Matola abwaga manyanga Simba

Mimi namshukuru Mungu siku hizi sifuatilii sana habari za Simba, maana kufuatilia habari za Simba inabidi uwe na akili kama za mwendawazimu hivi (In Nyerere's voice).

Mtu unapoteza muda kufuatilia habari za timu, unapoteza muda kwenda uwanjani, unapoteza hela kulipia kiingilio halafu viongozi wanafanya ujinga ujinga na mwisho wake unaumia roho bure.
 
Simba haiuzwi Ng'o kama kweli mnaipenda simba chukueni kadi halfu mtoe mawazo najua wengine mna kadi tatizo mnalalamika sana badala ya kuhoji uongozi nani aliyepitisha bajeti ya simba kupata milionin50 kwa mauzo ya jezi hivi mlishinda kuhoji huo mchanganuo kuwa ni jezi ngapi zitatengenrzwa mpaka wakfikia hiyo hesabu inabidi muache kulalamika na mchukue hatua njia nyingine kama mnaona viongozi wamekuwa wabishi ni kugoma kununua jezi na kugoma kuingia uwanjani hadi matakwa yenu yatimizwe njia inatumika sana mfano kunakipindi wakati ac milan inayumba washabiki walimwambia mmiliki hawaingii uwanjani hadi anunue mastaa ndio kipindi walinunuliwa wakina Rui costa,Nesta na wengineo
 
Mimi nazungumzia timu in general. Hii ya matola ni matokeo tu. Kuna watu pale hawamtaki matola wengine hawamtaki Kerr. Lakini chanzo ni nini?

ngoja tuone mwisho wake
 
Simba ipo chini ya wahuni yaani inaongozwa kihuni tu mfumo ule ule wa kizamani unaendelea....bora ya wameimprove kiuongozi
 
Nanusa dalili ya mtu kuabudiwa kwa sababu ya uzungu wake, nammis Mwina Kaduguda, sehemu kama hizi ndio anaoneshaga ubora wake.
 
Somethin is not right somewhere. Huyu Matola kusema eti wachezaji wanapewa mazoezi mepesi sielewi hasa anaongelea nini. Timu ilikaa Lushoto, Zenji, na then DSM wakijifua, sasa mechi za ligi zimeanza analalamika hawafanyi mazoezi asubuhi na jioni ??
Naona hapa kuna uswahili na sio kufuata mpira wa kisasa. Je, hizo mechi kibao walizoshinda wameshindaje ??

Uswahili ndiyo unaharibu timu hizi. Mimi niliwahi kumuonyesha MO zamani kuwa ni njaa tu za watu ndiyo zinaleta shida. Nilimwambia anipe timu week tatu, nikampa dk na kocha mkenya kazi ya kutayarisha menu ( waseme wanataka nini) tukatafuta uwanja, na sehemu nzuri ya kulala na bajeti MO akatoa hela, na nikasimamia mimi hakuna cha katibu mwenezi wala madudu yake.
Vijana pale dining maziwa na juisi, na matunda yapo 24/7 na mlinzi getini hakuwa anafungua wala ruhusu mtu kutoka bila ruhusa yangu- kocha alikuwa anawasiliana na mimi kila mara. Basi najaza mafuta mimi full tank (sio kumpa dereva hela alafu baada ya siku mbili anasema tanki linavuja au anazurura kununulia sigara na kubeba mademu kwa players). Tena enzi za akina Masatu na Mwameja wakiwa wakongwe: siku ya pili walilalamika eti wanafanywa kama watoto nikawaambia nitawakatia ticket warudi DSM wakalalamike vizuri (najua kuna viongozi wanawapapatikia), na mtu kama Nteze ambaye alishakaa nje na anajua professional futbol ilivyo akawa anawaambia hii itasaidia timu.

Mara moja weekend tena mji ukiwa dead ndiyo tulikuwa tunatoka as a team kwenda mjini, tembea as a team kupata fresh air na then ndani ya basi na kurudi kambini.
Ligi imeanza, dozi zikawa kama kazi, na kocha akawaambia viongozi km mkiwa kama yule jamaa tutafika mbali. Kumshangaza MO, chenji ilibaki tena nyingi sana nikamrudishia akabaki mdomo wazi ! Players ni kama watoto, lazima uwe na msimamo na then wakitekeleza majukumu unawapa rewards. Walichukia sana lkn walivyokuwa wanapiga watu mkono (5) mwisho wa gemu wanasema ah braza ile kambi kweli noma na hapo nawaambia baada ya kazi hivi mnaweza kujipoza ila kesho kocha atawanyosha !

Haya mambo ni rahisi sana, na hayahitaji PhD bali msimamo na kutokuwa na njaa ya kutaka kukwiba au kujinufaisha.

Mwachieni kocha na mwisho wa siku mhukumu kwa matokeo sio mambo ya kutaka kumwingilia kila siku !!
 
amfuate Julio inawezekana muzungu keshashtuka anaogopa wachezaji wake
 
lakini Matola hajatofautiana na viongozi ila katofautiana na kocha mkuu.

Mkuu Matola anatumika na viongozi kumfanya Kerr aonekane hafai.Mwisho wa siku,watamtimua Kerr halafu Matola ataungana na kocha atakayeletwa.Mark my words.
Viongozi wamekosa commitment ndiyo maana mambo yanaendana shaghala baghala.Watendaji wazuri wote wenye dhamira ya kweli hawawezi kudumu Simba badala yake watabaki wababaishaji wenzao.
Ushauri wangu,wanachama waridhie timu kuwa mikononi mwa MO DEWJI ili tuondokane na haya mashaka.Menejimenti iliyopo ni ya watu wa kupiga dili.
Van Gaal.
 

...kama hili la kumrudisha matola litatokea endapo kerr ataondoka, nitarudi kuishangilia simba siku Dewji atakapopewa hiyo timu.
Japo nina wasiwasi km hao viongozi wa simba wanaweza kuitoa hiyo timu, kwa sababu ni wapiga dili, na wanaitumia simba kama kitega uchumi chao, kwa manufaa yao.
Wamejaa maneno mengi midomoni, vitendo hakuna! wanakatisha tamaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…