Matonya aliamsha dude ni kuhusu wimbo wa zilipendwa

Kah! Huyu naye anatafuta kiki sasa na mimi nikiandika ngoma yangu nyingine beat nyingine na kuipa jina la "vaileti" nitakuwa nimemkopi? Naamini waru hawajui maana ya ku copy au ku sample. Kuna hatimiliki ya jina la wimbo?
 
Sasa amekupiwa nini kwenye huo wimbo? Yeye ni mmiliki wa neno Zilipendwa?
Unajua hawa wasanii walivyosikia kuwa AY na FA wamepiga hela kupitia Tigo basi wanafikiri ni rahisi tuu basi unapewa hela...Sijaona ni wapi WCB wamekopi kutoka kwa Matonya zaidi ya kufanana kwa jina la wimbo maana melody,beat,maneno na kila kitu ni tofauti kabisa...
Sasa ana fananisha na swala la saida wakati kwa saida ni kweli walikopi kila kitu tofauti na yake ambayo ina tofauti...
Matonya mjini hakuna hela ya bure utasaga meno.
 
Matonya yuko sahihi Ku claim, kwa sababu ..diamond amechukua the whole idea ya nyimbo ya matonya, maswala ya zilipendwa ilishaimbwa na matonya and everyone knows , sasa matonya asidai haki yake??.....ivi ingekuwa diamond katoa alafu matonya akaja kuimba tena... Unadhan ingekuwajee?....matonya apewe credit zake bana
 
Hovyo kwelikweli!

Msanii wa zamani kama huyu anakurupuka kijinga hivi?
 
Naomba wajuzi wa mambo ya mziki mnifahamishe ...hv msanii akiiga jina la wimbo wa msanii mwingine
kuna adhabu yoyote ya kisheria ?
 

"Maswala ya zilipendwa zilishaimbwa na matonya"

Hii sentensi yako ina ukakasi mahali...ina maana mtu akiimba maswala ya upinzani/kilimo/kufumaniwa haruhusiwi msanii mwingine kuja kuimba masuala hayo hayo yalioimbwa na waliopita?

Nikieleweshwa nitashukuru.
 
Umenikumbusha M4C ya Bwana Pombe.

"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…