Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 8,273
- 13,567
Habari ndugu zangu?
Naomba niseme haya ili wenye mamlaka wawachukulie hatua ikiwemo waziri wa mambo ya ndani na IGP nk.
Ifakara na Lupiro ipo mkoa wa Morogoro.
Iko hivi trafiki wa Ifakara hasa maeneo ya kabla na baada ya daraja la Magufuli (Kivukoni) wamekuwa kero sana kwa waendesha bajaji kwa kuwadai 2,000(elfu mbili) kila wanapopita hapo, na dereva asipotoa hiyo pesa humwandikia faini ya elfu kumi au kumtishia kumpeleka kituo cha polisi.
Yaani wamejihalalishia malipo ya pesa hizo kuwa ni stahiki zao,nasikia huko nyuma dereva bajaji walilalamika sana mkuu wa wilaya aliingilia kati na wakapunguza kuchukua elfu mbili toka kwa kila bajaji inayopita.
Kwa kifupi hakuna bajaji inayopita bila trafiki kuchukua elfu mbili. Pia trafiki wa Lupiro jirani na stendi ya mabasi ya Lupiro nao tabia zao za kuchukua elfu mbili zipo palepale, najiuliza mshahara hautoshi au lengo lao ni kufanya maisha ya dereva bajaji yawe ya dhiki kila kukicha?
Kama kuna taasisi inayoitwa ya kuzuia rushwa nendeni Ifakara na wilaya ya Ulanga mkaone matrafiki wanaochukua rushwa bila haya wala woga.
Nawasilisha.