Matrimonial assets

Matrimonial assets

32Roberts

Senior Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
109
Reaction score
17
Wakuu wa Sheria naombeni msaada,

kuna jamaa yangu mmoja wametofautiana na mkewe na mke amerudi kwao kama miezi minane iliyopita,

katika kujadili naye akanieleza walikuwa na argument ya kawaida tu na mkewe alimwambia anataka waachane,kesho yake jamaa yupo kazini mkewe akafungasha kila kitu na kuondoka zake,jioni jamaa anarudi akakuta hamna mtu ila mkewe amechukua nguo,viatu na vitu vinavyo mhusu tu vyote akaondoka navyo.

Alimwarifu jamaa kwamba ameondoka na amerudi kwao,

jama ame persue njia za usuluhishi ikiwemo kuongea na mkewe wasuluhishe ila mwanamke hataki kumsikiliza wala haelekei kuwa tayari.

Matron na Patron wamejaribu kuwasuluhisha ila bibie hataki katu kusikia swala linalo itwa suluhu.

jamaa amezungumza na wazazi wa binti na binti akaitwa aeleze tatizo akaishia kunyamaza na mazungumzo kuvunjika.

jamaa amefika mahali amekata tamaa na analoona mbele yake ni divorce.

Ila kuna vitu vinamchanganya zaidi,

1.kwakuwa yeye hakuwamtayari kuivunja ndoa je mahakama bado itafikiria kuhusu mgawanyo wa mali?

2.jamaa alioa akiwa tayari amejikamilisha kimaisha kwa maana ya mshara mzuri,nyumba na gari za kumtosha huku akiwa ana biashara zake zinazomtosheleza, na mkewe alivikuta vyotenhivi .... Sasa jamaa anajiuliza je hivi navyo vitakuwa kwenye scope of division?

3.mke naye alikuwa na kazi nzuri ila alikuwamhachangiimchochote ndani zaidi ya kumlipa maid tu,vingine vyoote jamaa alifoot na zaid alimextend hata kumsaidia wife wake madeni kwenye maduka ya nguo,je atalazimika kumtunza baada ya divorce?

4.jamaa hajaoa wala ku date mtu mwingine ila kwa sababu ya lonliness na pain anajikutanakihitaji walau mtu wa kumfariji... Je hili bado kisheria linachukuliwa kama adultery? Na ukizingatia mke katimkia kwao na hamtimizii jamaa mahitaji yake ya kindoa?

jamaa anauliza hizi consequences kabla hajaamua na kama final reconciliation itafail.

aliniuliza kwakweli nilishindwamkumpa majibu kutokana na fani kuwamtofauti na sheria.
 
ai...mwanamke si ndo anataka divorce na yeye, si hata usuluhishi...mwache aanze procedure mwenyewe,usijisumbue kichwa labda kama unauhakika kabisa kwamba unataka kumuacha which utaanza tu baraza la usuluhishi as per procedure, (waeleze kuhusu ulivyojaribu kusuluhisha n everytn,mayb wataitwa kuelezea) ikishashindikana utapewa form itakayokuruhusu uende mahakamani
mali mtagawana depending on mchango wa each party(kifedha na mengineyo) katika matrimonial property mliochuma kama alikukuta na kila kitu atapata hata 30/70 ila atapata tu
kama umefumaniwa, hiyo ni adultery,if not gud for you i ges.. kama unataka kuendelea na maisha yako endelea na procedure za divorce ( tafuta mwanasheria) if not, mwache aanze procedures mwnywe...lkn it seems ulifumaniwa wewe hahahahaaa
 
Kwa Mujibu wa jamaa hakufumaniwa na alikuwa ha cheat,

hii ilikuja kama supprise kwake na hwakuwa na mgogoro wowote.... Kilichotokea ni mkewe alimwambia waachane na following day akaondoka,

ila cha ajabu anaendelea kusimulia mkewe hajaendelea na procedures nyingine ila kakaa tu kwao confortably huku jamaa anaumia

ila ndo hivyo amejiuliza maswali hadi siku akaamua kufunguka yanayomsibu

jamaa nafikiri kwenye mgawanyo wa mali ndo panapomchanganya maaana inavyoonekana mkewe alikuwa hachangii

QUOTE=Viva89;5700383]ai...mwanamke si ndo anataka divorce na yeye, si hata usuluhishi...mwache aanze procedure mwenyewe,usijisumbue kichwa labda kama unauhakika kabisa kwamba unataka kumuacha which utaanza tu baraza la usuluhishi as per procedure, (waeleze kuhusu ulivyojaribu kusuluhisha n everytn,mayb wataitwa kuelezea) ikishashindikana utapewa form itakayokuruhusu uende mahakamani
mali mtagawana depending on mchango wa each party(kifedha na mengineyo) katika matrimonial property mliochuma kama alikukuta na kila kitu atapata hata 30/70 ila atapata tu
kama umefumaniwa, hiyo ni adultery,if not gud for you i ges.. kama unataka kuendelea na maisha yako endelea na procedure za divorce ( tafuta mwanasheria) if not, mwache aanze procedures mwnywe...lkn it seems ulifumaniwa wewe hahahahaaa[/QUOTE]
 
basi aanze procedure, kama kuna matrimonial property lazima mgawane, kuchangia sio kwa hela tu maintaining the home ni mchango pia
 
