Somethin is not right somewhere. Huyu Matola kusema eti wachezaji wanapewa mazoezi mepesi sielewi hasa anaongelea nini. Timu ilikaa Lushoto, Zenji, na then DSM wakijifua, sasa mechi za ligi zimeanza analalamika hawafanyi mazoezi asubuhi na jioni ??
Naona hapa kuna uswahili na sio kufuata mpira wa kisasa. Je, hizo mechi kibao walizoshinda wameshindaje ??
Uswahili ndiyo unaharibu timu hizi. Mimi niliwahi kumuonyesha MO zamani kuwa ni njaa tu za watu ndiyo zinaleta shida. Nilimwambia anipe timu week tatu, nikampa dk na kocha mkenya kazi ya kutayarisha menu ( waseme wanataka nini) tukatafuta uwanja, na sehemu nzuri ya kulala na bajeti MO akatoa hela, na nikasimamia mimi hakuna cha katibu mwenezi wala madudu yake.
Vijana pale dining maziwa na juisi, na matunda yapo 24/7 na mlinzi getini hakuwa anafungua wala ruhusu mtu kutoka bila ruhusa yangu- kocha alikuwa anawasiliana na mimi kila mara. Basi najaza mafuta mimi full tank (sio kumpa dereva hela alafu baada ya siku mbili anasema tanki linavuja au anazurura kununulia sigara na kubeba mademu kwa players). Tena enzi za akina Masatu na Mwameja wakiwa wakongwe: siku ya pili walilalamika eti wanafanywa kama watoto nikawaambia nitawakatia ticket warudi DSM wakalalamike vizuri (najua kuna viongozi wanawapapatikia), na mtu kama Nteze ambaye alishakaa nje na anajua professional futbol ilivyo akawa anawaambia hii itasaidia timu.
Mara moja weekend tena mji ukiwa dead ndiyo tulikuwa tunatoka as a team kwenda mjini, tembea as a team kupata fresh air na then ndani ya basi na kurudi kambini.
Ligi imeanza, dozi zikawa kama kazi, na kocha akawaambia viongozi km mkiwa kama yule jamaa tutafika mbali. Kumshangaza MO, chenji ilibaki tena nyingi sana nikamrudishia akabaki mdomo wazi ! Players ni kama watoto, lazima uwe na msimamo na then wakitekeleza majukumu unawapa rewards. Walichukia sana lkn walivyokuwa wanapiga watu mkono (5) mwisho wa gemu wanasema ah braza ile kambi kweli noma na hapo nawaambia baada ya kazi hivi mnaweza kujipoza ila kesho kocha atawanyosha !
Haya mambo ni rahisi sana, na hayahitaji PhD bali msimamo na kutokuwa na njaa ya kutaka kukwiba au kujinufaisha.
Mwachieni kocha na mwisho wa siku mhukumu kwa matokeo sio mambo ya kutaka kumwingilia kila siku !!