Kuna aina nyingi za Range Rover na bora katika zote nilioiendesha lilikuwa autobiography hilo dude bei yake barabarani lilikuwa £90,000 (bei ya UK)
Zingine nilizoendesha ni vogue na evogue pamoja na sport na Velar kwa kweli kama ni gari haya ndio ya kuendesha na kila mmoja anaendesha awe dume au jike
Yapo yenye muonekano mkubwa na yapo madogo
Lakini kama hujapenda unaweza ukatungua hata Land rover discovery ambalo lina heshima yake kubwa pia na ukiingia ndani na kuliendesha kwanza ukilitekenya tu ile button likawaka haliondoki bila kugusa kitufe kimoja hapo halafu unaliona linavyohiweka sawa katika ardhi.
Halafu ukiwa unashuka kwenye mteremko ina button unaigusa inanyanyuka mbele
Pia unaweza kuishusha chini na kuipandisha juu yaani kama ni beast hilo ni baba lao
Sent from my SM-G570F using Tapatalk