ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,938
- 6,942
Ndugu zetu Wakenya,
Tunawaalika mfuatane nasi katika matukio muhimu sana ya wikiend hii hapa Tanzania. Matukio yote yatakuwa mbashara Azam sports HD, king'amuzi bora east and central Africa.
Leo 28.08.2020 jioni uwanja wa uhuru, watu zaidi ya 20,000 watakisanyika kushuhudia ndondi live kati ya Twaha Kiduku vs Dulla Mbabe. Mmoja akiwa mwenyeji wa dsm na mwingine wa mji kasoro bahari Morogoro.
Kesho 29.08.2020 itakuwa ni hekaheka za kukamilisha wiki ya mwananchi. Siku nzima itakuwa busy sana, picha na shughuli mbalimbali za kijamii. Yanga wiki hii imeishika nchi hakika.
Kesho kutwa 30.08.2020 kutakuwa na matukio makubwa mawili. Tukio la kwanza litakuwa ni mchezo mkali wa ngao ya hisani kati ya simba sc na Namungo fc, utapigwa uwanja wa sheikh Amri Abeid pale Arusha town. Kama kawaida wakazi wa Arusha, Moshi na Manyara wataujaza uwanja.
Baadae ni kuhitimisha wiki ya mwananchi ambapo Yanga Sc itatambulisha mashine mpya za kampa kampa tena, na baadae mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na timu ya Burundi. Yanga wataujaza uwanja kwa rangi za njano na kijani, rangi za madini na utajiri wa mimea wa Tanzania. Matukio yote yatakuwa mbashara.
Tunawakaribisha maana corona imewachanganya mmesahau hata burudani ni kitu gani. Jifunzeni kwa mkubwa wenu.
Picha mbalimbali tutawatumia. Stay tuned brethrens