Wakuu wa Sheria naombeni msaada,

kuna jamaa yangu mmoja wametofautiana na mkewe na mke amerudi kwao kama miezi minane iliyopita,

katika kujadili naye akanieleza walikuwa na argument ya kawaida tu na mkewe alimwambia anataka waachane,kesho yake jamaa yupo kazini mkewe akafungasha kila kitu na kuondoka zake,jioni jamaa anarudi akakuta hamna mtu ila mkewe amechukua nguo,viatu na vitu vinavyo mhusu tu vyote akaondoka navyo.

Alimwarifu jamaa kwamba ameondoka na amerudi kwao,

jama ame persue njia za usuluhishi ikiwemo kuongea na mkewe wasuluhishe ila mwanamke hataki kumsikiliza wala haelekei kuwa tayari.

Matron na Patron wamejaribu kuwasuluhisha ila bibie hataki katu kusikia swala linalo itwa suluhu.

jamaa amezungumza na wazazi wa binti na binti akaitwa aeleze tatizo akaishia kunyamaza na mazungumzo kuvunjika.

jamaa amefika mahali amekata tamaa na analoona mbele yake ni divorce.

Ila kuna vitu vinamchanganya zaidi,

1.kwakuwa yeye hakuwamtayari kuivunja ndoa je mahakama bado itafikiria kuhusu mgawanyo wa mali?

2.jamaa alioa akiwa tayari amejikamilisha kimaisha kwa maana ya mshara mzuri,nyumba na gari za kumtosha huku akiwa ana biashara zake zinazomtosheleza, na mkewe alivikuta vyotenhivi .... Sasa jamaa anajiuliza je hivi navyo vitakuwa kwenye scope of division?

3.mke naye alikuwa na kazi nzuri ila alikuwamhachangiimchochote ndani zaidi ya kumlipa maid tu,vingine vyoote jamaa alifoot na zaid alimextend hata kumsaidia wife wake madeni kwenye maduka ya nguo,je atalazimika kumtunza baada ya divorce?

4.jamaa hajaoa wala ku date mtu mwingine ila kwa sababu ya lonliness na pain anajikutanakihitaji walau mtu wa kumfariji... Je hili bado kisheria linachukuliwa kama adultery? Na ukizingatia mke katimkia kwao na hamtimizii jamaa mahitaji yake ya kindoa?

jamaa anauliza hizi consequences kabla hajaamua na kama final reconciliation itafail.

aliniuliza kwakweli nilishindwamkumpa majibu kutokana na fani kuwamtofauti na sheria.
hapatakuwa na divorce mpaka ipite miaka 3 ambapo kwa sababu ya kutelekezwa huyo mwanaume anaweza akaomba talaka na akapewa, ila mtu aliyesababisha ndoa kuvunjika hawezi kustahili mgao.
 
duh basi sheria ya Ndoa Tanzania ni kandamizi kwa wanaume,kwasababu jamaa anavyosimulia mwnamke ni kama alikuja na kukaa kama malkia ilipo fika siku yake anajisikia kuondoka akaondoka japo mambo mengine yalikuwa yakiendelea kama kawaida.

sasa matrimonial assets zinaanzia wapi kabla au baada

basi aanze procedure, kama kuna matrimonial property lazima mgawane, kuchangia sio kwa hela tu maintaining the home ni mchango pia
 
Kwanza soma hii thread labda itakusaidia: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...da-wa-mgawanyo-wa-mali-baada-ya-talaka-2.html

Pili, naomba nikuulize swali. Wahusika wana watoto? Kama wana watoto wana umri gani?

Tatu unless kama sheria imeshabadiliswa makala ya Allan Kajembe yenye kichwa cha habari "Yanayojiri baada ya tamko la Talaka mahakamani" inaweza kukusaidia. Nimeweikwa hapo chini

========

MADA ya leo ni mojawapo ya vitu vinavyozua mambo na mvurugano katika jamii nyingi. Hapa nazungumzia mipango yote na vyote vitakavyojiri baada ya mahakama kutoa tamko la kuivunja ndoa kwa kutoa hati ya talaka. Kimsingi, ni mambo mawili yanayojumuishwa tunapozungumzia mipango baada ya tamko la kuivuja ndoa, mambo haya ni mgawanyo wa mali na kupata haki ya kubaki na watoto.

