Matonya aliamsha dude ni kuhusu wimbo wa zilipendwa

kwani matonya ndio ana mwandiko mbaya hivyo!? kama ndio basi hajaibiwa kwani kwa uandishi huo asingeweza kuandika yale mashairi.
 
Habari za jumapili wakuu , kwa povu hilo VP matonya yuko sawa?? Kama ni kweli wameiba idea ya matonya Hawa watu wataishia pabaya aisee


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ana hati miliki na jina ZILIPENDWA?? Aache upoyoyo, aya! Tumemsikia naye, angalau WCB wamempa umenyo wa kusikika!
Sielewi haya mapovu ya watu kuhusu huu wimbo yanatoka wapi, masikioni au puani au mdomoni!
 
Lets wait and see.
Sina shida ya pesa ila haki itafuata mkondo..

Afu kule mwisho kuna kionjo cha beat la wimbo mmoja hivi wa zilipendwa je wenye biti nao waliamshe dude?
 
ukweli usemwe idea, na kibwagizo ni vya matonya, hakuna kilicho fanyika cha maana kwa domo na genge lake zaidi ya uhuni tu.
 
Ni upuuzi tu. Hajaibiwa kitu na wala asifananishe na kesi ya Saida Karoli. Kule imechukuliwa sample ya beat, vipande vya mashairi n.k. Yeye kwake kimechukuliwa kitu gani? Kusema tu idea bila kuonesha kwa kiasi gani wameiba ubunifu wake ambao upo wa kipekee hio sio sahihi. Nadhani somo la intellectual property lifundishwe vizuri kwa wasanii wasichanganye mambo.
 
Matonya kama anashida na hela awaombe watu kistaarabu!!
Ule wimbo nimeusiliza labda wangesema Msondo na Les Wanyika!! Mengine mle naona burudani tu, "magari ya udongo, babu wa loliondo,"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini tulimsahau, sasa hivi tumemsikia angalau!
 
Hakuna mmiliki halali wa jina lolote katika wimbo,nyimbo nyingi zinaweza kuwa na jina moja ila idea tofauti,hata idea ikiwa moja na jina ni moja bado ni ngumu sana kusema umeibiwa nyimbo,mimi sio m WCB ila penye haki tuseme,Matonya anajilinganisha yeye na Saida Karoli kama kuidhinisha malalamiko yake kwa Wasafi,kitu amabacho si kweli kabisa yaani hakuna uhusiano hata chembe,Kwa Saida karoli wasafi wamechukua vitu vingi ikiwa Idea,beat,hadi vionjo kwa asilimia kubwa kutoka kwenye nyimbo ya Saida karoli,yaani karibia asilimia 90,kwa matonya wamechukua jina tuu la nyimbo kitu amabcho kwa wanaoelewa mziki hawawezi kumuelewa Matonya hata kidogo,kuna nyimbo nyingi sana zinazofanana majina ila idea na waimbaji tofauti
 
Ye mwenyewe kamuibia jina yule mzee Matonya ombaomba, sijui BASATA wako wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…