44,855 ambao ni sawa na asilimia 35 ndio waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo ambao ulitawaliwa na kasoro kibao na hivyo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luckison Mwanjali, kuibuka mshindi kwa kupata kura 32,867 ambazo ni asilimia 73
...
Basi ndugu zangu, kama hali yenyewe ndiyo hiyo,je, Mbunge huyu ni halali?
Licha ya kuwa maelezo mengine toka kwa Bosi wa NEC, anasema, katika orodha ya wapigakura yalikuwemo hata majina ya ndugu waliotutangulia mbele ya haki (marehemu), mimi hili haliniingii kichwani. Sijaridhika kabisa na idadi hiyo; Nionavyo mimi ni kweli kabisa kuwa wananchi wamesusia uchaguzi huo.
Nimeamua kuliweka hadharani tulijadili.