Matrafiki wameanza tena kamata kamata

Matrafiki wameanza tena kamata kamata

Tufanye nini sasa kama waliopewa mamlaka wanafosi, ujue hatutoi kwa hiyari.
kuna mmoja pale Misigiri nilimfinyia buku kwenye kadi akagoma bana,tukaanza kupatana nikamwambia"sina kitu nakuongeza jero tu",,akaniambia weka chuma pembeni,na mimi nikagoma kupaki pembeni, nikamuuliza"unataka shilingi ngapi?",akaniambia weka buku tano hapo.nikaongeza buku ikawa buku mbili akakubali akaifinya.akaniruhusu nikasepa.
 
kwani ukiwa umekamilisha vibali gari yako iko smart una leseni yako bado wnaasumbua maana saa nyingine tunalaumu askari wa usalama barabarani ila sisi hatujikamilishi kny vyombo vyetu
 
Kwanini wanashindwa kilivunja hili Geshi na kusuka jipya wanajua kampeni zitakapoanza watalihitaji katika "kuwanyoosha" Wapinzani.
 
Kuna watu mkiwa na magari mnajiona mmemiliki Dunia. Hufuati sheria, mtembea kwa miguu kwako ni takataka tu. Traffic endeleeni nao mpaka waheshimu maisha ya wenzao.
Bila shaka utakuwa sehemu ya wanufaika!! Tunatakiwa kutumia technologia!! Kamera zinatosha
 
kwani ukiwa umekamilisha vibali gari yako iko smart una leseni yako bado wnaasumbua maana saa nyingine tunalaumu askari wa usalama barabarani ila sisi hatujikamilishi kny vyombo vyetu
Definitely wewe unaishi huko Lala land country sio Tanzania
 
Definitely wewe unaishi huko Lala land country sio Tanzania
nipo hapahapa tz na sijawah sumbuliwa na hao askari wa usalama barabarani nikiwa na chombo chochote cha moto iwe bike iwe gari na sio dar tu hata mikoani nikienda kusalimia niko huru sana ndio maana nashangaa, au kuna uonevu baina ya mtu na mtu mpka wanachukiwa sana watu wa usalama barabarani au ni mapungufu yetu wenyewe wamiliki wa vyombo vya moto ?
 
Definitely wewe ni working class unayetumia SU au ST number plate, kati ya Dar na Morogoro kuna zaidi ya 10 to 15 road blocks na nyingi ni za kimchongo, ila mkuu wewe unapita salama mmmmm labda tunaishi in a different planet, rushwa ya traffic officer's in Tanzania ni terminal cancer
 
Kuna haja ya kutengeneza Mswada was Sheria ya Mageuzi ya Utendaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.

CCM chini ya mzee Comrade Kinana
Liangalie hili. Litawapa kukubalika na wananchi 2025

Lakini pia CDM ya Mbowe na Mnyika hii ni fursa ya kuamsha upya ushawishi.

Vinginevyo tamko la Makamu Myenyekiti Kinana kitengo cha Trafiki wamekataa kuliheshimu
 
Miezi michache baada ya rai ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Comredi Adulrahaman Kinana kwa jeshi la polisi kupunguza bugudha kwa magari na hasa maeneo ya mijini, hali imebadilika na taratibu inaanza kujirudia kama ilivyokuwa awali.

Ule unafuu uliokuwa umeanza kupatikana sasa unapotea kwa haraka. Mfano, jijini Dar Es Salaam barabara ya Morogoro utawakuta wanabugudhi madereva pale Urafiki, Kimara Baruti, Kimara Temboni, Kibanda cha Mkaa, kwa Yusufu na maeneo hayo hayana umbali hata wa kilometema 3-5 katikati yake. Na ukiendelea mpaka Maili Moja Kibaha ndipo wamejaa kila umabali wa wastani wa kilometer mbili Luguruni, Kibamba, Kilivya, Maili Moja nk.

Haya ni matumizi mabaya ya pesa za walipakodi kulipa mishahara wafanyakazi wasio na tija au mzigo kwa jamii.

Mdau hebu na wewe ongezea kero unazokutana nazo za hawa watu pamoja na kutakiwa kupunguza bugudha zao.

Mwisho, Je polisi na hasa hawa wa barabarini wako juu ya sheria?
Yeah! wanatekeleza majukumu yao kisheria.
 
Itasaidia kupunguza ajali, madereva ni SAwa na mbuzi kujiongoza hawawezi
 
Back
Top Bottom