Suala gumu ni linalojumuisha mgawanyo wa mali. Na kifungu cha 14 cha Sheria ya Ndoa, 1971 kilileta mgongano mkubwa wa kitafsiri ambao ulidumu kwa miaka 10 katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Neno juhudi za pamoja, ndilo hasa lililoleta utata wa tafsiri kwani swali lililojitokeza ni je, kazi anazofanya mama wa nyumbani kama kupika, kuosha vyombo na kumfulia nguo mumewe, nazo ni sehemu za juhudi za pamoja? Upande mmoja wa majaji walikubaliana na mtazamo kwamba kazi hizi nazo zinajumuishwa kama juhudi za pamoja na upande wa pili ukikataa mtazamo huo.

Baada ya miaka 10 ya mvutano huu, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kupitia moja ya shauri maarufu zaidi katika masuala ya ndoa, Hawa Mohammed dhidi ya Ally Seif (1983),TLR, 32, ilitoa msimamo kwamba majukumu ya mama nyumbani nayo yanajumuika kama sehemu ya neno juhudi za pamoja, kwani hata mume anahitaji chakula kilichopikwa vizuri, nguo safi na kadhalika.

Na hivi mara nyingi vinafanywa na kina mama (hasa wale wasiofanya kazi maofisini). Hata hivyo, Mahakama ya Rufaa iliongeza kitu cha ziada kwamba, pale mwanandoa anapotenda kosa linaloathiri ndoa yake, kosa hilo linapunguza kabisa mchango wake katika juhudi za pamoja na anaweza kuondoka mikono mitupu kabisa.

Hata hivyo, wakati wa kugawanya mali za wanandoa, vitu vya kuzingatia ni maendeleo ya watoto na mila na desturi za kabila husika, inapotokea wanandoa wanatoka makabila tofauti na hivyo mila na desturi zao zinatofautiana, basi mahakama itazingatia zaidi sheria za nchi kuliko mila na desturi za makabila hayo.

Katika shauri la Mohammed Abdalah dhidi ya Halima Msangwe (1988), TLR, 197 mahakama iliamua kwamba mgawanyo wa mali si suala la kulipana fidia bali ni kitendo cha kumpa mtu stahiki yake kwa juhudi za pamoja za kujenga familia yao. Shauri jingine linaloleta tafsiri pana zaidi juu ya mgawanyo wa mali ni la Bibie Maulidi dhidi ya Mohammed Ibrahim (1989),TLR, 162 ambapo mahakama ilikataa utetezi kwamba mali ya wanandoa walioachana inatakiwa igawanywe nusu kwa nusu.

Na kutoa maamuzi kwamba sheria haijatamka kwamba mali zigawanywe nusu kwa nusu, na kwamba kinachoangaliwa zaidi ni ustawi wa watoto, madeni yanayoikabili familia, labda mikopo ya benki na kadhalika, pia mila na desturi za wahusika.
Kwa hiyo kimsingi, mahakama inatuambia kwamba hakuna fomula moja, bali maamuzi yatategemea kesi yenyewe ilivyo.

Suala la pili la msingi ni haki ya kukaa na watoto. Hili pia ni suala linaloleta migogoro na migongano ya mara kwa mara kwa watu waliotalikiana. Kitu ambacho ndugu msomaji unatakiwa kuzingatia hapa ni kwamba watoto wanaozungumziwa hapa ni wale walio chini ya miaka saba, kwani chini ya sheria hii, kuna makundi mawili ya watoto, wale walio chini ya miaka saba na wale walio juu ya miaka saba.

Kwa watoto walio chini ya miaka saba, basi kwa ujumla ni kwamba mama ndiye atakayepewa jukumu la kukaa na watoto.
Hata hivyo wakati mwingine hii haitakubalika ikiwa tu tabia na hali ya kiakili na kifedha ya mama itathibitika si shwari. Kanuni kuu inayozingatiwa na mahakama wakati wote wa kutoa haki ya kuishi na watoto ni ustawi na maendeleo ya mtoto/watoto kwanza na si majigambo au vita ya wazazi.

Hii ina maana kwamba, ustawi wa mtoto ndiyo kitu cha kwanza na kwamba mtoto ni mali ya Jamhuri na hivyo Jamhuri ina jukumu la kuhakikisha kwamba ustawi wa mtoto unazingatiwa kwanza. Kwa mujibu wa kifungu cha 125 cha Sheria ya Ndoa, 1971, sheria imeweka wazi juu ya ni nani anaweza kupewa haki ya kukaa na watoto baada ya wazazi kuachana.
Hapa sheria inasema kwamba ni mtu yeyote anaweza kupewa haki ya kukaa na watoto ikiwa tu mahakama itaridhika kwamba baba na mama wa watoto hao hawawezi kufanya hivyo.

