cnjona
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 1,027
- 239
HALI si shwari ndani ya timu ya soka ya Simba, baada ya jana Kocha Msaidizi Suleiman Matola kujiuzulu wadhifa huo. Matola, kiungo mahiri na nahodha wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania `Taifa Stars', alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuwa na maelewano na Kocha Mkuu wake raia wa Uingereza, Dylan Kerr.
"Mambo si mazuri kwa muda mrefu sasa mpaka nimefikia hatua ya kukaa pembeni," alisema Matola aliyestaafu kuichezea klabu hiyo mwaka 2008, baada ya kuwa alijiunga nayo mwaka 2000 akitokea Kagera Sugar.
"Kocha hana ushirikiano na mimi kama msaidizi wake mambo mengi amekuwa akiyafanya mwenyewe hali inayonifanya nijione sina kazi ya kufanya Simba kwani hata ushauri wangu hautaki.
"Kuna wakati nami nakuwa sina tofauti na wachezaji kwamba sijui orodha ya timu inayocheza mpaka atakapotangaza yeye, huo si utendaji mzuri wa kazi, ili mfanikiwe ni lazima mshirikiane kama timu, sasa kama kocha mkuu na msaidizi wake hawana maelewano maana yake timu inaweza isifanye vizuri, kwa manufaa ya Simba nimeona nikae kando nimuachie timu," alisema.
Matola aliyewahi kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya SuperSport United ya Pretoria, Afrika Kusini, akizungumza kwa hisia kali alisema anakerwa zaidi kugombezwa na kocha huyo, wakati mwingine mbele ya wachezaji.
Alisema kutokana na hali hiyo, ameamua kujiondoa kwenye timu kwani haamini kwa kuendelea kubaki katika hali kama hiyo kutaisaidia klabu na kuongeza kuwa, tayari ameshawasilisha taarifa za kujiuzulu kwa uongozi utakaoamua hatima yake.
Msemaji wa Simba, Haji Manara alipozungumzia hilo alikiri uongozi kupata barua ya Matola kuachia ngazi na kwamba kikao cha kamati ya utendaji kilitarajiwa kukutana muda wowote kuanzia jana kutoa maamuzi.
"Ni kweli kocha wetu msaidizi Matola amekabidhi barua ya kujiuzulu jana (juzi) na amesema sababu ya kufanya hivyo ni kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mkuu…kamati yetu ya utendaji itakutana muda wowote kuanzia sasa kulijadili na kutoa ufafanuzi zaidi ya hilo," alisema Manara. Matola amejiuzulu huku Simba ikiwa kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 21.
Chanzo: HabariLeo