Matola abwaga manyanga Simba

Matola abwaga manyanga Simba

cnjona

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
1,027
Reaction score
239
HALI si shwari ndani ya timu ya soka ya Simba, baada ya jana Kocha Msaidizi Suleiman Matola kujiuzulu wadhifa huo. Matola, kiungo mahiri na nahodha wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania `Taifa Stars', alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuwa na maelewano na Kocha Mkuu wake raia wa Uingereza, Dylan Kerr.

"Mambo si mazuri kwa muda mrefu sasa mpaka nimefikia hatua ya kukaa pembeni," alisema Matola aliyestaafu kuichezea klabu hiyo mwaka 2008, baada ya kuwa alijiunga nayo mwaka 2000 akitokea Kagera Sugar.

"Kocha hana ushirikiano na mimi kama msaidizi wake mambo mengi amekuwa akiyafanya mwenyewe hali inayonifanya nijione sina kazi ya kufanya Simba kwani hata ushauri wangu hautaki.

"Kuna wakati nami nakuwa sina tofauti na wachezaji kwamba sijui orodha ya timu inayocheza mpaka atakapotangaza yeye, huo si utendaji mzuri wa kazi, ili mfanikiwe ni lazima mshirikiane kama timu, sasa kama kocha mkuu na msaidizi wake hawana maelewano maana yake timu inaweza isifanye vizuri, kwa manufaa ya Simba nimeona nikae kando nimuachie timu," alisema.

Matola aliyewahi kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya SuperSport United ya Pretoria, Afrika Kusini, akizungumza kwa hisia kali alisema anakerwa zaidi kugombezwa na kocha huyo, wakati mwingine mbele ya wachezaji.

Alisema kutokana na hali hiyo, ameamua kujiondoa kwenye timu kwani haamini kwa kuendelea kubaki katika hali kama hiyo kutaisaidia klabu na kuongeza kuwa, tayari ameshawasilisha taarifa za kujiuzulu kwa uongozi utakaoamua hatima yake.

Msemaji wa Simba, Haji Manara alipozungumzia hilo alikiri uongozi kupata barua ya Matola kuachia ngazi na kwamba kikao cha kamati ya utendaji kilitarajiwa kukutana muda wowote kuanzia jana kutoa maamuzi.

"Ni kweli kocha wetu msaidizi Matola amekabidhi barua ya kujiuzulu jana (juzi) na amesema sababu ya kufanya hivyo ni kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mkuu…kamati yetu ya utendaji itakutana muda wowote kuanzia sasa kulijadili na kutoa ufafanuzi zaidi ya hilo," alisema Manara. Matola amejiuzulu huku Simba ikiwa kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 21.

Chanzo: HabariLeo
 
Simba kuna tatizo kubwa. Nadhani kuna viongozi wanayaleta hayo. Wanaingilia sana timu. Na wazungu ndio kitu hawakipendi kuingiliwa katika majukumu yao.
Bora Simba iuzwe tu tujue moja. Ugggghgh
 
Alianza kocha bora kabisa wa viungo kuwahi kutokea ulaya Momclovic akabwaga manyanga.. Sasa Mchezaji bora kuwahi kushudiwa tangu miaka 2000 nae kaona isiwe tabu kajiweka pembeni.. Na haya yote yanatokea chini ya miezi 3.
Naomba nihifadhi comment yangu katika hili.
 
Mkuu kuna jambo ndani ya timu. Na ninavyojua Simba ilivyo tutapoteana muda si mrefu. Viongozi wanayatengeneza haya matatizo. Kwanini wamuingilie majukumu yake eti fulani asicheze wakati kocha ndio.anajua uwezo wa kila mmoja na nani atamsaidia kupata matokeo. Sitaki kuamini kocha ni tatizo.
Ushahidi ni baadhi ya viongozi kusema Kerr ataondoka tu, kwa kauli hizo unategemea nini? Kila msimi.tutakuwa na makocha wawili hadi watatu mpaka lini? Kila siku tutakuwa tunaandaa timu kwa kuleta kocha mpya mpaka lini? Sikuona sababu ya kumuondoa Kopunovic wakati ule.
Timu iuzwe tu haya kina Kaburu n Hanspope wanatuzingua tu
 
Kopunoviv aliondoka kwa sababu alitaka kulipwa hela nyingi tofauti na uwezo wa timu.

