Habari Jf!
Siku ya leo tarehe 25.10.2015 ni siku ambayo watanzania tunafanya maamuzi mazito kwa maslai ya nchi yetu.
Kwa hali ilivyo leo ni tofauti kabisa na matarajio ya wananchi wengi. hali ya usalama ipo vizuri sana, nchi imetulia kimya. mitaani unasikia kelele za ndege tuu na wala si mabomu kama wengi walivhotarajia.
Nadhani hata yale magari waliyonunua 777 hayana kazi katika uchaguzi huu. Ila sijasema ni matumizi mabaya ya hela za walipa kodi.
Kwa suala ya usalama hongera sana mheshimiwa Rais.
Ila upande wa pili wa hili zoezi kuna dosari za kura feki kukamatwa kila pande ya nchi pamoja na majina mengi ya wapiga kura kutokuwepo kwenye daftari.
Hili la kukamatwa kwa kura feki vipi mbona mheshimiwa upo kimya na tume nayo ipo kimya?
Naomba hili la majina kutokuwepo kwenye daftari wakati watu wanavitambulisho halali lifanyiwe kazi haraka lisitutie dosari.
Ukitatua haya mawili mkuu nadhani utaipa nchi yetu heshima kubwa sana kimataifa. Hata kina Paul Kagame wataamini democracy tunayoihubiri Tz ni ya kweli kabisa.