ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Gharama ya vita ni kubwa sana.“Matumizi ya vita yamefikia dola trilioni 2.2 katika vita mbalimbali ulimwenguni pote. Kiwango hicho hakijawahi kufikiwa wakati mwingine wowote.”—The Washington Post, Februari 13, 2024.
Hata hivyo, gharama zinachangiwa na mengi zaidi ya pesa. Fikiria mfano mmoja tu: Vita nchini Ukraine Wanajeshi Wataalamu fulani wanakadiria kwamba wanajeshi 500,000 hivi wameuawa au kujeruhiwa tangu vita hivyo vilipoanza miaka miwili iliyopita.Raia. Zaidi ya watu 28,000 wamekufa au kujeruhiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa. Ofisa mmoja wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa alisema hivi: “Haiwezekani kuhesabu ni maisha ya raia wengi kadiri gani ambayo yameharibiwa na vita hivi.”Wanadamu wamelazimika kuteseka sana kutokana na vita ulimwenguni pote.
Milioni 114. Idadi ya watu waliolazimika kuondoka makwao kwa sababu ya vita na jeuri ulimwenguni pote kuanzia Septemba 2023.
Milioni 783. Idadi ya watu wanaokabili njaa kali. “Vita ndicho kisababishi kikubwa zaidi cha njaa, kwa kuwa asilimia 70 ya watu wenye njaa ulimwenguni pote wanaishi katika maeneo yaliyoathiriwa na vita na jeuri.”Kwa mujibu wa Shirika la Chakula Ulimwenguni