Mkuu timu tumuuzie nani?... Mpaka sasa sijaona mwenye "dhamira" ya kweli.
 
Kopunoviv aliondoka kwa sababu alitaka kulipwa hela nyingi tofauti na uwezo wa timu.

Mkuu timu tumuuzie nani?... Mpaka sasa sijaona mwenye "dhamira" ya kweli.

Hizo propaganda tu za viongozi. Kopunovic alikubali kukaa na viongozi kupunguza kiwango cha pesa. Viongozi kwa kuwa wao wanajiona watoto wa mjini wakampiga chini. Hivi ni kweli Simba inashindwa kumlipa kocha 40,000 au 30,000 na mshahara wa 7,000?? Haya sasa zengwe lishatengenezwa kocha aonekane hafai watuletee kocha mpya. Badala ya kujiweka pamoja kuimarisha timu tunaanza upya tena.
 
unamshauri mzungu wachezaji wakalale makaburini siku moja kabla ya mechi unadhani atakuelewa?
 
Hii timu huwezi kukosa mtu wa kumuuzia sababu anajua pesa yake itarudi tu. Mo kaonyesha interest wache aweke pesa yake. Atajua pesa nyingine itatoka wapi kuijenga timu ndani n nje ya uwanja. Tumenunua jezi kibao Simba day siku ile n uwanja ukajaa. Viongozi wamegawana pesa wameshindwa kusajili striker wametuletea yule -----. Hivi tunakosa 50-70m ya kupata striker wa maana.
Tuache ujinga muda mwingine viongozi wanazingua. Ingekuwa yanga kungekuwa kushawaka kitambo.
 
Ni bora simba iuzwe tu mana watu walioko simba wanaona kama wamezaliwa ukoo mmoja na timu na kila mtu anataka kutoa maamuz atuwez kufika kokote kwa namna hii mpk inafikia kukumbuka simba ya m/kiti hasan dalali kuliko hivi sasa...

yan klabu kama azam inatuzid kwa kila idara kama leo nmepta k/koo sokon naona duka limeandikwa azam sc shop na ndani ni vifaa vya michezo vya azam tu roho ikaniuma sana klabu kama ya simba yenye washabiki wasioesabika lkn akuna kitu kama icho ambacho kingekua kinaingizia pesa klabu
 
Kama timu uongozi umeahindwa basi wampe Mo Dewji tu tujue moja!
 
Tatizo la timu za bongo hasa Simba na Yanga ni 'wazee wa club'.

Watu wa kuleta utaalamu hawawezi kukaa mezs moja na wanywa kahawa.

Ndio maana club ina miaka 75 lakini haina uwanja.
 
Moise Katumbi wa TP Mazembe hajafika bei kwaani maana mikia imezoea figisu kila uchao mi naifananisha na Ukawa aka fungu la kukosa.
 
Mkuu kuna jambo ndani ya timu. Na ninavyojua Simba ilivyo tutapoteana muda si mrefu. Viongozi wanayatengeneza haya matatizo. Kwanini wamuingilie majukumu yake eti fulani asicheze wakati kocha ndio.anajua uwezo wa kila mmoja na nani atamsaidia kupata matokeo. Sitaki kuamini kocha ni tatizo.
Ushahidi ni baadhi ya viongozi kusema Kerr ataondoka tu, kwa kauli hizo unategemea nini? Kila msimi.tutakuwa na makocha wawili hadi watatu mpaka lini? Kila siku tutakuwa tunaandaa timu kwa kuleta kocha mpya mpaka lini? Sikuona sababu ya kumuondoa Kopunovic wakati ule.
Timu iuzwe tu haya kina Kaburu n Hanspope wanatuzingua tu

lakini Matola hajatofautiana na viongozi ila katofautiana na kocha mkuu.
 
Matola ung'eng'e unamshinda mzungu anashindwa kumwelewa
 
lakini Matola hajatofautiana na viongozi ila katofautiana na kocha mkuu.

Mimi nazungumzia timu in general. Hii ya matola ni matokeo tu. Kuna watu pale hawamtaki matola wengine hawamtaki Kerr. Lakini chanzo ni nini?
 
Kweli simba iuzwe mashabiki na wanachama tutabaki watazamaji maana hawa viongozi wababaishaji tu.
 
Ni aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya simba suleiman matola amejiuzulu nafasi hio leo mchana
 
Back
Top Bottom