SI KWELI Matone ya kitunguu maji yanaweza kutuliza maumivu ya sikio?

SI KWELI Matone ya kitunguu maji yanaweza kutuliza maumivu ya sikio?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kwenu Wataalam, Naomba ufafanuzi kabla sijajitoa muhanga na kuwa kiziwi kabisa na milele

1786095967721.png

Picha ya AI​
 
Tunachokijua
Baadhi ya watu wamekuwa na imani ama kuambiwa kuwa matumizi ya baadhi ya vitu ikiwemo vitunguu maji inaweza kutibu maumivu ya sikio.

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alichapisha video na kueleza kuwa watu wenye maumivu ya sikio ama yanayotoa uchafu wanaweza kutumia maji ya vitunguu maji kuweka sikioni inaweza kuwa na tiba ya jambo hilo.

JamiiCheck imefuatilia na kubaini yapo baadhi ya machapisho kupitia makala tofauti ambazo zinabainisha kuwa vitunguu maji vina viambata ambavyo vinaweza kutumika kama tiba ya maumivu sikioni, lakini je ni salama?

Daktari Godlove Mfuko, Daktari Bobezi wa Mishipa ya Fahamu na Usikivu na Usawazo kutokea hospitali ya Taifa ya Muhimimbili-Mloganzila anafafanua kuwa kufanya hivyo ni hatari kwa afya ya sikio na mwili kwa ujumla wake.

Dkt. Mfuko anafafanua kuwa maumivu ya sikio yanaweza kuwa ni ishara ya changamoto nyingine kutoka katika sehemu ya mwili ikiwemo koo.

“Kwanza, kwanza ni hatari sana... Nadhani ni sentensi ya kwanza tu. Ni hatari sana kuweka chochote kwenye sikio kama linauma. Ni very dangerous. Kwa sababu kinachokufanya usikie maumivu ni mishipa ya fahamu. Tunaita ni pain receptors.

Wewe unajua... unapata maumivu kwa sababu tafsiri ya maumivu inatoka kwenye mfumo wa fahamu wa kati.”
- Dkt. Mfuko

Tovuti ya Mimi kupitia makala yao ya debunking ear myth wanaeleza kuwa si salama kutumia tiba za majumbani kwa ajili ya maumivu ya sikio na badala yake ni vema kwenda kukutana na wataalau wa afya.

Inabainisha kuwa tiba hizo zinaweza kusababisha changamoto kama vile;

“Maumivu ya sikio yanaweza kuwa dalili ya matatizo mbalimbali, ikiwemo maambukizi, kuziba kwa sikio, au hali nyingine mbaya. Hivyo basi, ni muhimu sana kumuona mtaalamu wa afya ambaye anaweza kutambua chanzo cha tatizo na kupendekeza matibabu sahihi ili kulitatua kwa ufanisi”.
Back
Top Bottom