Matonya amekamatwa na madawa China ?

Matonya amekamatwa na madawa China ?

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Matonya amefunguka kuhusu tuhuma zilizosambaa kuwa amekamatwa na Madawa ya Kulevya nchini China akisisitiza kuwa sio kweli na wala yeye hajawahi kujihusisha na biashara hiyo kwenye maisha yake.

MATONYA 123.jpg


Mkali huyo wa Bongofleva akiongea na eNEWZ amesema taarifa hizo zilimkwamisha sana kwenye mipango yake mingi pamoja na mama yake kuumizwa nazo kiasi cha kumpigia simu na kumuuliza kama ni kweli.

''Kiukweli nimesikitika sana na sio mimi tu hata mama na familia yangu kwa ujumla, mama alikuwa akinipigia simu kila muda akitaka kujua kama ni kweli lakini tulizushiwa wengi akiwemo Alikiba japo ya kwangu ilivuma sana ila ni fununu tu haina ukweli'', amefunguka.

Msanii huyo pia ametoa ya moyoni kuhusu stori zilizopo kuwa anabifu na msanii Alikiba kitu ambacho amesema anashangaa kimetokea wapi kwasababu wao wako poa ila hajua fununu hizo zimetoka wapi.
 
Hii kiki imebuma, bora tu atafute kazi ya maana afanye.
 
Back
Top Bottom