Mahakama ina uwezo wa kuamuru wapi mtoto akasome, wapi akaishi na hata wakati mwingine dini gani afuate kwa kuzingatia mazingira ya kesi yenyewe. Inapotokea mzazi mmoja akafariki, ndugu wa mzazi huyo wataruhusiwa kila wakati utakaofaa kufanya hivyo. Hata hivyo, chini ya kifungu cha 126(e) cha sheria hii, sheria imekataza kwa hifadhi ya mtoto kupelekwa nje ya nchi na mtu aliyechaguliwa kuwalea.

Katika shauri la Mariam Tumbo dhidi ya Harod Tumbo (1983), TLR, 293, mahakama iliamua kwamba linapokuja suala la kuishi na watoto baada ya tamko la talaka, inapotokea mtoto mwenyewe akatoa maoni yake juu ya wapi anapenda kwenda kukaa ( yaani kwa baba au kwa mama), mahakama inatakiwa kuzingatia maoni hayo ya mtoto.

Wakati hali ya kitabia, kifedha, kiakili na kimaadili inapobadilika kwa mtu aliyepewa haki ya kulea watoto, kwa mfano, mtu aliyepewa watoto hao alikuwa si mlevi kupindukia, na alikuwa ana uwezo wa kuwapeleka shule vizuri, lakini baada ya kupewa watoto anaanza kubadilika na kuwa mlevi kupindukia, au mwenye matatizo ya akili, basi upande wa pili una haki ya kwenda katika mahakama ileile iliyompa haki ya kukaa na watoto mara ya kwanza na kuiomba ibatilishe tamko hili kwa sababu hali ya mlezi imebadilika.

Hii ni kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama katika shauri la Halima Kalima dhidi ya Jayantulahu (1987)TLR,147.
Kwa kuhitimisha tu, mambo makuu mawili ndiyo yanayoangaliwa pale watu waliopata hati ya talaka mahakamani wanapoanza kuangalia mipangilio baada ya talaka. Mambo haya ni pamoja na mgawanyo wa mali zilizopatikana wakati wa ndoa na pili ni suala la malezi ya watoto baada ya tamko la mahakama la kuivunja ndoa hiyo.

Chanzo: Yanayojiri baada ya tamko la talaka mahakamani
 
Swala la kupeana talaka kwa mjibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania ya 1972, siyo rahisi kihivyo ni hadi ndoa iwe haiwezekani tena, kwa sheria wanasema (irrepelable) kitendo anachofanya huyo mwanamke kukaa kwao ni njia pia ambayo inatambuliwa na sheria hiyo kama hatua za kuirudisha ndoa kama mwanzo ( mnatengana kwa mda kwa ajili ya kujipa mda kutafakari na huenda baada ya mda kupita mkaamua kurudiana, LAKINI, NA HAPA NAOMBA TUELEWE katika kipindi hiki mume hana haki ya kumfuata na kutaka haki ya ndoa na ukilazimisha wakati muko separate unakuwa ni ubakaji)
Sasa hoja ni taraka, kisheria taraka inatoka baada ya ndoa kuwa katika hali niliyosema hapo juu, pili lazima iwepo hati kutoka katika baraza la usuruhishi la kata ikionesha siyo tu kwamba imesuluhisha jambo hilo, lakini pia imeshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo na kwa mtazamo wa baraza ndoa hiyo haiwezi tena kuendelea

Kwa hali hiyo huyu mwanaume anaona kabisa hawezi kutoa taraka kwa sababu vigezo hivyo havijatimia,

USHAURI WANGU; Mtoa mada kuna kitu atakuwa hajasema au hajafanyia uchungunzi kuhusu hiyo familia yake, nadhani aachane na harakati za taraka kwa sababu hata mke wake ( hata mume) hawezi kufanya chochote na akifanya utakuwa ni uzinzi kwa vile bado ni ndoa halali hiyo, afanye usuruhishi lazima kuna sababu huyo mke wake siyo chizi
Kama wakipeana taraka kugawana mali ni jambo ambalo halizuiliki japo mwanamke hakuchangia kwa mali, kitendo cha yeye kuwepo nyumbani kinatoa mchango kwa mafanikio kwa mwanaume huyo rejea hukumu ya kesi ya Bi Hawa Mohamed
Kuhusu hisia za kutaka mwenzake (kama binadamu wengine)kisheria itakuwa ni uzinifu japo kama binadamu anahisia.
 
Nilikutana na mheshimiwa and aliona thread hii na anakiri imemfungua akili safi sana Jf....ila nilichogundua kwenyenjamii kuna wanaume wengi wenye matatizo ya aina hii ila hawapo tayari kutazungumzia na wakati mwingine huishia kufanya maamuzi yasiyostahili,au kupanda mahakamani na kukosa haki zao
 
Back
Top Bottom